KI 311 SEMANTIKI NA PRAGMATIKI YA KISWAHILI





Daniel Seni

Academia.edu
KI 311 SEMANTIKI NA PRAGMATIKI YA KISWAHILI
DOWNLOAD

27 Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com 27
Mfano wa maswali; Familia yenu ina watu wangapi? Mbali na Wamasai ni watu gani wengine wanaojihusisha na ufugaji?
2. Matendo uneni yasiyo dhahiri
Haya ni matendo ambayo aina ya sentensi haiwiani bali inakinzana. Kwa mfano:- Unaweza kumkopesha shilinga elfu kumi

sentensi hii kimuundo ni swali lakini dhima ni ombi. Kwa hiyo inafanya tendo uneni lisilo dhahiri. Mfano mwingine Njaa inaniuma sana

kimuundo sentensi hii inatoa inatoa taarifa lakini dhima ni kuomba chakula. Kwa hiyo katika muundo huu ni kuwepo kwa muundo tofauti na dhima.
Aina za Matendo Uneni
Austin (1962) ametaja aina tatu:-
1. Kile kisemwacho
Aina hii inahusu usemi wa sentensi yoyote yenye maana inayoeleweka pia iwe na kitu kinachorejelewa.
2. Lengo la kusema/kunena
Hii inahusu lengo la kile msemaji anachokisema au anachokiongea. Lengo la kile msemaji
anakiongea kinatengeneza tendo uneni. Kwa mfano mwanafunzi anawaambia wenzake ‗mwalimu anakuja‘—
badala ya kuwaambia waache kelele, wanafunzi wanaosikia mwitiko huu wanaweza kuitika tofauti tofauti. Wengine kwa kunyamaza, wengine kuzomea au wengine kuendelea kupiga kelele tu.
3. Matokeo ya kisemwacho
Inahusu athari/matokeo ya kile kisemwacho kwa msikilizaji. Matokeo ya kisemwacho kwa msikilizaji inaweza kuwa iliyokusudiwa au haikukusudiwa. Kwa ufupi aina hii inahusu majibu ya msikilizaji kimwili,kimaneno, kisaikolojia, kiakili nk.
Aina za Matendo Uneni Zilizoboreshwa
John Searle (1975) aliboresha aina za matendo uneni. Katika uboreshaji wake alisema kwamba kuna aina nyingi sana za matendo uneni na labda hazina ukomo. Hii ni kwa sababu aina hizo hutegemea lengo, muktadha na lugha husika. Hivyo akapendekeza aina za ziada za matendo uneni. Baadhi ya aina alizopendekeza ni hizi zifuatazo:-
1. Ahadi
Haya ni matendo uneni ambayo humfunga mnenaji katika utekelezaji wa kile alichokinena kwa siku za baadaye. Mfano wa vitenzi kwa tendo uneni hii ni; tuza, ahidi, zawadi, nk lazima utekeleze.
2. Maelekezo/ Directives
Haya ni matendo uneni ambayo hulenga kuchochea jambo fulani lifanyike na msikilizaji kama atakavyo msemaji. Vitenzi vinavyoweza kutumika ni pamoja na; amrisha, omba, onya, shauri, pendekeza, sihi nk. Kwa mfano; Tunapendekeza jaribio la Pragmatiki lifanyike Alhamisi badala ya Jumatano Nakusihi uachane na kile kivulana chako cha chuo
3. Hisia (Expressive)
Haya ni matendo uneni ambayo hudhihirisha hisia, imani, mitazamo au mawazo ya msemaji juu ya jambo fulani. vitenzi kama vile; shukuru, pongeza, sifu, fariji, samehe nk hudhihirisha. Kwa mfano


28 Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com 28

Nimeamua kukusamehe rafiki yangu

Nashukuru kwa wema wako
4. Matamko
Ni matendo uneni ambayo hunenwa kwake hubadili ukweli fulani wa mambo katika dunia. Vitenzi vinavyoweza kutumika ni kama vile; jiudhuru, achisha kazi, fungua (mkutano), funga (mkutano), hukumu, oza(mke au mume), tangaza, kupa jina nk. Kwa mfano;

