RIWAYA YA KISWAHILI NA SIFA ZAKE
RIWAYA
YA KISWAHILI
NUKUU ZA
SOMO:
MAANA YA
RIWAYA NA AINA ZA RIWAYA:
Riwaya imefasiliwa na wataalamu mbalimbali miongoni
mwao nikama vile,
Encyclopedia Americana (EA), Jz. 20 (1982:510f)
wakinukuliwa naMulokozi (1996) wanasema, riwaya kuwa ni hadithi ya kubuni
inayotosha kuwa kitabu.
Udhaifu; Maelezo haya yanaibua utata kwani
hayafafanui kitabu kinapaswa kuwa na urefu kiasi gani. Matharani kwa mujibu wa
UNESCO katika Mulokozi (1996) kitabu ni chapisho lolote lenye kurasa 48 au
zaidi. Ama urefu wa kitabu hautegemei idadi ya kurasa tu pia unategemea ukubwa
wa kurasa (upana na kina) ukubwa wa maandishi na mpangilio wake.
Encyclopedia Britanica EB, Jz.8, (1985:810)
wakinukuliwa naMulokozi (1996) wanaeleza kuwa, riwaya ni masimulizi marefu
yakinathari yaliyochangamana kiasi, yenye kuzungumzia tajriba yamaisha ya
binadamu kwa ubunifu.
Udhaifu: Udhaifu wa hoja hii ni kwambawamejikita
katika kigezo cha urefu, lakini hatujui urefu huo wapaswa kuwa kiasi gani.
Wamitila (2002) Senkoro(2011) na hawakubaliani na
kigezo cha kufasili riwaya kwa kutumia
kigezo cha urefu. Mfano Senkoro anaeleza kuwa
,“Ikiwa tutakichukua kipimo cha jumla ya maneno(75,000)kuwa kielelezo cha
riwaya basi itaonekana kuwatunariwaya chache mno katika fasihi kwa hali
hiinadhani sifa ya mchangamano ni nzuri zaidikuelezeamaana ya riwaya” (uk.
56)Naye Wamitila anendelea kuelezea kuhusiana na suala urefu kuwa,“Kigezo hiki
cha urefu hakifaitunapoziangalia kaziza fasihi ya Kiswahili...Mfano kazi mbili
zaE. Kezilahabi,“Nagona naMizingile” hazina idadi kubwa yamaneno lakinini
riwaya”.
Wamitila (2002) na Senkoro (2011) wanasema riwaya
nikisa mchangamano ambacho huweza kuchambuliwa kupimwa kwamapana na marefu
kifani na kimaudhui.
>> Riwaya ni kisa aumkusanyiko wa visa, nyenye
urefu unaoviruhusu vitambe nakutambaa mahali pengi na kuambaa vizingiti vingi
vya maisha kamaapendavyo mwandishi wake.
>> Riwaya basi ni hadithi ndefu ya
kubuni,yenye visa vingi, wahusika zaidi ya mmoja, na yenye mazungumzona maelezo
yanayozingatia kwa undani na upana, maisha ya jamii.Riwaya hutoa picha ya jumla
ya maisha ya mtu toka nyumbani hadikatika kiwango cha taifa na dunia nzima.
Madumula (2009), Riwaya ni masimulizi marefu ya
kubuni yaliyo katika mtindo wa kubuni yakisawili mtindo maalumu na madhumuni
maalumu. Mhusika katika Riwaya anakuwa ni kipaza sauti cha mwandishi.
KWA UJUMLA;riwaya ni masimulizi ya kubuni ya
kinathari yenye msuko au mpangilio fulani wa matukio au ploti inayofungamana na
wakati au kusawili wakati na yenye visa vingi vivavyotendeka katika wakati
fulani na yenye mawanda mapana yenye mchangamano wa dhamira, visa na wahusika.
MAANA YA RIWAYA KISWAHILI:
Riwaya ya Kiswahili ni ile ambayo inafungamana na
utamaduni wa jamii ya waswahili katika lugha ya kiswahili ambao hupatikanakatika
nchi ya Afrika mashariki. Pia ni ile riwaya ambayo inawahusu waswahili wenyewe.
VIPENGERE VYA MSINGI KATIKA RIWAYA;
Inaonyesha kuwa ili kujua maana ya riwaya ni
vyemakuzingatia mambo kadhaa ambayo ndiyo ya msingi, na mambohayo ni;
1) Lazima
riwaya iwe na lugha ya kinathari,
2) Isawiri
maisha ya jamii,
3) Iwe na masimulizi ya kubuni na visa virefu,
4) Wahusika zaidi ya mmoja,
5) Iwe na mpangilio na msuko wa matukio,
6) Lazima na
maneno kuanzia elfu thelathini na tano na kuendelea, na
7) Riwaya ni lazima ifungamane na wakati yaani visa
na matukio ni lazima viendane na matukio.
HISTORIA FUPI YA RIWAYA:
Riwaya ilizuka kutokana na maendeleo ya mageuzi ya
kiutamaduni. Suala la ukoloni na uvumbuzi pia liliumba hali ambazo zilihitaji
kuelezwa kwa mawanda zaidi ya yale ya ngano na hadithi fupi. Hapo hapo kuzuka
kwa miji na viwanda pamoja na maendeleo ya wasomaji yalifanya riwaya nyingi
ziandikwe.
