LEO TUANGAZIE MAANA HALISI YA MUZIKI NA JINSI JAMII INAVYOLICHUKULI
UTANGULIZI
kuna wanazuoni wengi ambao wamefasili maana ya mziki kwa ujumla wake aidha kwa mtazamo na zama walizonazo na mazingira yao kama ifuatavyo
Kamusi ya Webster II ya New Riverside University inatafsiri muziki kuwa ni Sanaa ya kupanga sauti katika mtiririko maalum ili kutengeneza muundo endelevu.
Kamusi ya Oxford toleo la 7 inafafanua; muziki ni sauti zilizopangiliwa vizuri kiasi ambacho zinafurahisha kusikiliza. Inaendelea kusema watu wanaweza kuimba muziki au kuupiga kwa kutumia ala za musiki.
aidha katika majadiliano na baadhi ya watu majukwa kwenye jamii
wanaeleza maana ya muziki kuwa muunganiko wa sauti zinazotoka kwenye ala sauti na maneno ya binadamu yakiwa na mpangilio maalumu @Siza jonathan kwa madai yake aaneleza dhana hii kuwa yeye amezaliwa na kukua pamoja na wanamziki kanisani ndio maana anaeleza hayo
Muziki ni kitu kipana sana na huweza kufafanuliwa kwa jinsi tofauti tofauti, maana mbalimbali zimeweza kutolewa na wataalam mbalimbali na maana zote hizi zina mlengo mmoja wa kuufafanua muziki.
Kamusi ya Webster II ya New Riverside University inatafsiri muziki kuwa ni Sanaa ya kupanga sauti katika mtiririko maalum ili kutengeneza muundo endelevu.
Kamusi ya Oxford toleo la 7 inafafanua; muziki ni sauti zilizopangiliwa vizuri kiasi ambacho zinafurahisha kusikiliza. Inaendelea kusema watu wanaweza kuimba muziki au kuupiga kwa kutumia ala za musiki.
Maana zote hizo na nyingine nyingi ziko sahihi kabisa. Kwa upande wangu ninaweza kuuelezea Muziki kuwa ni; sauti za binadamu au za ala za muziki {au zote kwa pamoja} zisikikazo kwa mpangilio maalum na kwa madhumuni maalum; mf; kuburudisha, kuelimisha, kuonya, nk.
Muziki ni kitu chenye nguvu kubwa sana na hivyo kuwa chanzo cha mambo makubwa tofauti kutokea; kwa mfano jeshini nyimbo hutumika sana katika kutia moyo wa kupigana na adui na hatimaye kushinda. Muziki huweza kuleta faraja kwa mtu aliyeumizwa na vitu mbalibali mfano kazini kwake au katika mahusiano yake na marafiki au jamii kwa ujumla.
Katika kitabu chake cha “Jifunze gitaa”, ndugu Lister Nhukuwalla anafafanua zaidi kwa kusema “Muziki ni kitu ambacho huvuta usikivu wa mwanadamu. Maana upigaji wake na upangaji wa vyobo humfanya anayevitumia vimfikishe anakotaka au msikilizaji avutwe na muziki huo.
Katika kuielezea maana ya muziki hapo juu nimesisitiza maneno manne {sauti za binadamu, ala za muziki, mpangilio, na madhumuni } kwa sababu ni ya muhimu sana katika muziki.
Sauti za binadamu; katika muziki sauti za binadamu huweza kupangwa katika mpangilio maalum na wenye kuvutia kusikiliza. Kuna mpangilio wa takriban sauti nne; sauti ya kwanza, ya pili, ya tatu, nay a nne. Sauti hizi zote hupangiliwa kitaalam na hivyo huweza kuleta msikiko mzuri na wa kupendeza masikioni mwa msikilizaji. Kuna mbinu nyingi na nzuri hutumika katika kuzipanga sauti hizi na hivyo kuleta radha nzuri masikioni mwa msikilizaji n ahata mwimbaji mwenyewe. Katika kitabu hiki hatutaangalia kwa undani sana jinsi ya kuimba kwa hivyo kwa uchache utakuwa umepata nini umuhiu wa sauti za binadamu katika kuunda muziki.
