CHAKUWAHATA NA 5000 YAKO
*Je, Tsh. 5000/- inatosha kuendesha Chama Cha Wafanyakazi?*
*Utangulizi*
Makala haya yanalenga kujibu swali Hilo, ikiwa ada ya 5000 inatosha kuendesha Chama Huru Cha Wafanyakazi, kwa misingi ya kazi adhimu za Vyama husika.
*Dhana ya Vyama Huru vya Wafanyakazi*
Chama Cha Wafanyakazi Ni umoja wa wanachama, wanaoamua kuja pamoja kwa ajili ya kulinda na kutetea haki na maslahi.
Hata Hivyo, nchi nyingi katikati ya majangwa ya Murzuq na Red, kulinda haki na maslahi si kazi ndogo, kwa kuwa, kazi ya Kwanza Ni _kulinda ajira zenyewe na hadhi yake_.
*Kazi za Vyama Vya Wafanyakazi Ni Zipi?*
Kwa muktadha wa Tanzania, na Afrika kwa ujumla, Chama Cha Wafanyakazi kinatarajiwa kufanya yafuatayo na ziada;-
i) Kuwaunganisha Wafanyakazi wa kada husika wawe kitu kimoja.
ii) Kuwawakilisha wanachama wake kwenye majadiliano Kati yao na mwajiri, eneo walipo, wilayani, mkoani na Taifa. Lakini inakwenda mbali zaidi, kwa kuwa dunia Haina visiwa kwa mantiki ya ajira, Wafanyakazi wa Tanzania wanapaswa kuunganishwa na jumuia ya kimataifa pia. Afrika Mashariki, Mashariki Mwa Afrika, Afrika na Dunia kwa upana wake. Ikimbukwe Tanzania Ni sehemu ya ILO na tunafuata miongozo kadhaa ya jamii ya kimataifa. (Solidarity globally) Uwakilishi unahitaji kuundwa au kushiriki kwenye meza za majadiliano, vyombo na Bodi mbalimbali. Mifano Ni Mabaraza mbalimbali ya Kisekta, na Bodi anuai Kama vile za Ajira, Mishahara,Afya n.k
iii)Kuwatetea wanachama. Hapa Ni kwa masuala yote. Mengine yatahusu kwa mwajiri ngazi husika, Wilaya mkoa na Taifa.
Hii inaweza kufanya Chama kitumie rasilimali zake(Muda, Fedha na Maafisa wake) kufuatilia masuala mbalimbali ya wanachama, na inaweza kuwa Kwa mwajiri au CMA (Mahakama ya Masuala ya Ajira) na Mahakamani kwa ujumla.
iv) Kuwaelimisha wanachama wake. Ni nadra sana, kwa mwajiri kutenga muda na rasilimali zake Kuwaelimisha waajiriwa juu ya _haki na maslahi yao_
Kimsingi, mwajiri anahitaji tu kuajiri au kupata mtumishi ambaye ana afya,anafahamu majukumu yake, Anajituma na ana nidhamu ya kazi, basi.
v) Kufanya tafiti mbalimbali zitakazotumika kuwanufaisha wanachama wake, aidha moja kwa moja, au kupitia kumshawishi mwajiri kuboresha mazingira ya kazi pia maslahi na stahiki za watumishi.
Tafiti Kama vile juu ya ujira, hifadhi ya uzeeni na umuhimu wa motisha hazikwepeki. Kufanya tafiti hizi, kwa ubora wake, kunaweza kulazimisha kutengeneza mikataba ya kuwatumia wanazuoni, walio nchini na nje, ili matokeo ya tafiti hizi, yawe ya kuamini, juu ya mstari wa mashaka k.v Methodology, Analysis Procedures n.k. Ikumbukwe kuwa walaji wa mwisho wa tafiti hizi Ni wanazuoni na wazoefu wa masuala ya Ajira, ambao wanafanya kazi k.n.y mwajiri. Huwezi kuwalisha kitu kisichoiva.
vi) Vyama pia vinatarajiwa kutoa huduma ndogondogo za kijamii. Hii Ni kwa wanachama na pia kuhusu CSR. Vyama vinapaswa kuchangia masuala mtambuka yanayoigusa jamii
pia. Hili sio la hiari.
vii) Chama makini kinatarajiwa pia kuwaendeleza wanachama wake kitaaluma na utaalamu.
Hapa sio lazima kuwalipia ada. Lakini kuwa na mafunzo ya Mara kwa Mara yanayolenga kuwafanya waipende kazi yao kwa kuiona rahisi.
viii) Vyama pia vinajihusisha kuhakikisha usawa, na haki za kijinsia zinahakikishwa kuwepo na mwajiri. Hii Ni pamoja na kuchechemua upatikanaji wa huduma kwa makundi maalum na yenye mahitaji.