Uchangamano wa maisha ya jamii kisiasa, kiuchumi na
kiutamaduni wenyewe ulizusha haja ya kuwa na utanzu wa fasihi ulio na
uchangamano kifani na kimaudhui.
Kupanuka kwa usomaji, hasa wakati wa mapinduzi ya
viwanda huko Ulaya, kuliwafanya waandishi waandike waandiko marefu kwani sasa
walikuwapo wasomaji hasa wanawake waliobaki majumbani wakati waume zao
walipokwenda viwandani, wasomaji ambao muda wao uliwaruhusu kusoma maandiko
marefu marefu ijapokuwa hii lilikuwa jambo la baadaye sana wakati wa kina
Charles Dickens. Hii historia fupi ya chimbuko. Senkoro (2011:55).
HISTORIYA KATIKA RIWAYA YA KISWAHILI;
Tanzu za asili zinaonyesha kuwa ndio zilichangia kwa
kiasi kikubwa sana katika kuibua riwaya za Kiswahili.Na yafuatayo ni mawazo ya
wataalamu mbalimbali juu ya chimbuko la riwaya ya Kiswahili.
Madumulla (2009), ameeleza kuwa riwaya ilitokana na
nathari bunifu simulizi kama vile hadithi, hekaya, na ngano inayosimuliwa kwa
mdomo. Anaendelea kusema kuwa fasihi ilitokana na maandiko ya fani ya ushairi
hususan ni tendi za Kiswahili katika hati za kiarabu kwa sababu ndiyo maandishi
yaliyotamba katika pwani ya afrika mashariki. Wazungu na waarabu
hawakubadilishana maarifa kwa urahisi na hivyo pakapelekea kuwa na majilio ya
taratibu za maandiko ya kinathari. Mwanzoni riwaya zilitafsiriwa kwa Kiswahili
toka katika lugha za ulaya na kufanya riwaya za Kiswahili kutokea. Mfano wa
riwaya hizo ni kama vile; Habari za mlima iliyoandikwa na Sheikh Ali Bin Hemed
(1980).
Senkoro (2011) anaeleza kuwa riwaya zilizuka
kutokana na maendeleo na mageuzi ya kiutamaduni, uchangamano wa maisha ya
kijamii, kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni yaliyopelekea haja ya kimaudhui
zaidi ya ngano na hadithi fupi. Anaendelea kusema kuwa riwaya za kwanza
zilitafsiriwa toka riwaya za kizungu mpaka za Kiswahili, Anasema riwaya
mojawapo ni ile ya James Mbotela ya Uhuru wa Watumwa. Ndiyo riwaya ya kwanza
kutafsiriwa kwa Kiswahili. Pia anaeleza kuwa riwaya ni utanzu uliozuka kutokana
na hali mahususi za kijamii. Riwaya kama ile ya kiingereza ya Robinson
Crusoe iliyoandikwa naDaniel Defoe ni miongoni mwa
riwaya za mwanzo.
Mulokozi (1996) anaeleza kuwa chimbuko la riwaya ya
Kiswahililipo katika mambo makuu mawili ambayo; nifani za kijadi za
fasihipamoja na mazingira ya kijamii.Fani za kijadi za fasihi, Mulokozi
anaeleza kuwa riwaya haikuzukahivihivi tu bali ilitokana na fani za masimulizi
yaani hadithi, na ndipozikapatwa kuigwa na watunzi wa riwaya wa mwanzo. Fani
hizozilizopata kuchipuza riwaya za mwanzo ni kama vile; riwaya zakingano,
tendi, hekaya, visakale, historia, sira, masimulizi ya wasafiri,insha na
tafsiri.
Ngano, Mulokozi anasema, kuwa ni hadithi fupi simulizi
pia huwa nihadithi za kubuni na nyingi hasa zinawahusu wanyama wakali,
piazinahusu malaika, binadamu, mazimwi na majini. Anasema kuwamara nyingi ngano
huwa na msuko sahihi na wahusika wake ni bapana wahusika hao ni mchanganyiko wa
wanyama, mazimwi nabinadamu. Anatolea mfano wa ngano zilizo chukua visa vya
kinganokuwa ni kama vile riwaya ya Adili na Nduguze ya Shaaban Robart(1952),
Lila na Fila ya Kiimbila (1966), Kusadikika ya Shaaban Robart(1951).
Hekaya,ni hadithi za kusisimua kuhusu masaibu na matukio
ya ajabuyaani yasiyokuwa ya kawaida. Mara nyingi masaibu hayohufungamanishwa na
mapenzi. Hekaya hizo zimepelekea riwaya
zaKiswahili kama vile; Hekaya ya Adili na Nduguze ya Sharban Robart(1952),
hekaya ya Ubeberu Utashindwa ya Kiimbila (1971), na Hekayaya A.J.Amiri, ya
Nahodha Fikirini, (1972).
Tendi (utendi), ni hadithi ya kishairi kuhusu
mashujaa wa kihistoria na wa kubuni, ambao waweza kuwa ni wa kijamii au
kitaifa. Kwa kawaida baadhi ya tendi zina sifa za kiriwaya ila tu badala ya
kuwa na umbo la kinathari zenyewe zina umbo la kishairi. Kuna tendi za aina
mbili ambazo ni tendi andishi na tendi simulizi. Riwaya pevu kama tendi
husawiri mawanda mapana ya kijamii na kihistoria. Huwa na wahusika wababe yaani
mashujaa wenye kuwakilisha pande zinazopingana. Mfano wa tendi ni kama vile;
Utendi wa Vita vyaWadachi Kutamalaki Mlima ya Hemedi Abdallah, (1895), Utendi
war as (Ghuli), utenzi wa Fumo liyongo wa Mohamed Kijumwa K.(1913).Tendi katika
riwaya za Kiswahili imetumia wahusika wawili tuambao ni wahusika wa kubuni na
wale wa kijadi wa kiafrika.