Kuanzia leo nimekuachisha kazi

Kuanzia sasa natangaza kwamba Wiliam na Helena ni mume na mke

Naufungua mkutano rasmi, mjisikie huru kuchangia hoja
5. Uwakilisho
Haya ni matendo uneni ambayo hueleza kile ambacho mnenaji haamini kuwa ni kweli au si kweli. Matendo uneni ya aina hii hujumuisha maelezo, shadidia au mahitimisho kwa mfano:-

Lulu hakumuua Kanumba

Wanaume si waaminifu katika mahusiano

Wasichana wa mjini hawana mapenzi ya kweli

Wanaume siyo waaminifu katika mahusiano

Kada yule hatapitishwa na chama chake kugombea urais na chama chake mwaka huu

Yule mwanao wa pili wa kiume ni shoga
DHANA YA UOLEZI
Uolezi ni uoneshaji maalum wa vitu, mahali, watu, hali nk katika muktadha husika wa mazungumzo kwa kutumia maneno (violezi) tofauti na uoneshaji wa kawaida wa kutumia viungo vya mwili hususan vidole. Si rahisi kwa mtu asiyejua muktadha kujua ni kitu gani kinachojerejelewa. Kwa mfano
‘ukija yeye utamkuta pale, itabidi usubiri kwa dakika 40 kisha
tutakwenda kule kuwaona wale tuwarejeshee hiki nao wapate kile
. Hapa maneno yote yaliyopigiwa mstari ni violezi.
Aina za Uolezi
Kuna aina zifuatazo za uolezi:-
1.

Uolezi nafsi
Huu ni uolezi unaotumia viwakilishi vya nafsi. Uolezi huu una violezi sita (6) vinavyogawanyika katika makundi matatu (3) 1. Kundi la nafsi ya kwanza


hapa kuna violezi ‗mimi‘ na ‗sisi‘
2. Kundi la nafsi ya pili
—hapa kuna violezi ‗wewe‘ na ‗ninyi‘
3. Kundi la nafsi ya tatu
—hapa kuna violezi ‗yeye‘ na ‗wao‘
Uchanganuzi wake ni kama ifuatavyo (maana yake) Mimi/sisi-hurejelea wazungumzaji au mzungumzaji. 2.

Uolezi Wakati
Hujumuisha kutambulisha kipindi tamko fulani linatolewa. Uolezi huu hutofautisha wakati wa kutolewa tamko na wakati tamko lilipopokelewa na msikilizaji. Kwa mfano Andika barua yako sasa hivi
o

Tutaenda
kesho



29 Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com 29
o

Seni alizaliwa tarehe ishirini na sita mwezi wa Kumi na Mbili Mwaka elfu moja mia tisa na themanini
o

Nitakuja kwako
Jumapili
ijayo
o

Habari za
asubuhi

o

Pia njeo za wakati katika sentensi huweza kubainisha uolezi wakati. Kwa mfano mwalimu wetu a
li
kuwa a
na
chekesha
3.

Uolezi Mahali
Ni aina ya uolezi ambao huashiria mahali ambapo mawasiliano yanafanyika (Muktadha). Katika lugha ya Kiswahili kuna viashiria kadha wa kadha vinavyoashiria mahali kwa mfano:
hapa, pale, huku, kule, huko, humu, mule nk
4.

Uolezi Uelekeo
Huu ni uolezi ambao hurejelea uelekeo kwa mfano Mbele-nyuma Kulia-kushoto Chini juu nk
5.

Uolezi Jamii
Katika aina hii ya uolezi maana ya tungo hutegemea uhusiano wa kijamii kuweza kueleweka. Uhusiano huo hurejelewa na maneno fulani fulani ambayo hupata maana kamili yanapotumiwa na watu wa kaida mbalimbali katika jamii. Huonesha uhusiano wa aina mbalimbali kwa mfano cheo, hadhi au umri wa msemaji na msiki
lizaji. Kwa mfano ‗ndiyo mzee nimekuelewa!‘ nk

Mahusiano ya Ukweli
Mahusiano ya ukweli yako ya aina mbili:-
Uchopezi Udhanilizi
A.

Uchopezi
Ni uhusiano wa sentensi mbili ambapo ukweli wa sentensi ya pili hudhihirisha ukweli wa sentensi ya kwanza. Kwa mfano; i.

