Machapisho

TWENDE NA TIMU KWENYE UCHAGUZI WA CWT 2025

*Na mwandishi wetu* *Sir PANCRAS MAHELA* *From SONGEA MC* *0767549833/0786549833* *VIONGOZI NA TIMU ZAO ZA KAMPEINI* Ngoja tuongelee kidogo hizi timu za kampeni mwaka huu nimezipenda sana hasa hapa *KAHAMA MJINI* Zamani ilizoeleka kamati yote ya uendeshaji inasafiri pamoja hawataki mtu mwingine aivuruge kiukweli hapa ilikuwa ngumu sana kuimega ila miaka ya hivi karibu hapa kahama mwenyekiti ana msafara wake *Ke* anakundi lake *Vu* anakundi lake na *Ki* anakundi lake hapa zinapigwa siasa safi tulipokuwa kata ya mwendakulima Jana pale mgodini kabla ya kuingia kahama MJINI walimu walikuwa na shauku kubwa kumsikiliza mgombea alifika ila sasa tulicholalamika wengi mgombea Ali *select* mwakilishi tu kuzungumza naye kana kwamba huyu mwakilishi amebeba Mawazo ya walimu wote poa najua kupunguza maswali na muda ila mkishinda mje kama mnavyopita sasa hivi kutusikiliza matatizo yetu halafu myafikishe kwa mwajiri wetu. *Wawakilishi nawaomba msiwaombe* *chochote hawa wagombea* Uongozi ni d...

UCHAGUZI WA CWT 2025

Imeandikwa na:- Mwl PANCRAS MAHELA PHONE NUMBER:- 0786549833/ 0767549833 FROM SONGEA MC TZ *KAMPENI* *ZA* *CHAGUZI* *CWT* *2025* *TZ* Awali ya yote nianze kuwapongeza waasisi wa chama cha walimu TZ kwa kuweka muda maalumu wa uongozi na kutengeneza misingi ya kidemokrasi ya upatikanaji wa viongozi wake kote nchini kwa ngazi ya shule hadi Taifa. *MINYUKANO* *NGAZI* *YA* *WILAYA* Katika sehemu kubwa yenye minyukano na hekaheka basi nikuanzia ngazi ya wilaya muda wa kuchukua form ulikuwepo wakutosha na watu wamejitokeza sana japo mwaka huu tulitegemea ushindani mkubwa japo watu wetu wengi wazuri wajiondoa kwenye makato na kupelekea kukosa sifa za kugombea poleni sana mliofanya hivyo na hongereni kwa uamuzi wenu. Nijikite kwenye hizi kampeni, wawakilishi ngazi ya shule nyie ndiyo mapilato wa hili zipo nafasi nyeti tano ngazi ya wilaya ambazo viongozi wake wanatakiwa kuwa na muono wa hali ya juu siyo kuchaguana kirafiki au kishkaji au kwakuwa huyu mwanetu akishinda tutakunywa naye ...

LEO TUANGAZIE MAANA HALISI YA MUZIKI NA JINSI JAMII INAVYOLICHUKULI

UTANGULIZI kuna wanazuoni wengi ambao wamefasili maana ya mziki kwa ujumla wake aidha kwa mtazamo na zama walizonazo na mazingira yao kama ifuatavyo Kamusi ya Webster II ya New Riverside University inatafsiri muziki kuwa ni Sanaa ya kupanga sauti katika mtiririko maalum ili kutengeneza muundo endelevu. Kamusi ya Oxford toleo la 7 inafafanua; muziki ni sauti zilizopangiliwa vizuri kiasi ambacho zinafurahisha kusikiliza. Inaendelea kusema watu wanaweza kuimba muziki au kuupiga kwa kutumia ala za musiki. aidha katika majadiliano na baadhi ya watu majukwa kwenye jamii wanaeleza maana ya muziki kuwa muunganiko wa sauti zinazotoka kwenye ala sauti na maneno ya binadamu yakiwa na mpangilio maalumu @Siza jonathan kwa madai yake aaneleza dhana hii kuwa yeye amezaliwa na kukua pamoja na wanamziki kanisani ndio maana anaeleza hayo Muziki ni kitu kipana sana na huweza kufafanuliwa kwa jinsi tofauti tofauti, maana mbalimbali zimeweza kutolewa na wataalam mbalimbali na maana zote hizi zina ml...