Visasili, hizi ni hadithi zinazohusu asili na hatima
ya watu, vitu,viumbe, ulimwengu na mataifa, na pia huangalia uhusiano
wawanadamu na mizimwi pamoja na miungu. Hadithi za kivisasilizinapoonyeswa
huaminika kuwa yakweli tupu hasa kwa kusimuliamatukio mengi ya
kiulumwengu.Mfano wa visasili; Lila na Fila ya Kiimbila (1966) ambayo
imekopamotifu ya asili ya ziwa ikimba huko Bukoba. Hadithi ya Mungu waKikuyu
huko Kenya. Roza Mistika ya Kezilahabi (1971), Nagona(1987) naMzingile (1991),
Siku ya Watenzi Wote ya Sharban Robart.
Visakale, ni hadithi ya kale kuhusu mashujaa wa
taifa,kabila au dini. Mara nyingi visa kale huchanganya historia na masimulizi
ya kubuni, na hadithi hizi hupatikana karibu katika kila kabila kila lugha.Baadhi
ya visakale vya Kiswahili masimulizi huhusu chimbuko la miji ya pwani,
mijikenda, mwinyi mkuu huko Zanzibar.Visa kama hivi ndivyo vinavyopelekea
kuandikwa kwa riwaya za kiswahili. Mfano wake ni riwaya ya Abdalla Bin Hemed
bin Ali Ajjemy (1972) katika kitabu cha Habari za Wakilindi, Kisima cha na
Giningi ya M.S.Abdulla (1968) na ile Hadithi ya Myombekela na Bibi Bugonoka na
Ntulanalwo naBuhliwali (1980) ya A. Kitereza.
Masimulizi ya kihistoria, haya ni masimulizi ya
matendo ya, mwanadamu katika muktadha wa wakati, na ni fani muhimu sana katika
jamii yeyote ile. Masimulizi halisi ya kihistoria yaweza kuwa ni ya mdomo au
hata maandishi na yote huwa ni chemichemi nzuri ya riwaya. Mfano wa riwya hizo
ni; Habari za pate za Fumo Omari Nabhany (1913) ambayo yalikuwa ni maandishi ya
masimulizi na uchambuzi. Riwaya zingine zilizoathiriwa na matukio ya kihistoria
ni;Uhuru wa Watumwa ya J. Mbotela (1934), Kifo cha Ugenini ya O. Msewa (1977),
Kwa Heri Iselamagazi ya B. Mapalala (1992) na Miradi Bubu ya Wazalendo ya G.
Ruhumbika (1992).
Sira, ni masimulizi ya kweli kuhusu maisha ya mtu au
watu. Sira iliathirikuchipuka kwa riwaya hasa kwa kuonyesha masilimulizi ya
maishaya mtu toka utotoni mpaka uzeeni. Masimuliza ya riwaya hiziyalikuwa
katika masimulizi na hata katika maandishi pia kwa maanakabla ya ukoloni
yalikuwepo maandishi yaliyohusu maisha ya mitumena masahaba.Mifano ya hadithi
hizi ni; Kurwa na Doto ya M. S.Farsy(1960),Rosa Mistika ya Kezilahabi
(1971),Kichwa Maji ya Kezilahabi(1974) pamoja na Dunia Uwanja wa Fujo
(1975),Mzimu wa Baba waKale ya Nkwera (1967),na riwaya ya Maisha Yangu baada ya
MiakaHamsini ya Sharban Robart (1951).
SIFA ZA RIWAYA;
Kwa mujibu wa Wamitila (2002) sifa hizo ni kama
zifuatazo;
i)
Uwazi na uangavu,
ii) kazi husika ya fasihi isiwasumbue
nakuwatatiza wasomaji kuzielewa,
iii)
muwala na muumano,
iv)
kazi yariwaya lazima iwe na mshikamano au mtiririko mzuri wa visa
aumatukio kuijenga kazi ya kifasihi,
v) uchangamano wa visa yaanikutokea kisa
zaidi kimoja,
vi)
Wingiwa maana kuhusiana na sifa yauchangamano na ukamilifu ni kule
kuwako kwa elemeti zotemuhumiu na za kimsingi katika kazi ya fasihi.
SIFA NYINGINE NI:
vii)
Riwaya haifungwi na sheria wala kanuni.
viii)
Riwaya ina matumizi ya lugha ya kinathali. Ni lugha ya mjazo wa
maneno na mtiririko wa mawazo.
ix)
Riwaya ina urefu na upana wa kutosha,,,,,, urefu na upana wa kimaudhui unapelekea kubeba
vijitanzu vingine vidogovidogo ndani ya Riwaya.
x)
Riwaya zao la kibepari: Riwaya ilizuka katika mfumo wa kibepari huko
Ulaya , Riwaya ina sifa ya ubinafsi, ina uhitaji mkubwa wa viwanda nah ii
ilianza ktk kipindi cha mapinduzi ya viwanda hivyo inahitji uchumi madhubuti
kama vile uandishi na uchapaji.
xi)
Riwaya iko karibu na uhalisia, inahusisha masimulizi ambayo
yalikuwepo,,,,, yapo,,,,,au yanatazamiwa yatokee na whusika hujengwa katika
mazingira hayo.
xii)
Riwa inahitaji ujuzi wa kusoma na kuandika.
xiii)
Riwaya inahitaji maisha tulivu,,,,, maisha anbayo yatamfanya mtunzi awe
katika hali ya kutunga Riwaya.
