CHAKUHAWATA NI QNET ILIYOCHANGAMKA
CHAKUHAWATA NI QNET ILIYOCHANGAMKA.
Na Thadei Ole Mushi.
Juzi niliandika kuwa Chakuhawata ni mchongo wa wahuni wengine waliopo mjini, wakanipigia simu wakaniambia Koma kama kocha wa Simba Robentihno alivyokoma kumtoa Chama.
Ninachojua mimi kumkata mwalimu maokoto ya 5,000 kila mwezi ni kumlagai Mwalimu tu ili aingie kwenye 18 na watu waanze kuokota maokoto na kutokomea kusikojulikana. Kwa vyovyote vile kama wanataka kuja kuwa chama cha kweli cha kutetea maslahi na haki za waalimu hawataweza kukiendesha chama hicho kwa shilingi 5,000 kwa kila mwalimu kukakatwa kila mwezi.
Hesabu hazidanganyi.
Kwa mujibu wa Takwimu zilizopo jumla ya walimu wote nchini Msingi na Sekondari wapo 258,291. Fuata link kupata taarifa za takwimu za walimu:-
http://demo8.eganet.go.tz/tsc/statistics
MAPATO YA CHAKUHAWATA.
Chakuhawata wanakata 5,000 kwa kila mwalimu, tuseme sasa walimu wote wamejitoa wamejiunga nao hivyo ni 5,000 X 258,291 X 12 (Miezi) unapata jumla ya 15,497,460,000 (Bilioni 15.4) hapa ni kama walimu wote bila kubaki hata mmoja watajiunga CHAKUHAWATA. Wakipingua ni balaa zaidi.
Sasa twende kwenye kitu kinaitwa MATUMIZI.
Tutakwenda kwa hali ya chini kabisa na hapa tutachukua maeneo mengine Kodi na sio kufanya ujenzi na idadi ya watumishi tutalunguza na kuwalipa kidogo sana, Gari wala pikipiki hatutanunua kabisa watendaji wote wataprint kwa miguu kwenda kwenye Shughuli zao.
Jumla ya wilaya zipo 139 jengo lenye ofisi zote za chama kodi yake chini ya shilingi 500,000 ukizidisha mara Wilaya zote unapata Milioni 69,500,000 zidisha mara miezi 12 ya mwaka mzima utapata 834,000,000
Mishahara ya makatibu wa wilaya tuseme watalipwa 1,500,000 kwa mwezi zidisha mara wilaya zote 139 utapata jumla ya shilingi 208,500,000 zidisha mara miezi 12 jumla ya bilion 2,502,000,000
Chukua majengo ya kukodi kwa ajili ya mikoa. Mikoa ipo 26 tu zidisha kwa bei ile ile ya wilaya utapata 13,000,000 zidisha mara 12 unapata 156,000,000.
Chukua Mishahara ya watumishi wengine wa usafi kila wilaya tuseme analipwa tu laki tatu hapa hatujaajiri kampuni ukizidisha kwa halmashauri 139 unapata 41,700,000 zidisha mara 12 unapata 500,400,000
Chukua walinzi wa wilayani kote na hapa tumlipe kama mtu wa Usafi laki tatu jumla ni 41,700,000 zidisha mara 12 unapata 500,400,000
Chukua PS wa katibu naye tumlipe laki tatu kwa wilaya zote itakuwa 41,700,000 zidisha mara 12 unapata milioni 500,400,000
Chukua mishahara ya maderava wa wilaya zote 139 tulipe laki ile ile tatu itakuwa 41,700,000 zidisha mara 12 unapata 500,400,000 (Madereva hawa watasubiri kama chama kitakodisha gari au mfadhili wa kununulia gari kila wilaya atajitokeza au anaweza kutumika kama mtu wa kuchukua barua na kumtengea bosi chai😀)
Chukua mishahara ya makatibu wa Mikoa 26 tuseme tutawalipa 2,000,000 kwa mwezi utapata jumla 52,000,000 zidisha mara 12 unapata 624,000,000.