*Je, Tsh. 5,000/- inatosha*
NDIO, Kama tu Chama hakina *Majukumu, Sera Wala maono* kukihusu.
a) Ikiwa kazi kubwa ya Chama Ni kununua tu mkoba( 💼 ) na ndio Ofisi ya Wilaya, Basi haya 1,000/- inatosha.
-Ikiwa Chama hakikusudii kuwa na Manpower(kuajiri) itakayokuwa na majukumu ya kukutana na wanachama, kuwasikiliza, na kutatua shida zao, Basi elfu 5 pia Ni nyingi mno.
- Ndio Ikiwa Chama kitajiendesha Bila kuwa na vikao, Wala mikutano, na Hivyo kuwa na watu waliojichagua wenyewe, wanaotumia nafasi zao za kujiteua, kuteua wenzao, kukaimu ofisi nchi nzima, huku wakitegemea kulipwa Mishahara na serikali.
-Ndio Ikiwa hukusudii kulipa usafi wa ofisi,(huna) wala ulinzi, maji na umeme.
-Ndio kwa kuwa hununui vitendea kazi vingine Kama meza, kiti, Kompyuta, karatasi, mafuta ya gari Wala wino wa printa.
-Ndio Kama mwanachama wako akipata shida, ndogo au kubwa, hajui pa kukupata, na Wala hujihushishi.
-Ndio Kama kazi yako kubwa Ni *kusajili na kuingiza makato tu ya ada* na humwakilishi mteja wako popote.
-Ndio Kama wanachama wako hawana mahali pa kuja kukulamikia shida zao.
-Ndio Kama huna gari la kufanyia matengenezo baada ya kutoka ziara.
-Ndio Ikiwa tu, huna mpango wa kufuata katiba yako, kwa maana ya kutokufanya mikutano na vikao vya kikatiba.
-Ndio, Ikiwa tu mwajiri atakubali udumu daima dumu katika mazingira ya kuvunja Sheria za Kazi, Ikiwa Ni pamoja na utoro kazini kwa kukosa Waajiriwa wako mwenyewe kutenda kazi za Chama.
-Ndio Kama tu Chama hakikusudii kuwa Huru, kwa maana ya kuwa, Kama Chama kinategemea kutumia rasilimali za mwajiri, watumishi wa mwajiri, muda wa mwajiri, Basi *hakitegemei kumsimamia mwajiri*
b) *HAPANA*
- Elfu 5 haitoshi Ikiwa tu, unakusudia kutekeleza majukumu yako yote kwa mujibu wa Sheria za Kazi na Katiba mliyojitengenezea.
- Haitoshi Ikiwa mtaajiri watumishi halali wa kuwahudumia wanachama wenu kila wakati wanapohitaji.
-Haitoshi Kama mna makusudi ya kuelimisha wanachama wenu kwa undani kwa kuwafuata mahali pa kazi, au kuwakusanya sehemu moja.
-Haitoshi Ikiwa mnakusudia kuwa na ofisi zenye hadhi zilizo na vifaa muhimu kwa ajili ya huduma.
-Hapana asilani, elfu 5 Haitoshi Ikiwa mnakusudia Kuwatetea wanachama wenu CMA, Kwa mwajiri na Mahakamani.
-Kamwe Haitoshi kufanya tafiti muhimu. Haitoshi hata tafiti moja.
*Hitimisho*
Kuanzisha Chama Cha Wafanyakazi, kwa msingi wa Ada ya elfu 5, na kuwadanganya Walimu kuwa ndio suluhu ya matatizo yao, Ni WIZI wa mchana.
Hii Ni kwa kuwa, toka Vyama vyenye mtazamo huo, vianzishwe, havijawahi kumsaidia hata Mwalimu mmoja, wa mfano, Wala kumtetea popote.
Kazi kubwa imekuwa Ni kuikosoa CWT. Ukiwauliza Kama CWT Ina kasoro, ninyi mpango wenu wa muda mfupi na mrefu katika kuwasidia Walimu Ni upi, hawana.
Wa muda wote Ni kuisema tu CWT. Ndio master plan wanayoishi nayo.
Natambua kuwa CWT inaweza kuwa na udhaifu kwenye maeneo kadhaa, kwa kuwa hakuna taasisi isiyo na kasoro duniani. Ila,
Ukweli Ni kuwa, CWT(Katika ubaya inayosemwa nao)bado *Ni Bora Mara 10*, ( _Ten folds_) ya hivi Vyama Vya kwenye briefcase.
Comments
Post a Comment
Tafadhari usicomment matusi