AINA ZA RIWAYA:
RIWAYA ZINAGAWANYIKA KATIKA MAKUNDI MAKUU
MAWILIAMBAYO NI
(A) RIWAYA DHATI; Hizi ni Riwaya ambazo zina mambo
dhati, wasaha na manbo ambayo ni adili kwa binadamu. Hutumia lugha fasaha,
nyofu na hakuna matusi. Mfano ‘Kosa la
Bwana Mussa’, ‘Mzimu wa Watu wa Kale’, ‘Utengano’ na ‘Almasi za Bandia’.
(B) RIWAYA
PENDWA;Hizi huzungumzia maswala ya upelelezi, mapenzi na mambo mengine ambayo
ni pendwa. Riwaya pendwa huchomaza zaidi vipengere vya fani kuliko maudhui.
Mara nyingi hutumia methali, misemo na mbinu nyingine ambazo humfanya msomaji
asitafakari zaidi maudhui. Mfano: Pendo la Kifo, Njama, Kikosi cha Kisasi,
Nyuma ya Pazia na Mfadhili.
AINA ZA RIWAYA KWA KUZINGATIA VIGEZO
I)
KIGEZO CHA FANI:
Riwaya sahili; ni dhana inayotumiwa kuelezea aina za
riwaya ambayo ina muundo rahisi na inaweza kueleweka kwa urahisi. Kwa mfano;
riwaya ya “Kaburi Bila Msalaba” ya P . Kureithi.
Riwaya changamano; Ni riwaya ambayo ina muundo mgumu
na inayohitaji umakini kuielewa. Kwa kawaida msuko wa riwaya hii huwatata.
Inawezekana pakawepo na matumizi mapana ya mbinu rejeshi,upana mkubwa wa
wahusika na mandhari, matumizi mengi ya lughaya kitamathali, mfano; “Mzingile”
ya E. kezilahabi, “Zirail na Zirani” yaW.E Mkufya.
Riwaya ya majaribio, Ni riwaya inayojadili mkondo wa
nafasi na riwaya kweli. Riwaya ya mjadara nafsi hutungwa bila kuzingatia kanuni
za kawaida za uandishi wa riwaya, watunzi wa riwaya hii hudai kuwa kumbo la
kawaida ya riwaya hii haitoshelezi mahitaji ya karne hii huwakilisha ukweli wa
maisha.Riwaya hizi hutumia nafsi ya pili na wakati mwingine hutumia nafsi mimi
kiasi kwa mwandishi ndiye mhusika. nafsi ya pili humfanya msomaji kuonekana
kuwa ndiye katenda jambo. Mfano, “Mtunzi wa Hukumu” ya Kasri na “Bina-Adamu” na
Musaleo” za Wamitila vilevile Nagona na Mzingire zake E, Kezilahabi.
II)
USIMULIZI:
Riwaya barua ni riwaya ambayo huwa na muundo wa
barua kuanzia mwanzo hadi mwisho, au ni majibizano ya barua. mfano “Pamela” ya
S.Richardson na “ Barua Ndefu kama Hii.
Riwaya ya kimonolojia ni riwaya ambayo sauti
inayotawala ni moja. Sauti hiyo ni ya mwandishi. Wahusika wanaopatikana katika
riwaya hii hudhibitiwa kwa kiasi kikubwa na sauti ya mwandishi. Mfano
“Walenesi” na “Mafula” za Katama Mkangi.
III)
UPEO WA KIJIOGRAFIA:
Riwaya ya kiambo; ni riwaya ambayo inatilia mkazo
kwenye mandhari, usemi au muundo wa kijamii na desturi za mahali maalumu.
Mandhari na mahali huathiri njia mbalimbali za kuhisi na kuwaza kwa wahusika
wanaopatikana kazi ya aina hii. Huelezea mambo ya tamaduni mfano, ‘Bwana
Myombokera na Bi Bugonoka’, watu wa Ukerewe na ‘Kisiwa Cha Giningi’.
Riwaya ya kidastopia hii husawili jamii isiyokuwa ya
kawaida na isiyokuako kwa wakati maalumu bali inafikirika tu. Katika jamii hiyo
sheria za kawaida za kijamii zimebadilishwa kwa namna inayowafanya watu wengi
waishie kutaabika na kuteseka sana. Mfano wa riwaya hizi ni kama vile “
Kusadikika” ya Shabani Robert na “Walenisi” ya Katama Mkangi.
Riwaya Kitaifa; hizi hujikita katika upeo wa
kijiografia ambapo haivuki mipaka ya nchi. Maudhui na mawanda huwa ni yamambo
yanayojiri katika taifa husika,
Riwaya za Kimataifa; Hi ni Riwaya ambazo ni kinyume
cha zile za kitaifa kwa hujadili mambo ya nchi zaidi ya moja, mfano wan chi
zinazoendelea na zilizoendelea.