Chukua mishara ya watumishi wanne kila mkoa (Ps, Mtu wa usafi, mlinzi, Dereva) itakuwa ni mikoa 26 mara Watu wanne jumla ni watu 104 tuwalipe tu laki tatu itakuwa 31,200,000 zidisha mara 12 unapata 374,400,000
Tununue Tshirt za walimu kwa ajili ya Mei Mosi. T shirt kama waliyovaa 2023 ile ya Blue tuinunue kwa 15,000 bei ya chini kabisa bila kofia. Chukua idadi ya walimu wote pale juu 258,291 mara 15,000 utapata bilion 3,874,365,000
Twende Ruzuku ya uendeshaji Wilayani maana Makatibu hawatumii mishahara yao kuendesha Ofisi. Kila wilaya tuipe kadirio la chini 3,000,000,000 zidisha mara wilaya 139, zidisha mara miezi 12 unapata 5,004,000,000
Chukua Ruzuku mikoani kadirio la chini wape 5,000,000 zidisha mara mikoa 26 halafu zidisha mara 12 utapata 1,560,000,000
Chukua mishahara ya watumishi makao makuu tuseme wapo wapo 10 tu hawa kuanzia katibu mkuu hadi Kampuni la ulinzi tuwape 2,000,000 zidisha mara watu kumi halafu zidisha mara 12 utapata 240,000,000
Ruzuku makao makuu tufanye ni 10,000,000 kwa mwezi zidisha mara 12 utapata jumla 120,000,000
Jumla ya Matumizi ni shilingi 17,289,600,000 kwa maana hiyo ili chama kiweze kuendeshwa kwa makadirio hayo hapo juu itabidi tukakope karibia ya Bilioni 2 na kwenye account mwisho wa mwaka inakuwa haina hata Cent.
Nimesema hapo juu Hapa hakuna kununua Gari wala baiskeli watumishi wataprint kwa miguu na hapa chama hakijapata migogoro ya wateja wake ambao kesi kumi zinatosha kukiua kabisa.
Nini cha Kufanya?
Kutokana na hali ilivyo ngumu ya maisha na namna watu wanavyosaka vyeo huku na kule ili kupata ahueni ya maisha ya kufanya utapeli wa kisomi ambapo waanzilishi wanajua wanaenda kukwama wapi na watakuwa wamenufaika wapi mkija kuzinduka yatatokea yale ya DECI na upatu mwingine uliowahi kutokea.
Ushauri wangu kwa walimu wasomi ni bora kurekebisha waliyoanayo Cwt.
Juzi niliwaambia kuwa endepo Bank ya CWT itatumika Vizuri hakuna mtu atakayekopa bank nyingine nchi. Warekebishe tu vigezo kukopa riba asilimia 7 kwa wingi wa walimu nchini mtafanya mambo makubwa sana na huenda benki nyingine zikafa kabisa kutokana na kuwa zinategenea sana kundi kubwa la walimu wakope kwenye benk zao ili zijiendeshe.
Kama viongozi wetu wakitulia majengo yetu ya wilaya na Mikoa yakirekebishwa kidogo tu yanaweza kuwa branch za bank hii na kutapakaa nchi nzima.
Ni kweli kuwa mwanzoni nilishauri kujitoa ila nimekuja kugundua kuna watu wanataka kuokota maokoto kilaini kabisa otherwise waje kwa hoja wanishawishi ila siwezi kuwaachia watu bank na miradi kibao ambayo ilitafutwa kwa jasho langu.
Matatizo huwa hayakimbiwi bali huwa yanakabiliwa. Ukimuona mtu anayakimbia matatizo badala ya kuyatatua huyo uwezo wake ni mdogo. Kinachonisikitisha haya yanafanywa na watu ambao wapo kwenye Taaluma Mama (Ualimu) yaani anadanganywa kama mtoto ndio maana matukio ya wastaafu wetu kucheza kekundu hayaishi huko mtaani na kuibiwa mafao yote.Tunaweza kufanya mapinduzi kwa ndani ila sio kutoka kwa sasa.
Ole Mushi
0712702602
Comments
Post a Comment
Tafadhari usicomment matusi