Daniel amemuoa Esther ii.

Esther ameolewa na Daniel Uchopezi ni uhusiano wa sentensi ambapo sentensi moja huchopeza sentensi nyingine. Yaani ukweli wa sentensi moja unahakikisha ukweli wa sentensi ya pili au usikweli wa sentensi ya moja hubeba usikweli wa sentensi ya pili.
Aina za uchopezi 1.

Uchopezi wa kileksia
Ni uchopezi ambao hujitokeza pale ambapo maana ya neno au leksimu moja hujumuishwa katika maana ya neno au leksmu nyingine katika jozi ya sentensi zinazoshughulikiwa; kwa mfano a) Jana nilikuwa machungwa b) Jana nilikula matunda a) majangili yalimuua tembo b) Tembo alikufa.


30 Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com 30
Mfano mwingine ni kama vile; a)

Nilikula mchicha jana b)

Nilikula mboga jana Katika mifano hii neno matunda limechopezwa katika sentensi B. tunasema hivyo kwa sababu machungwa ni aina ya matunda na kama sentensi A ni kweli basi sentensi B pia ni kweli. Kwa ujumla uchopezi wa kileksia hutokea pale ambapo neno fulani katika sentensi moja katika jozi huwa na uhusiano wa kiuhiponimia na neno jingine katika sentensi ya pili katika jozi. Kwa hiyo katika mfano A na B hapo juu neno machungwa katika A ni hiponimia ya neno matunda katika B (Lyons (1977).
2.

Uchopezi wa kisintaksia/Kimuundo
Huu ni uchopezi unaohusisha sentensi mbili zenye miundo tofauti lakini maana yake ya msingi ni ile ile. Mara nyingi hujitokeza katika miundo tenda na utendwa. kwa mfano; a) Mtoto amevunja chupa ya chai b) Chupa ya chai imevunjwa na (mtoto). Ingawa sentensi hizi kimuundo ni tofauti lakini maana ya msingi ni ile ile, kwa maana ya kwamba chupa ya chai imevunjika. Kwa ujumla katika uchopezi wa kisintaksia sentensi moja huchopeza sentensi ya pili lakini katika uchopezi wa kisarufi sentensi mbili huchopezana. B.

UDHANILIZO
Udhanilizo ni mtazamo wa kimaana katika Pragmatiki ambapo mzungumzaji huchukulia kwamba msikilizaji anafahamu taarifa fulani za awali kuhusu jambo linalozungumzwa kabla hujamweleza taarifa mpya. Kwa mfano;-
o

Siku hizi mumeo kaacha kunywa pombe
o

Leo umechelewa na wewe
o

Mtoto amepiga chafya tena
o

Ameacha kuvuta bangi?
Sifa za udhanilizo


Haubadiliki hata pale sentensi msingi inapokanushwa. Kwa mfano
Seni ameingia darasani
au
Seni hakuingia darasani



Haubadiliki hata pale sentensi msingi inapobadilishwa.


Unaweza kubadilika kutokana na uchopekaji, udondoshaji na hata upanguaji
***Mwisho wa mihadhara***
Swali la kazi ya nyumbani ya watu watano watano; Changamoto kuu tano za kushughulikia Semantiki na Pragmatiki
Utangulizi:
Kama ambavyo imebainishwa katika swali kwamba kuchambua maarifa aliyo nayo mwanalugha ni shughuli nzuri lalkini ina changamoto nyingi sana. walau kwa uchache tunabainisha changamoto saba.
Mosi, hifadhi ya maana
. kinachoangaliwa hapa ni mahali ambapo maana ya lugha huhifadhiwa. Wengine wanaamini kwamba maana ya lugha huhifadhiwa na mtumiaji akilini mwake lakini wengine huamini kwamba maana ya lugha huhifadhiwa katika kamusi. Swali la kujiuliza hapa ni kwamba ikiwa maana ya lugha huhifadhiwa akilini mwa mtu iweje mtu aweze kukosolewa kwa madai kwamba kamusi haisemi hivyo? Ikiwa maana inahifadhiwa katika kamusi, je waliotunga