IV)
MAUDHUI:
Riwaya historia ni aina ya riwaya ambayo msingi wake
kuhusu matukio fulani katika jamii ya mwandishi, tukio hili huwa ni kubwa na la
muhimu kijamii, laweza kuwa la kikabila au la kitaifa mfano “Uhuru wa Watumwa”
ya J. Mbotela, “Miradi Bubu ya Wazalendo” ya Luhumbika na “Zawadi ya Ushindi”
ya B. Mtombwa.
Riwaya ya kimaadili ni riwaya ambayo ina nia ya
kufundisha maadili fulani mfano “Kufikirika” ya S Robert. Ni riwaya inayotoa
maadili kwa jamii. Riwaya hizi huelezea mambo ya dini, mafunzo na maonyo ya
maisha. Hujengwa katika nguzo tatu ambazo
a)
Mathema (kosa): Kosa analolifanya mhusika mkuu linafanya jamii ipate
shida. Kosa hilo humfanya mhusika ajifunze na jamii ijifunze.
b)
Pathema (Funzo):Mafunzo anayoyapata mhusika juu ya kosa alilolifanya,
c)
Cathersis (utakaso): Utakaso unapatikana baada ya funzo na kubadilika.
Riwaya ya kimapinduzi ni riwaya ambayo inajadili
migogoro namaisha ya binadamu kwa kutafakari kwa mantiki na kina kuhusumambo
ambayo urazini wake hauonekani kwa urahisi.Hudodosa mapambano, mikinzano na
matabaka katika jamii Mfano“Umleavyo” ya Haji na Kichwa Maji” ya E.Kezilahabi,
vilevile na Dunia mti mkavu na Kusadikika.
Riwaya ya kisosholojia au jamiini riwaya ambayo
inasawiri maisha ya kawaida ya jamii kwa kuchunguza matatizo yake, yawe
kifamilia kitabaka, kiuchumi, kisiasa au hata kiutamaduni mfano “Titi la Mkwe”
ya A. Banzi, “Kurwa na Doto” ya M.S. Farsi na “Rosa Mistika” ya E. Kezilahabi.
Riwaya saikolojiani aina ya riwaya inayododosa nafsi
ya mhusika, fikra, hisia mawazo, imani, hofu, mashaka, matumaini na athari ya
mambo hayo kwake binafsi na labda kwa jamii mfano “Kichwa Maji” ya
E.Kezilahabi, “Kipimo cha Mianzi” ya Feud na “Kiu” ya M.S. Mohammed.
Riwaya ya kifalsafa, ni riwaya ambayo inashughulikia
masuala ya kifalsafa. Mada ya kifalsafa huchukua sehemu muhimu katika riwaya ya
aina hii kuliko wahusika, mandhari, msuko au mtukio.Mtunzi hutaka wasomaji
wafikirie kifalsafa mambo Kama vile kuwepo au kutokuwepo kwa MUNGU, Baadhi ya
viumbe, kufa na kuishi ni nini? Utu na mtu nini? Mfano, “Nagona na Mzingile” ya
E kezilahabi na “Umleavyo” ya Haji Gorra Haji.
Riwaya ya mapenzi ni riwaya yenye kusawiri uhusiano
wa kimapenzi kati mvulana na msichana. Huchomoza zaidi fani kuliko maudhui,
Mfano “Kweli Unanipenda” “Mwisho wa Mapenzi” za Simbamwene.
Riwaya ya kitawasifu, ni riwaya ambayo ina muundo
unafanana na muundo wa tawasifu kwa kuyachunguza maisha ya mtu fulani na kwa
nafsi ya kwanza. Mfano riwaya ya “Uhuru wa watumwa” J. Mbotela na “Maisha Yangu
baada ya Miaka Hamsini” ya S.Robert.
Riwaya ya wasifu, ni riwaya ambayo mwandishi
huandika kwa lengo la kumhusu mtu fulani, mfano “Wasifu wa Siti Binti Saad” ya
S. Robert.
KUNA MAKUNDI MENGINE YA RIWA AMBAYO HAYAKUAINISHWA
HAPO JUU NAYO NI:
Riwaya ya ujasusi ni wa upelelezi wa kimataifa.
Majasusi ni wapelelezi wanaotumwa na; nchi, serikali au waajiri wao kwenda
katika nchi nyingine kuchunguza siri zao hasa siri za kijeshi, kiuchumi na
kisayansi ili taarifa hizo ziwanufaishe wale waliotumwa mfano “The thirty nine
steps” ya E. Msiba. “Mzimu wa Watu wa Kale”.
Riwaya ya kisayansi ni riwaya inayotumia taaluma ya
sayansikama msingi wa matukio, masahibu na maudhui, mathalani riwaya
hiihubashiri namna sayansi itakavyo athiri maendeeo ya mwanadamukatika karne
zijazo. Mfano “Safari Kiini cha Dunia” ya Jules Vernes.
Riwaya tendi ni riwaya yenye mawanda mapana kama
tendiaghalabu riwaya hii husawili matendo ya ushujaa na masuala mazitoya
kijamii yenye kuathiri historia ya taifa husika. Mfano “Vita naAmani” ya Leo
Tolstoi na “Chaka Mtemi wa Wazuru” ya Thomas M.
