TUNAKUTHAMINI TUNAKUPENDA NI FAHARI YETU KUKULETEA TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA SEHEMU TOFAUTITOFAUTI ZA DUNIA KUWA MJANJA KUPATA TAARIFA MAPEMA
**IJUE DUNIA YAKO MAPEMAAAAAA**
RIWAYA YA KISWAHILI NUKUU ZA SOMO: MAANA YA RIWAYA NA AINA ZA RIWAYA: Riwaya imefasiliwa na wataalamu mbalimbali miongoni mwao nikama vile, Encyclopedia Americana (EA), Jz. 20 (1982:510f) wakinukuliwa naMulokozi (1996) wanasema, riwaya kuwa ni hadithi ya kubuni inayotosha kuwa kitabu. Udhaifu; Maelezo haya yanaibua utata kwani hayafafanui kitabu kinapaswa kuwa na urefu kiasi gani. Matharani kwa mujibu wa UNESCO katika Mulokozi (1996) kitabu ni chapisho lolote lenye kurasa 48 au zaidi. Ama urefu wa kitabu hautegemei idadi ya kurasa tu pia unategemea ukubwa wa kurasa (upana na kina) ukubwa wa maandishi na mpangilio wake. Encyclopedia Britanica EB, Jz.8, (1985:810) wakinukuliwa naMulokozi (1996) wanaeleza kuwa, riwaya ni masimulizi marefu yakinathari yaliyochangamana kiasi, yenye kuzungumzia tajriba ...
Daniel Seni Academia.edu KI 311 SEMANTIKI NA PRAGMATIKI YA KISWAHILI DOWNLOAD 27 Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com 27 Mfano wa maswali; Familia yenu ina watu wangapi? Mbali na Wamasai ni watu gani wengine wanaojihusisha na ufugaji? 2. Matendo uneni yasiyo dhahiri Haya ni matendo ambayo aina ya sentensi haiwiani bali inakinzana. Kwa mfano:- Unaweza kumkopesha shilinga elfu kumi — sentensi hii kimuundo ni swali lakini dhima ni ombi. Kwa hiyo inafanya tendo uneni lisilo dhahiri. Mfano mwingine Njaa inaniuma sana — kimuundo sentensi hii inatoa inatoa taarifa lakini dhima ni kuomba chakula. Kwa hiyo katika muundo huu ni kuwepo kwa muundo tofauti na dhima. Aina za Matendo Uneni Austin (1962) ametaja aina tatu:- 1. Kile kisemwacho Aina hii inahusu usemi wa sentensi yoyote yenye maana inayoeleweka pia iwe na kitu kinachorejelewa. 2. Lengo...
SEMANTIKI NA PRAGMATIKI IMEANDALIWA NA MUBARAKA A HAMAD CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM Maarifa ya lugha ni elimu ya kupambanua vijengo mbalimbali vya lugha na kanuni zake kulingana na taratibu za lugha hio. Ulimwengu halisi ni mukatadha ambao maarifa ya lugha huweza kutumika ili kuleta taathira kama ilivyokusudiwa na msemaji au mwandishi. Richmond Thomason (2012) anafafanua maana ya semantiki kwamba ni tawi la isimu ya lugha linalohusu maana za viyambo vya lugha. Hivyo basi ni kusema kuwa, semantiki ni utanzu wa isimu unaojishughulisha na maana ya maneno au viyambo vya maneno katika lugha. Swali kuu katika wanasemantiki ni kuhusu ninini maana ya maana. Hata hivyo wanasemantiki hujikita katika kuchunguza maana katika viwango mbalimbali kama vile; ngazi ya sauti (fonimu), neno, virai, vishazi na hata sentensi. Tawi hili la isimu limekuwa ni muhimu sana hasa kutokana na umuhimu wa mazungumzo, kwani ili mazungumzo yaeleweke na ujumbe ufahamike panahitajika maana. Aidha nivyema if...
Comments
Post a Comment
Tafadhari usicomment matusi