31 Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com 31
kamusi walizipata wapi maana hizo? Je kamusi ina maana ya msamiati wote wa lugha? Na kama neno halipo kwenye kamusi ina maana watumiaji wa lugha hawalitumii neno hilo kwa sababu halina maana? maswali haya yanaonyesha ugumu mkubwa wa kushughulikana na Semantiki na Pragmatiki.
Pili, maana ya maana.
Neno maana, maana yake ni nini? Ni dhahiri kwamba neno maana linadokeza fahiwa nyingi sana. Kuna nadharia nyingi zinazoelezea juu ya maana ya maana. kwa hiyo hakuna maana moja. Jambo hili linaleta ugumu sana katika kushughulika na semantiki na Pragmatiki kwani ni maana ipi ichukuliwe kuwa ndiyo maana ya maana.
Tatu, ufasili wa maana.
katika hoja hii tunachokiangalia ni kwamba tunawezaje kufasili maana ya maneno mbalimbali. Hii inatokana na kwamba kuna urudiaji wa maneno usoukomo. Ili ueleze maana ya neno moja unahitaji kueleza maana hiyo kwa kutumia maneno mengine. Swali, je unajuaje kwamba msikilizaji anajua maana ya maneno hayo? Na je unajuaje kwamba ufafanuzi wako wa kutoa maana ya neno fulani ni sahihi au sisahihi?
Nne, umiliki wa maana.
hapa tunachoangalia ni kwamba maana ni ya nani hasa? Je ni ya msemaji? Na kama ik
iwa maana ni ya msemaji kwa nini inafika mahali msemaji anasema ‗mimi sikumaanisha hivyo?‘ kama maana ni ya msikilizaji, je kwa nini kuna wakati msikilizaji anasema
mimi sielewi unachosema?
Tano, kipashio cha Msingi.
Hapa tunajiuliza maswali kwamba kipashio cha msingi cha semantiki ni kipi? Kuna baadhi ya wataalamu husema kuwa ni neno (jambo ambalo haliwezekani) na wengine husema kwamba hakuna kipashio cha msingi cha kisemantiki. Sasa tunawezaje kuchambua maana pasipo kujua kipashio cha msingi?
Sita, mipaka kati ya Semantiki na Pragmatiki.
Hapa tunachohitaji kujiuliza ni kwamba kuna mpaka dhahiri kati ya semantiki na pragmatiki? Au mipaka iliyopo ni ya kiuchambuzi tu? Je watu wanapozungumza hufikia wakati wanajua kwamba sasa naingia Pragmatiki?
Saba, pengo la Kileksika.
Ni wazi kwamba hakuna lugha yoyote duniani ambayo inajitosheleza kimsamiati kuweza kuelezea kila dhana. Hivyo kila lugha ina pengo la kileksika. Swali la kujiuliza hapa sasa ni je, lugha inapokosa msamiati wa kutaja dhana fulani kuna mbinu gani inatumika kutaja dhana hiyo? Mbinu hiyo nani aliiweka?
Hitimisho
Kutokana na hoja hizo hapo juu ni wazi kwamba si rahisi kujishughulisha na Semantiki na Pragmatiki katika uhalisia wake bali itabaki kuwa katika nadharia tu.
Uchambuzi wa sinonimia
1.

Sinonimia:
inua, nyanyua, nyakua

Utofauti:
Inua ni wakati sehemu tu ya kitu inakuwa juu wakati nyanyua sehemu yote ya kitu inakuwa juu na hakuna sehemu itabaki kuwa chini lakini nyakua ni sehemu yote ya kitu itakuwa juu lakini tendo linafanyika kwa haraka sana.
Ufanano:
zote humaanisha kuweka juu kitu 2.

Sinonimia: Cheo, Madaraka na Wadhifa
Utofauti:
cheo ni ngazi, ajira au madaraka. Ni ngazi ya kimuundo ambayo hutegemea elimu na ufanisi wa mtu lakini madaraka ni nguvu za kiutendaji kazi alizo nazo mtu kutokana na cheo chake lakini wadhifa ni haki inayofungamana na madaraka aliyo nayo mtu kutokana na cheo chake. Ni hadhi ya kijamii



32 Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com 32
Ufanano
: zote zinahusu mtu kupata heshima fulani 3.