Riwaya istiara ni riwaya mafumbo ambayo umbo lake la
nje niishara au kiwakilishi tu cha jambo jingine. Mfano “Kusadikika” yaS.Robert
ambayo inasawili utwala wa mabavu na “Shamba laWanyama” ya Kawegere
Riwaya chuku ni riwaya ambayo hueleza vituko na
masahibuyasiyo kuwa ya kawaida, ni riwaya ambayo haizingatii uhalisia namara
nyingi masahibu yake huambatanana mapenzi.Mfano “Alfu lela
Ulela” ya G. Bocci ccio na “Kusadikika” ya S.Robert”
Riwaya ya kingano, ni riwaya yenye umbo na mtindo wa
nganomathalani huweza kuwa na wahusika wanyama,visa vyenyekutendeka nje ya
wakati wa kihistoriA.Mfano “Lila na Fila” yaLongman na “Adili na Nduguze” ya
S.Robert
Riwaya kinzani ni riwaya inayotumiwa kuelezea ambayo
imekwendakinyume na matarajio au kaida za uandishi wa riwaya. Mfano, kuwana
muundo wa kimajaribio wahusika kukosa motisha, kuwako kwamatendo yasiyoweza
kuungwa kimantiki.
Riwaya ya utetezi hii hutumiwa kuielezea riwaya
ambayo inahusumatatizo ya kijami, kiuchumi pamoja na dhuluma
inayowapatawanyonge au wasiokuwa na uwezo katika jamii fulani. Hivyo riwayahii
hukusudia kurekebisha hali iliyopo katika jamii. Mfano “Walenisi”na “Mafuta” ya
Katama Mkangi na “Kuli’ na “Vuta n’kuvute” za ShafiA.Shafi.
Riwaya ya kipolifoni; ni riwaya ambayo inahusishwa
na urejeleaji ambapo kila wahusika wanapozungumza au kuongea sauti zaombalimbali
zinawakilisha mikabala mbalimbali kiitikadi. Mfano “Duniamti mkavu” ya S.A
Mohamed.
Riwaya ya kisasa; ni riwaya inayohusu wanasiasa na
maisha yaowanasiasa. Hudhamiria kuyafichua mambo yanayotendeka kinyumena picha
inayoonekakana waziwazi. Mfano; “Nyota ya Huzuni” yaGeorge Liwenga na “Njozi
Iliyopotea” ya C.G. Mng’ong’o.
Riwaya ya kitarihi ni riwaya ambayo inajihusisha na
mawanda makubwa ya kiwakati na kimandhari.Wahusika wengi walioteuliwakuakisi
hali mbalimbali za kijamii na kiuchumi za wakati maalumu.Mfano;Riwaya ya
“Habari za Wakilindi”
Riwaya ya kiutopia hii ni riwaya ambayo inasawiri
jamii anayoionamwandishi kama jamii kielelezo na aghalabu huhusisha sifa
zaKifantasia au kinjozi. Mfano wa riwaya hii ni kama, “Siku ya WatenziWote” ya
Shaaban Robert.
Riwaya ya kiurejelevu hii ni riwaya inayojirejelea.
Aghalabu katikausimulizi wake, riwaya ya aina hii huishia kutoa maoni
kuhusuusimulizi wake na njia za kubuni na kutunga riwaya.Tunawezakusema hii ni
riwaya inayofichua mbinu zake za kiutunzi. Mfano“Musaleo” ya K.W.Wamitila.
Riwaya tatizo; ni riwaya ambayo inajishughulisha na
tatizo aumgogoro fulani katika jamii. Huweza pia kuelezea aina ya riwayaambayo
inachunguza tasnifu au swala fulani la kisaikolojia. Mfano;“Kuli” ya Shafi
A.shafi na “Mafuta” ya K. Mkangi.
Riwaya kampasi; ni riwaya ambayo mandhari yake ni
chuo kikuu. Hata hivyo hii imepanuliwa nakuhusishwa na kazi za kuchekesha
auzenye mwelemeo wa kitashititi. Kazi za aina hii hukusudia kufichuaudhaifu
uliopo katika tabia za wanachuo.Mfano; “Small world” yaDavid Lorge.
NADHARIA ZA UCHAMBUZI WA FASIHI
Wataalamu mbalimbali wameainisha nadharia mbalimbali
za uchambuzi wa kazi yoyote ya fasihi. Miongoni mwa nadharia hizo ni pamoja na;
(i)
Nadharia ya umuundo (structuralism)
Umuundo ni nadharia inayojibainisha kwa kuangalia
Ujumla wa uhusiano wa sehemu moja kwa nyingine katika kufanya kitu kizima. Kwa
mfano muungano wa maneno hufanya sentensi na sentensi zikiungana zinaunda aya
au onesho na onesho kuunda tamthiliya. Ntarangwi (2004) anasema kuwa umuundo
waweza kuelezwa kama mtizamo wa kitathimini ambao huzingatia zaidi miundo
inayojenga kazi binafsi.
Mwasisi
anayetajwa sana katika nadharia hii ni Ferdinard De saussure aliyependekeza
mtizamo mpya kuhusu lugha. Kinyume na wataalamu wengine walioshughulikia
historia na sura maalum za lugha fulani, Saussure alivutiwa na miundo
inayohimili lugha zote, huku akijaribu kuonyesha kwamba lugha zote za ulimwengu
zaweza kutathiminiwa kwa kaida maalum za umuundo. Alizua istilahi `parole' na `langue'
kueleza maoni yake: `Parole' au uzungumzi ni lughakatika matumizi na hiki
ndicho walichokizingatia wanaisimu wa awali,
Mkondo huu wa mawazo ya umuundo kuhusu sayansi za
jamii ulianzia ulaya na kuathiri mtazamo wa elimu mbalimbali (duniani) kama vile:
Falsafa, Anthropolojia, Historia, Uhakiki wa kifasihi naSasiolojia. Kwa hivyo
twaweza kuangalia jamii katika muundo wake wa kijuu juu na kuielewa lakini
tukitaka kupata maana mwafaka lazima tuchunguze muundo wake wa ndani ambao
hupatikana katika kila jamii ya wanadamu. Kwa hiyo hata katika kuielewa fasihi
lazima tuifahamu lugha yake.
