Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2026

WANGONI WANGONI WANGONI NA ASILI YA MAJINA YAO

HABARI NA HISTORIA YA KABILA LA WANGONI NA MGAWANYIKO WA MAJINA YAO. Kama ilivyokwisha kufafanua kwenye makala zilizopita juu ya kabila la Wangoni, kuwa ni moja ya kabila linalopaikana nchini Tanzania na sehemu zingine za kusini mwa bara la Afrika. Na kutokana na kabila hili kupita sehemu mbalimbali wakitokea kusini mwa Afrika mpaka Afrika ya kati na mashariki,kuna mengi ya kujua. Kimasingi kuna aina mbili za Wangoni, kuna Wangoni asilia na kuna Wangoni wa kujiita tu. Wangoni wa asili ni wale ambao chimbuko lako ni kusini mwa Afrika. Na Wangoni wa kujiita hawa ni wale wakazi waliokutwa kwenye maeneo yao na kuamua kujiita Wangoni kwa sababu mbalimbali ambazo wao walikuwa nazo(nitafafua hili kwa kina hapa chini). Kwa ujumla Yapo mengi sana ya kusimulia juu ya kabila hili la Wangoni. Ila kwa leo tutajadili mgawanyiko wa majina ya Wangoni. Ukweli ni kwamba, Wengi tumekuwa tukifahamu kuwa Wangoni wanapatikana mkoani Ruvuma hasa kwenye wilaya ya Songea. Na kutokana na kabila hili...