UCHAGUZI WA CWT 2025
Imeandikwa na:-
Mwl PANCRAS MAHELA
PHONE NUMBER:- 0786549833/ 0767549833
FROM SONGEA MC TZ
*KAMPENI* *ZA* *CHAGUZI* *CWT* *2025* *TZ*
Awali ya yote nianze kuwapongeza waasisi wa chama cha walimu TZ kwa kuweka muda maalumu wa uongozi na kutengeneza misingi ya kidemokrasi ya upatikanaji wa viongozi wake kote nchini kwa ngazi ya shule hadi Taifa.
*MINYUKANO* *NGAZI* *YA* *WILAYA*
Katika sehemu kubwa yenye minyukano na hekaheka basi nikuanzia ngazi ya wilaya muda wa kuchukua form ulikuwepo wakutosha na watu wamejitokeza sana japo mwaka huu tulitegemea ushindani mkubwa japo watu wetu wengi wazuri wajiondoa kwenye makato na kupelekea kukosa sifa za kugombea poleni sana mliofanya hivyo na hongereni kwa uamuzi wenu.
Nijikite kwenye hizi kampeni, wawakilishi ngazi ya shule nyie ndiyo mapilato wa hili zipo nafasi nyeti tano ngazi ya wilaya ambazo viongozi wake wanatakiwa kuwa na muono wa hali ya juu siyo kuchaguana kirafiki au kishkaji au kwakuwa huyu mwanetu akishinda tutakunywa naye hapana chagua kwa maslahi ya walimu kwenye wilaya yako. Nafasi hizo ni:-
1. *Mwenyekiti* *wa* *wilaya* huyu ndiye msemaji wa chama kwa wanachama usimchague mtu kisa upo Jilani naye no chagua jembe ambalo litaisaidia wilaya yako kwenye utatuzi wa changamoto za walimu kuanzia ngazi ya shule siyo kidogo hadi afisa elimu aje au afisa utumishi au Mkurugenzi yapo mambo ambayo mwenyekiti na watu wake wanaweza kuja kwenye shule na wakayachukua na kumfanya mwl abaki kituoni akijua changamoto Yake inafanyiwa kazi na kurudishiwa majibu stahiki. Wengi wao hawakuwa wakifanyahivyo wakiupata uenyekiti tu basi sasa wakati wa kuwaondoa ndiyo huu.
Nitahadhalishe hapa matumizi ya Pesa huwa ni makubwa kwaajili ya kuinunua haki piga chini mwenyekiti anayetaka kutengeneza mazingira ya kutaka kukupa rushwa ili umchague baada ya ushindi wake mtu anayetumia rushwa harudi kwa wanachama tena, nakinabaki kilio kwa wanachama kusema Cwt ni mbovu kumbe mwakilishi wako alichagua viongozi kwa interest ya zake. *Kemea* *Rushwa*
Naongeza kitu tena viongozi w Cwt Mkoa nchini nzima nyie nyamazeni waachieni watu wa wilaya waamue kwenye wilaya yao usimsapoti kwa Pesa mgombea yoyote maana atakayeshinda ni mwalimu mwenye ushawishi kwa wanachama nyie tulieni dawa yenu inakuja mwezi ujao.
Naamini wapo viongozi ambao hamtamani kutoka madarakani yaani hamtamani hata kufanyika kwa uchaguzi lakini tulieni hivyo hivyo mfano wewe kiongozi wa Mkoa unatokea wilaya ya Kaliua unataka Ku monitor uchaguzi wa Nzega inakuhusu nini? Waachie watu wa Nzega waamue baadaye watakuja mkoani watakuamua na wewe, kwani wewe wasiwasi wako upo Wapi tulia usiingilie uchaguzi wa watu katika Halmashauri yao.
2. *Mweka* *Hazina* *wa* *wilaya* huyu ndiye anayeongezeka kutengeneza utatu wa Halmashauri husika yaani m/kiti, katibu na mhazini hawa sikuzote lao moja kwa uzoefu wangu bora watoke kwenye kambi mbili tofauti ukikuta mgombea wa uenyekiti anakuambia mweka hazina mpeni Fulani hilo linaenda kuwa genge la wapigaji waliokuwa na interest zinazofanana hapo kinachofaa timu A itoe mwenyekiti timu B itoe mweka hazina collaboration Yake inakuwa safi sana , ikumbukwe huyu ndiye anayelipa 15% ya mahali pa kazi hatakiwi kuwa mtu wa kulaumiwa na kuwa mtu wa kutiliwa mashaka mtu kwelikweli.
3. *KATIBU KITENGO KE* huyu ni mwanamke mwalimu anayeratibu mipango yote ya walimu wanawake kwenye Halmashauri huyu anamiliki Pesa za kitengo hiki zinazorudi kutoka Cwt makao makuu kusaidia walimu wanawake muulize katibu wake Pesa za miaka 5 iliyopita alifanyia nini kabla hujamchagua tena mwalimu kajifungua, kafiwa na mume, kaachwa kwa dharau na mume kwa kunyang'anywa kila kitu je katibu alipopata taarifa alikuja kumtia moyo kwa asilimia chache ya Pesa ya kitengo hiki ? Hawa makatibu wanamezwa sana na makatibu wa Cwt wilaya na mwenyekiti wa wilaya huyu anastahili kuadhibiwa kwenye boksi la kura kama alikuwa haeleweki.
4. *Mwakilishi wa walimu walemavu* huyu mwamba anakuwa na tu % tuchache kutokana na walimu kwenye ulemavu kwenye Halmashauri Yake ila hawa pia hawana nguvu sana za kimaumuzi kutokana na kukosa mafungu Mara nyingi huishi kwa kusubiri hisani ya mwenyekiti au katibu wa wilaya awaambie fanyeni hivi mwangalie wako kama anafaa MPE ila kama kakaa zaidi ya miaka 10 pigs nchini kura MPE mlemavu mwingine
5. *Mwakilishi wa walimu vijana* huyu anatakiwa kuwa wa moto unteachable wanyasa wanasema hivyo kama mwakilishi wako ndani ya miaka 5 alikuwepo kuwepo tu hata wewe uliyempigia kura umeanza kumsahau jina piga chini hakuna mtu hapo yeye ndo catalyst ya chama anafanyakazi hata ambazo katibu hajamtuma yaani mwalimu ikipiga chafya kata ya *mwanjolo* meatu huko basi yeye *mwandoya* anataarifa pakiwa na matumizi ya hovyo ya fedha yeye wakwanza kuhoji .
Itaendelea jioni ya Leo elimu ya fedha za Cwt.
Mwakilishi amka usivirigwe virigwe unapouendea mkutano Mkuu hapa ndo kuna madudu
Maoni
Chapisha Maoni
Tafadhari usicomment matusi