UMUUNDO NA FASIHI
Kama vile muundo wa lugha ulivyo mfumo, muundo wa
fasihi pia una vipengele vinavyotegemeana na vinavyoelezwa katika muktadha wa
vipengele vingine. Katika kazi ya fasihi kuna kitengo cha kisanaa kama vile
maudhui, ploti, wahusika, muktadha na lugha. Hakuna kipengele cha fasihi kati
ya hivi kitakachoelezwa katika upekee wake. Lazima kielezwe kwa kuzingatia
kuwepo kwa jukumu la vipengele vingine. Kwa mfano katika kueleza au kuzungumzia
ploti, wahusika watashirikishwa na lugha yao kuzingatiwa. Kwa hiyo nadharia ya
umuundo husisitiza vipengele vya kazi ya sanaa, jinsi vinavyohusiana hadi
kuikamilisha kazi hiyo. Huangalia namna sehemu mbalimbali za kazi za sanaa
zilivyofungamana. Yaani Neno halihitaji urejelezi ili lipate maana, na Kazi
yenyewe ilivyoundwa ndivyo hutoa maana. Yaani maana inavyoumbwa ina dhima kubwa
kuliko maana yenyewe.
(ii)
Nadharia ya umarx (marxism)
Kwa maana rahisi kabisa, tunapoongelea kuhusu
nadharia ya UMarxtuna maana ya kurejelea mikabala mbalimbali ambayo misingiyake
mikuu ni mawazo yanayohusishwa na Carl Marx na FriedrichEngels. Katika kitabu
cha The Germany Ideology, Marx na Engelswalisema kuwa kitu cha msingi katika
maisha ya binadamu ni kula nakunywa, kupata malazi na mavazi na mambo mengine.
Tendo lakwanza la kihistoria kwa hiyo ni kutafuta njia ya kuyakidhi
mahitajihaya ya msingi. Ili kufanikiwa katika lengo hilo, binadamu
hulazimikakujiunga pamoja au kuunda umoja ili kuimarisha umoja na wepesi
wakuizalisha mali ya kukidhi mahitaji hayo. Muungano huo huwa naugawaji wa
majukumu au kazi ambayo ndiyo msingi wa kuundwakwa matabaka katika jamii.
Umarx katika Fasihi
>Usanii ni uumbaji wa Ukweli katika maisha.
> Ukweli unaooneshwa katika kazi za fasihi hiyo
ni usahihi wa mambo katika jamii? Kama niRiwaya, Tamthilia, Ushairi na
kadhalika inawakilishaje ukweli?
> Kazi za kisanaa zinatakiwa kuonesha mivutano
iliyopo katika jamii hasa kati ya wanyonyaji na manyonywaji.
(iii) Nadharia ya urasimi
Kwa mujibu wa Njogu na Wafula (2007) Urasimi ni
wakati maalumuambapo misingi ya kazi za sanaa huwekwa na kukubalika kuwavipimo
bora kwa kazi nyingine. Hii ina maana kwamba kila jamii inaurasimi wake.
Urasimi katika Kiswahili ulikuwepo kati ya karne ya 18na karne ya 18. Nao
urasimi wa Kigiriki ulikuwepo baina ya karne yanne (KK) na takriban karne ya
nne (BK).
Sifa za urasimi kwa ujumla
Pamoja na kwamba imeshatajwa hapo mwanzo kuwa kila
jamii ina urasimi wake, lakini bado tunaweza kutoa sifa za jumla za urasimi
mahali popote ulipo. Kwa mfano:
>Kazi ya kirasimi huwasilishwa katika lugha
inayoeleweka kwa urahisi. Hii ina maana kuwa wazo linaelezwa moja kwa moja.
Mitindo ya Kinjozi (mf.Nagona, Mzingile, Bina-Adamu, Walenisi)
haitumiwi.Uhalisia unasisitizwa.
·>Kazi nyingi za kirasimi hazichoshi kusoma. Hii
ni kwa sababu kazi hizi ni kazi bora. Husomwa mara nyingi na watu wengi na kila
unapoisoma wazo jipya hupatikana.
>Fani na maudhui katika kazi za kirasimi ni mambo
yaliyofinyangwa kwa kutumia mbinu kamilifu na teule. Daima kuna ufungamano
uliokamilika kati ya kinachoelezwa na jinsi kinachoelezwa.
(IV) JE ONTOLOJIA YA KIAFRIKA INAWEZA KUTUMIKA KAMA
NADHARIA YA KUCHAMBULIA KAZI ZA FASIHI ZA KIAFRIKA?.