MTOTO YESU KAZALIWA

Picha
Sikiliza kutoka kwa wanakwaya hawa wabunifu

UCHAMBUZI WA SHERIA ZA KAZI NA MASLAHI YA MTUMISHI KATIKA UTUMISHI WA UMA

TWENDE SAWA NA MCHAMBUZI WETU TUKIREJELEA KANUNI ZA UTUMISHI WA UMA NA MAHUSIANO KAZINI -------------------- *kwenye utumishi wa umma kuna posho zifuatazo:-* 1.posho ya kujikimu(subsistence allowence) 2.posho usumbufu(distabance allowence) 3.Takrima(entertainment allowence) 4.posho ya kukaimu(acting allowence) 5.posho ya kazi maalumu) 6.posho ya mavazi(outfit allowence) 7.posho ya masaa ya ziada na kazi za ziada(overtime and extra duty allowence) 8.posho ya kilometa(kilometers allowence) 9.posho ya kikao(settings allowence) 10.posho ya mimba(housing allowance) 11.posho ya sare(unform allowence) 12.posho ya jeshi la polisi na magereza, huduma za zimamoto na uokoaji(police force and prisons,fireand rescue service allowence) 13.posho ya kukaimu; sehemu G( maintenance allowence)- section G N.k *Rejea kwenye kanuni za kudumu za Utumishi wa umma(standing order)L2* *NiPo* SHERIA ZINAZOSIMAMIA UTUMISHI WA UMMA, HAKI NA WAJIBU WA MTUMISHI WA UMMA 2.1 Utangulizi Katika mad...

FAHAMU VIKEMBE AU VIZALIA VYA WANYAMA MBALIMBALI

1.Bata – Kiyoyo 2.Ndovu – Kidanga 3.Nyani – Kigunge 4.Mbweha – Nyamawa 5.Fisi – Kikuto 6.Chui – Kisui/chongole 7.Simba – Shibli/Kibuai 8.Sungura – Kitungule 9.Punda – Kihongwe 10.Ngamia – Nirihi/Nirigi 11.Kondoo – Kibebe/Katama 12.Mbuzi – Kimeme/kibuli 13.Mbwa. – Mbwa/kidue/kilebu 14.Nguruwe – Kivinimbi 15.Farasi – Kitekli 16.Ndege/nyuni – Kinda 18.Paka – Kipusi/Kinyaunyau 17.Ngombe – Ndama 19.Chura – Kiluwiluwi 20.Samaki – kichengo 21.Mamba – Kingwena 22.Nyangumi – Kinyangunya 23.Papa – kinegwe 24.Nyoka – Kinyemere 25.Nzige – Kimatu/matumatu/funutu/tunutu/maige 26.Kipepeo – kiwavi 27.Nzi – Buu 28.Nge – kisuse 29.Nyuki – Jana 30.Mbu – Kiluwiluwi 31.Binadamu – Atifali/mwana

PITIA HII

Picha

UMISETA TANZANIA WATEMBELEWA NA WAWAKILISHI WA FIFA

Picha
wawakilishi toka fifa wakagua vipaji UMISETA mkoani tabora

MAELEKEZO YA KIKAO CHA MKURUGENZI WA ELIMU (DEA) NA WALIMU-BARIADI

*KIKAO CHA MKURUGENZI WA ELIMU (DEA) NA WALIMU-BARIADI (TC & DC) 18/06/2024* _Both organizational goals and individual goals should go parallel_ *Changamoto zilizobainika kutoka kwa Walimu* 1. Madaraja 2. Madai: mapunjo, uhamisho, likizo..... *Kazi Msingi za Mwalimu* •Malezi •Utoaji maarifa *Malezi* -Kuwajibika katika kuwalea watoto/wanafunzi. Kwa moyo wa dhati pasi na kukata tamaa. -Wajibu huu uwe kwa wanafunzi, jamii, mwajiri na taifa zima. -Shule salama. Uwepo wa masanduku ya maoni -Kuzungumza na wanafunzi juu ya vitendo kama (Ubakaji, ulawiti.....) *Utoaji wa maarifa (Taaluma)* -Kufundisha kwa hatua na dhati ya kweli -Mwalimu aliyejiandaa na anayeandaa -Mwalimu anayebadili mtazamo -Kuwatia moyo wanafunzi katika ujifunzaji _"Mwalimu bora ni anayemwezesha mwanafunzi na mwanafunzi ameweza"_ *Maelekezo ya Katibu Mkuu* 1. Ustawi wa Walimu (Chakula kazini, motisha stahiki....) 2. Viongozi watoe maelekezo kwa staha (Lugha ya staha) 3. Kutii na kuheshim...