Mpangilio; dhana hii ya mpangilio ni pan asana na inahusisha uundaji mzima wa muziki. kwa mfano lazima ujue ni vyombo vya aina gani utavitumia katika muziki wako au wimbo, ni sauti zipi utaimba, pia lazima ujue utapigaje vyombo vyako mfano kinanda au gitaa utavipiga kwa wakati gani, na kwa nidhamu ipi; mfano katika mpangilio wako labda unaweza kuanza kwa kupiga Kodi kuu {Major chord} na kuishia na kodi ndogo {Minor chord}.
Au pia ni jinsi gani mtaachiana nafasi ya kupiga kila chombo katika nidgamu inayoeleweka, kwa mfano wakati waimbaji wanaimba gitaa ya solo inaweza kuwa chini nap engine vyombo vingine vikawa katika hali ya utulivu mkubwa na baadae waimbaji wakinyamaza kuupisha vyombo vya muziki hapo gitaa ya solo inaweza ikapanda kidogo na kusikika likiwaongoza vyombo vingine kama kinanda na besi gitaa. Kwa hiyo mpangilio ni wa muhimu sana ili kuweza kuleta maana inayoeleweka kwa sikilizaji na mwanamuziki mwenyewe pia, pia ni lazima upangilie jinsi korasi au ubeti utakavyoenda katika wimbo na vyombo gani vya muziki utakavyotumia pia.
Madhumuni; dhana hii pia ni ya muhiu sana katika muziki, kila aina ya muziki auimbao tu inakuwa na maudhui nyuma yake, maudhui hayo huweza kutofautiana kutoka muziki mmoja na mwingine kutokana na sababu mbalimbali kama mahitaji ya jamii husika, au kusudi la mwanamuziki wenyewe. Kwa mfano muziki unaweza kupigwa kwa dhumuni la kuelimisha jamii kwa jambo fulani mfano; afya, elimu bora, mapenzi, kusifu nchi. Pia muziki unaweza kuwa na dhuuni la kuchekesha, kumsifu na kumwabudu Mungu, kuonya.
Ala za muziki/vyombo vya muziki; Kuna ala za muziki {vyombo vya muziki}, za aina mbalimbali, na pia huweza kutofautiana kutoka tamaduni moja na nyingine pamoja na mazingira ya watu husika. Kwa sababu kitabu hiki kinaangalia Zaidi chombo kimojawapo cha muziki {kinanda} tutapitia kwa uchache aina nyingine za vyombo vya muziki kwa sababu vina mahusiano ya karibu sana na kinanda.
Kuna makundi manne ya vyombo vya muziki na vimegawanywa kutokana na mlio wa chombo husika
1: Ala za kupuliza {Aerophones}
Kundi hili linahusisha vyombo vyote vinavyotoa sauti kwa kutegemea hewa. Mfano wa vyombo hivyo ni kama tarumbeta, zumari, filimbi, pembe n,k.
2: Ala za kugonga {Idiophones}
Kundi hili linahusisha vyombo vyote vinavyotoa mlio kwa kugongwa na kitu kingine kama chuma, mti n.k. vyombo vinavyoweza kuingia kwenye kundi hili ni kama; Marimba ya mikono {thumb piano} ambayo hupigwa kwa kutumia vidole gumba. Kifaa kingine ni marimba ya vibao ambayo hupigwa kutumia vibao.
3: Ala za kuwambwa {Membranophones}
Vyombo vinavyohusihwa humu ni vile vinavyotoa sauti yake kutokana na mtetemo wa ngozi. Ngoma ndicho chombo kinachoingia sana katika kundi hili; zote ngoma za asili na hata zile za kigeni.
4: Ala za nyuzi {Chordophones}
Ala zinazoingia katika kundi hili ni zile zilizotengenezwa kwa nyuzi ambazo ndizo hutoa mlio. Ala hizo kama; zeze, gitaa, violincello, violin na kinanda cha piano
Maoni
Chapisha Maoni
Tafadhari usicomment matusi