( fuatiliya makala hii katika mtandao ili kupata
nukuu zaidi )
JE UNGEPENDA KUJUA MAANA AU FASILI YA FALSAFA
Wikipedia kamusi elezo huru wanasema,falsafa ni neno
linalotokana na neno la kigiriki lenye maana ya upendo na hekima,wanaendelea
kusema kuwa falsafa ni jaribio la kuelewa na kueleza ulimwengu kwa kutumia
akili inayafuata njia ya mantiki . Falsafa huchunguza mambo kama vile kuweko,au
kutokuweko,ukweli,ujuzi ,uzuri,mema, na mabaya,lugha na haki.
Kwa mujibu wa Wamitila (2003 ) anasema, falsafa ni
mawazo anayoyaamini mtu au mwandishi kuwa yana ukweli unaotawala misingi ya
maisha.
Hivyo, Falsafa ni taaluma au mtazamo unaochunguza
matumizi ya dhana,kupima hoja,mbinu za ujengaji hoja,kufanya uhakiki au
tathimini,kuthibitisha au kutoa ushahidi wa hoja zinazozungumzwananadharia
mbalimbali zinazohusu maisha.Mfano,kuua ni tendo zuri au sio zuri?
BASI IMANI NA MTAZAMO WAKO VIKUONGOZE KATIKA KUSOMA
NA KUTAFAKARI NUKUU HIZI:
NAKUTAKIA USOMAJI MWEMA WA KISWAHILI (RIWAYA
KISWAHILI);
Nukuu hizi ni baadhi zimekusanywa kutoka wataalamu
mbalimbali, Vitabu na mitandao ya kijamii; na
MWLIMU
ALLY ABDUL MKINDI
NA AISHA ALLY ABDUL MKINDI
MALEJEO.
Madumulla, S.J. (2009) Riwaya yaKiswahili: Nadharia
Historia na Misingi yaUchambuzi.Dar
es Salaam: MtureEducational Publishers Ltd.
Mulokozi, M.M. (1996) Utangulizi wa Fasihiya
Kiswahili. Dar es Salaam: TUKI.
Senkoro, F.E.M.K. (2011) Fasihi. Dar esSalaam:
KAUTTU.
Wamitila, K.W. (2002) Uhakiki wa Fasihi:Misingi na
Vipengele Vyake. Nairobi:Phoenix
Publishers Ltd.
Wamitila, K.W. (2003) Kamusi ya Fasihi:Istilahi na Nadharia.
Nairobi: FocusPublicatins Ltd.
Madumulla, J.S. (2009), Riwaya ya Kiswahili,
Historian a Misingi ya Uchambuzi. Nairobi:
Sitima Printer andstations L.td.
Mulokozi, M.M. (1996), Utangulizi wa Fasihi ya
Kiswahili. Dar es Salaam. TUKI.
Mhando, P. na Balisidya, (1976), Fasihi na Sanaa za
Maonyesho. Dar es Salaam: Tanzania
Publishing House.
Nkwera, F.V. (1978), Sarufi na Fasihi Sekondari na
Vyuo. Dar es Salaam: Tanzani Publishing
House.
TUKI,(2004),Kamusi ya Kiswahili
Sanifu.Nairobi.Kenya:Oxford University Press.
Senkoro,F.E.M.K.(2011), Fasihi Andishi.Dar es
Salaam.Kauttu L.t.d.
Wamitila,K.W.(2003),Kamusi ya Fasihi, Istilahi na
Nadharia. Nairobi:Focus Publication.
Mihanjo A,(2010)Falsafa na ufunuo wa
maarifa.Toriam.MorogoroTanzania.
Mohamed S.k (1988)Fungate ya uhuru.Dar-es-salaam
universityplace(DUP).
Muhando p (1982) Nguzo mama. Dar-es-salaam
universityplace(DUP).
Njogu na Chimera R(1999)Ufundishaji wa
fasihi,Nadharia naMbinu.Jomo Kenyatta.Nairobi
Tuki(2004)Kamusi ya Kiswahili sanifu.Taasisi ya
Uchunguzi waKiswahili.Dar-es-salaam.
Wamitila K.W (1996) Utangulizi wa Kiswahili.Chuo
kikuu cha Dares-salaam.Dar-es-salaam.
Nimependa sana posti zenu kuhusu somo la kiswahili ni nzuri kwa wanafunzi na walimu Wa somo la kiswahili
ReplyDeleteasante kwa hilo
DeleteNmependa Sanaa
ReplyDeleteVzr
ReplyDeleteNzuri kwa kweli asant
ReplyDeleteNaomba mwenye sifa bainifu za riwaya apost
ReplyDeleteNaomba mwenye sifa bainifu za riwaya ya kiswahili
ReplyDeleteInaeleweka vizuri Sana, hongera mchambuzi wetu
ReplyDeleteHongera
DeleteNaomba mfano wa riwaya ambayo haijahakikiwa
ReplyDeleteNaomba dhima za riwaya
ReplyDeleteNimeipenda sana ipo njema
ReplyDeleteNaomba mwenye fasili za riwaya pendwa Kwa mujibu wawatalamu mbalimbali
ReplyDeleteulinakili wapi? tumia machapisho ya hivipunde
ReplyDeletefanya tafiti soma kaka
Deletekazi kundu mwalimu
ReplyDeleteNaomba maana za riwaya kupitia wataalamu mbali mbali
DeleteHongera mchambuz
ReplyDeleteUnaweza kutupatia pia maoni Yako juu ya ukurasa wetu
Delete🤞🤞
ReplyDeleteSo nice but give more current isseu
ReplyDeleteAsante tumepokea ushauri wako
Delete