WALIMU WAKUU WILAYANI MPWAPWA WAPATIWA MAFUNZO YA MATAALA ULIOBORESHWA

Picha
PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI ZIMECHUKULIWA NA MWANDISHI WETU CHRISPINE KIHOMBO KUTOKA MAKTABA YA OFISI YA UKAGUZI MPWAPWA href="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEirtD76Q3PzXcX61uYQXq2QciExHoHXRVNlocYlSP6j9DuoCWhsum-k-PQnXn6hnUWRRhCwxO6u58lJSAhLY1_p7LuGA6n_OqR5i9MUjqqME9xNIa5dJApynhvMouCaSX190GHGUiwbhNI4eg5a1Jt0CpoAOsXnZizFjf-gN_aBwnkNM5-jCIhOI4gKgks/s1600/IMG_20220928_100543_489.jpg" style="display: block; padding: 1em 0; text-align: center; "> matukio mbalimbali katika mafunzo ya mtaala ulioboreshwa kwa walimu wakuuu wilayani mpwapwa

WALIMU WAKUU MKOA WA DODOMA WAPATOWA MAFUNZO YA UONGOZI

Picha
imeandikwa na Thenyota chriss serikari ya ya rais mama SAMIA SULUHU HASANI katika kuboresha usimamizi wa kielimu kupitia wakala wa maendeleo ya uongozi wa elimu ADEM wametoa mafunzo hayo kwa siku tatu mkoani dodoma kwa makundi muda wa siku tatu kila kundi na kuwajengea uwezo wa uongozi walimu hao kufanya kazi kwa ari zaidi aidha muda wote wa mafunzo ambayo mpaka sasa yanaendelea washiriki wana utulivu zaidi ili kupata maarifa hayo. mafunzo hayo yataisha siku ya jumatano tarehe 04/10/2023 usisahau kulike na kusubscibe toa maoni yako

CHAKUHAWATA NI QNET ILIYOCHANGAMKA

CHAKUHAWATA NI QNET ILIYOCHANGAMKA. Na Thadei Ole Mushi. Juzi niliandika kuwa Chakuhawata ni mchongo wa wahuni wengine waliopo mjini, wakanipigia simu wakaniambia Koma kama kocha wa Simba Robentihno alivyokoma kumtoa Chama. Ninachojua mimi kumkata mwalimu maokoto ya 5,000 kila mwezi ni kumlagai Mwalimu tu ili aingie kwenye 18 na watu waanze kuokota maokoto na kutokomea kusikojulikana. Kwa vyovyote vile kama wanataka kuja kuwa chama cha kweli cha kutetea maslahi na haki za waalimu hawataweza kukiendesha chama hicho kwa shilingi 5,000 kwa kila mwalimu kukakatwa kila mwezi. Hesabu hazidanganyi. Kwa mujibu wa Takwimu zilizopo jumla ya walimu wote nchini Msingi na Sekondari wapo 258,291. Fuata link kupata taarifa za takwimu za walimu:- http://demo8.eganet.go.tz/tsc/statistics MAPATO YA CHAKUHAWATA. Chakuhawata wanakata 5,000 kwa kila mwalimu, tuseme sasa walimu wote wamejitoa wamejiunga nao hivyo ni 5,000 X 258,291 X 12 (Miezi) unapata jumla ya 15,497,460,000 (Bilioni 15.4) hapa...

CHAKUWAHATA NA 5000 YAKO

*Je, Tsh. 5000/- inatosha kuendesha Chama Cha Wafanyakazi?* *Utangulizi* Makala haya yanalenga kujibu swali Hilo, ikiwa ada ya 5000 inatosha kuendesha Chama Huru Cha Wafanyakazi, kwa misingi ya kazi adhimu za Vyama husika. *Dhana ya Vyama Huru vya Wafanyakazi* Chama Cha Wafanyakazi Ni umoja wa wanachama, wanaoamua kuja pamoja kwa ajili ya kulinda na kutetea haki na maslahi. Hata Hivyo, nchi nyingi katikati ya majangwa ya Murzuq na Red, kulinda haki na maslahi si kazi ndogo, kwa kuwa, kazi ya Kwanza Ni _kulinda ajira zenyewe na hadhi yake_. *Kazi za Vyama Vya Wafanyakazi Ni Zipi?* Kwa muktadha wa Tanzania, na Afrika kwa ujumla, Chama Cha Wafanyakazi kinatarajiwa kufanya yafuatayo na ziada;- i) Kuwaunganisha Wafanyakazi wa kada husika wawe kitu kimoja. ii) Kuwawakilisha wanachama wake kwenye majadiliano Kati yao na mwajiri, eneo walipo, wilayani, mkoani na Taifa. Lakini inakwenda mbali zaidi, kwa kuwa dunia Haina visiwa kwa mantiki ya ajira, Wafanyakazi wa Tanzania wanapaswa ku...