Sinonimia: pikipiki na bodaboda
Utofauti:
pikipiki ni kwa ajili ya matumizi ya jumla lakini bodaboda ni kwa ajili ya biashara (kubeba abiria)
Ufanano:
zote hutumia matairi mawili na mota ya kutumia mafuta. Zote ni pikipiki lakini si pikipiki zote ni boda boda 4.

Sinonimia: Uso na Sura
Utofauti:
Uso ni halisi ni kitu kinachoshikika (complete) lakini sura ni dhahania na haishikiki.
Ufanano:
zote hurejelea sehemu ya mbele ya kichwa cha mnyama (hasa binadamu) 5.

Eleza tofauti kati ya sinonimia zifuatazo Shimo, tobo na tundu Ufafanano wake ni uwazi tu. Kwamba vyote hivi vinazungumzia uwazi. Lakini kuna totauti zake.


Fahiwa ya mwelekeo.
Shimo lazima uelekee chini ambapo tobo na tundu si lazima uwazi wake uelekee chini lakini kwa shimo ni lazima


Fahiwa ya ukomo
; uwazi katika shimo lazima uwe na ukomo ilhali tobo halina ukomo. Linapitiliza mpaka upande wa pili. Na tundu linaweza kuwa na ukomo au lisiwe na ukomo. Kwa mfano matundu kama ya chandaria. Lakini kwa tundu kwa mfano matundu ya choo yana ukomo.


Uasilia-
katika uasilia tunajiuliza je huo uwazi ni wa asili kama sehemu ya umbile ya hicho kitu au ni matokeo ya uharibifu? Kwa hiyo ukijiuliza swali hili ni kuwa: shimo si maumbile asilia ya hicho kitu, linaweza kuwa limechimbwa na wadudu fulani au wanadamu. Pia uwazi katika tobo si wa asili bali ni matokeo ya uharibifu lakini uwazi katika tundu ni wa asilia


Fahiwa ya ukubwa.
Ingawa fahiwa hii haina mipaka dhahiri kati ya tundu na tobo lakini kuhusu shimo uwazi wake lazima uwe mkubwa. Hata hivyo ukubwa wake hauwezi kupimika isipokuwa kwa watumiaji wa lugha mahususi. Kwa upande wa tobo na tundu si rahisi kutofautisha hata hivyo tunaweza kufikiri kwamba tundu ni kubwa kuliko tobo (hakuna makubaliano katika hili)

Je uwazi katika miili yetu ni mashimo au matobo?
Maswali ya Semina
Swali la 1
Inadaiwa kwamba nyanja za isimu, zimepangwa kingazi ambapo katika ngazi ya chini kuna fonolojia, ikifuatiwa na mofolojia, Sintaksia katika ngazi ya mwisho juu. Kwa kutumia taaluma ya semantiki uliyo nayo, hakiki dai hili kwa mifano ukionesha dosari inayojitokeza na kisha pendekeza mbadala
Jibu la kiini Huwezi kutenganisha semantiki na nyanja nyingine za lugha kwani kila Nyanja inatarajiwa itoe maana ya kile ambacho inakielezea na kushughulika na maana ni kushughulika na semantiki.
8

Comments

  1. Ni muhimu kuonesha marejeleo katika kazi yako

    ReplyDelete
  2. Vipi kuhusu vimanilizi vya mazungumzo

    ReplyDelete
  3. Kuna uhusiano gani Kati ya uolez na kategoria ya hali

    ReplyDelete
  4. Vipi kuhusu maana ya udokezi katika mazungumzo

    ReplyDelete
  5. uhusika ni nini?

    ReplyDelete
  6. Mkuu msada juu ya dhana zifuatazo
    Uhusika
    Uchukulio
    Ujumlishaji
    Dhana awali

    ReplyDelete
  7. kazi yako ni mpya?

    ReplyDelete
  8. Fafanua mahusiano ya kiurejeo yanayodhihirika katika lugha ya kiswahili

    ReplyDelete

Post a Comment

Tafadhari usicomment matusi

Popular posts from this blog

RIWAYA YA KISWAHILI NA SIFA ZAKE

SEMANTIKI NA PRAGMATIKI