KAIKA KUELEKEA MEI MOSI 2023 KILIO CHA WALIMU KIPO HAPA

WARAKA KWA SERIKALI KUHUSU WAALIMU, SERIKALI IWAJALI WALIMU Ni muda sasa umepita kukiwa na manung'uniko kwa walimu katika nyanja nyingi zinazohusu maslahi yao ikiwemo mishahara yao, stahiki zao na kunyima haki na kuonewa na kuchukuliwa kama watu wa shida na kila kiongozi. Kuna haja serikali kumwangalia mwalimu kwa jicho la tatu, walimu wanapitia wakati mgumu sana katika utendaji kazi wao. Nimejaribu kuorodhesha changamoto hizi ambazo kama serikali ikizitatua hasa katika bajeti ijayo, ili mwalimu naye aone faraja ya maisha Baadhi ya changamoto hizo ni; MISHAHARA Serikali ipitie a iboreshe kwa mapana mishahara ya walimu, suala hili limekuwa tatizo kwa muda mrefu ikiwa kuna manung'uniko makubwa juu ya mishahara kiduchu wanayopewa waalimu Mara kwa mara tumekuwa tukisikia "mama anaupiga mwingu" kwenye Elimu, lakini ukichunguza kwa kina na kwa mapana na hata ukiwasikiliza wanaosema hivyo wanaishi kutaja vyumba vya madarasa na mabweni au katika miundombinu tu, huwezi ...

WALIMU WA MPWAPWA WASHUKURU HALMASHAURI YA BAHI KWA MAWAZO YA KUINUA UFAURU

Picha
Katika kikao chao ambacho walimu wa mpwapwa waliomba kujifunza mbinu za kuinua taaluma ikiwa ni lengo la kuifanya dodoma mpya ya kielimu aidha katika hali isiyo ya kawaida walimu wameshangaa Bahi walivyoweza kushirikiana katika suala la kielimu kwa pamoja ikiwa kuanzia wazazi na viongozi wote katika idara mbalimbali. kwaherini bahi karibuni mpwapwa mwakani mtajifunza kwetu pia.

WALIMU WA MPWAPWA WAFANYA ZIARA YA KUJIFUNZA WILAYANI BAHI UNGANA NAMI KATIKA MATUKIO

Picha
matukio ya awali katika ukumbi. tumekaribiswa vzuri sana

YANGA WASHAONDOKA TAYARI

Club ya Yanga SC kwenda Tunisia leo Feb 7, 2023, Afisa habari afunguka haya “Tuna Wachezaji 25” February 7, 2023 Share 1 Min Read Club ya Yanga SC inaondoka leo kuelekea Tunisia kwa ajili ya kuanza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika US Monastir. Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe amesema Timu itaondoka na kikosi cha Wachezaji 25, Aboutwalib Mshery atasafiri na Timu kwa ajili ya kwenda Tunisia kupatiwa matibabu wakati Bernard Morrison atabaki Dar es Salaam akitibiwa nyonga. “Tuna Wachezaji 25 katika kikosi chetu lakini hawa 25 yupo pia Aboutwalib Mshery, Mshery anakwenda Tunisia kwa ajili ya matibabu”

MAANA YA SEMANTIKI, MAANA YA MAANA

Picha
15.1  Utangulizi Katika muhadhara huu, tunakusudia kuelezea semantiki. Awali neno semantiki lilitumika kumaanisha sayansi ya “maana” kwa ujumla, hivi kwamba ilishughulikiwa na wanafilosofia, wanasaikolojia, wanamantiki, wanaanthropolojia na wengineo. Baadaye stadi hii ilijishughulisha zaidi na maana katika muktadha wa mwanadamu. Katika muhadhara huu tutashughulikia semantiki katika muktadha huu yaani maana katika misingi ya kinadharia ya isimu. Madhumuni ya Muhadhara Baada ya kumaliza kusoma muhadhara huu, mwanafunzi ataweza: (i)     Kueleza maana ya maana (ii)   Kuainisha aina za maana (iii)  Kueleza na kutofautisha uhusiano wa maana (iv) Kueleza dhana ya maana kiutendaji  15.2 Maana  Neno maana linafahiwa nyingi. Watu wa kawaida wamelitumia kumaanisha vitu mbalimbali: Una maana gani kwa kufika umechelewa Yale mawingu meusi yana maana mvua itanyesha sasa hivi Hiyo nguo nyekundu inamaanisha hatari Mradi huu una maana kubwa “Baba” maana ...