UCHAMBUZI WA SHERIA ZA KAZI NA MASLAHI YA MTUMISHI KATIKA UTUMISHI WA UMA

TWENDE SAWA NA MCHAMBUZI WETU TUKIREJELEA KANUNI ZA UTUMISHI WA UMA NA MAHUSIANO KAZINI -------------------- *kwenye utumishi wa umma kuna posho zifuatazo:-* 1.posho ya kujikimu(subsistence allowence) 2.posho usumbufu(distabance allowence) 3.Takrima(entertainment allowence) 4.posho ya kukaimu(acting allowence) 5.posho ya kazi maalumu) 6.posho ya mavazi(outfit allowence) 7.posho ya masaa ya ziada na kazi za ziada(overtime and extra duty allowence) 8.posho ya kilometa(kilometers allowence) 9.posho ya kikao(settings allowence) 10.posho ya mimba(housing allowance) 11.posho ya sare(unform allowence) 12.posho ya jeshi la polisi na magereza, huduma za zimamoto na uokoaji(police force and prisons,fireand rescue service allowence) 13.posho ya kukaimu; sehemu G( maintenance allowence)- section G N.k *Rejea kwenye kanuni za kudumu za Utumishi wa umma(standing order)L2* *NiPo* SHERIA ZINAZOSIMAMIA UTUMISHI WA UMMA, HAKI NA WAJIBU WA MTUMISHI WA UMMA 2.1 Utangulizi Katika mada hii utajifunza haki na wajibu wako katika utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka za Serikali za Mitaa. Mada hii itakuwezesha kutambua sheria zinazosimamia Utumishi wa Umma, haki na wajibu wako, na makosa na adhabu zinazotokana na ukiukwaji wa misingi ya mienendo na utendaji kazi katika Utumishi wa Umma. Malengo Mahsusi Baada ya kujifunza mada hii, utaweza:- Kuainisha sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma, Kuzingatia sheria za Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu ya kazi, Kuanisha haki na wajibu wa Mtumishi wa Umma, Kuainisha makosa na adhabu mbalimbali zilizoko kwenye Utumishi wa Umma. 2.2 Sheria za Utumishi wa Umma Tambua kwamba uendeshaji wa Utumishi wa Umma, unapaswa kuzingatia sheria mbalimbali zilizoko kwenye Utumishi wa Umma ili kuwa na utumishi unaotoa haki bila upendeleo kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Aidha zipo Sera, Sheria, na Kanuni zinazosimamia Utumishi wa Umma. 2.2.1 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sura ya 2 Kwa mujibu wa ibara ya 36 (1-2) ya Katiba, Rais ana mamlaka ya kuanzisha, kuteua na kufuta nafasi za madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Pia, ibara 36(3) ya Katiba imempatia mamlaka Rais kuanzisha Tume ya Utumishi wa Umma yenye mamlaka ya kusimamia Utumishi wa Umma na mamlaka ya rufaa ya watumishi wa umma ambao hawateuliwi na Rais. Rejea kielelezo Na 2.1. Kielelezo Namba 2.1: Kinaonesha ibara ya 36 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwisho ibara ya 36(4) ya Katiba inampatia mamlaka Rais kuchukua hatua za kudhibiti nidhamu ya watumishi na utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano. 2.2.2 Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma, 1999 Tamko namba 1 hadi 7 la Sera husika linatoa tafsiri ya Utumishi wa Umma, misingi na malengo ya Utumishi wa Umma na maadili ya msingi ya uwepo wa Utumishi wa Umma. Pia, sera husika inaweka sifa za msingi za kujiunga kwenye Utumishi wa Umma, uwepo wa mipango ya watumishi, ajira na uteuzi. Vile vile uwepo wa mikataba ya ajira, upandishwaji wa madaraja, usimamizi wa tathmini ya utendaji kazi, mafunzo kazini, mahusiano kazini, mwenendo na nidhamu kazini, na majukumu ya msingi ya wadau wa Utumishi wa Umma. 2.2.3 Sheria ya Utumishi wa Umma sura ya 298, 2019 Kifungu cha 4-8 cha Sheria hii kinazungumzia usimamizi wa Utumishi wa Umma. Kifungu cha 9-20 cha sheria husika kinaanzisha Tume ya Utumishi wa Umma pamoja na masuala yanayohusiana na tume hiyo. Pia, kifungu cha 21-25 kinatoa ufafanuzi wa mamlaka ya Rais katika usimamizi wa Utumishi wa Umma. Aidha, kifungu cha 26-28 kinazungumzia masuala ya mafao ya hitimisho la kazi. Vilevile, kifungu cha 29-36 cha sheria kinatoa ufafanuzi wa masuala ya kiujumla ya kiutumishi kama kuumia kazini kwa watumishi wasio maafisa (operational services). 2.2.4 Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, 2004 Sheria hii imetungwa ili kuweka masharti ya kazi, vigezo vya msingi vya ajira, muundo kwa ajili ya majadiliano ya pamoja, kuweka mifumo ya kuzuia na kutatua migogoro na mambo mengine yanayofanana na hayo. Sheria hii inatumika kwa wafanyakazi wote ikiwa ni pamoja na wale wa sekta binafsi. 2.2.5 Sheria ya Taasisi za Kazi, 2004 Sheria hii imetungwa kwa ajili ya kuanzisha Taasisi za kutolea maamuzi mbalimbali ya kiutumishi na ajira kama vile Kamisheni ya Usuluhishi na Uamuzi ikiainisha mamlaka na wajibu wake na mambo mengine yanayofanana na hayo. 2.2.6 Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009 Kanuni hizi zimebeba masharti ya ujumla katika Utumishi wa Umma na zimetengenezwa chini ya kifungu cha 35 (5) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 (2002). Kanuni hizi ni toleo la tatu na zilianza kutumika rasmi tarehe 1 Julai, 2009. Kanuni hizi zinatoa ufafanuzi wa masuala mengi ya kiutumishi kama vile ajira, uteuzi, nidhamu, kuthibitisha kazini watumishi, likizo, matibabu, mafunzo, mitihani, posho mbalimbali, mikopo ya watumishi, nyumba na samani na uendeshaji wa jumla wa Utumishi wa Umma. 2.2.7 Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003 Kanuni hizi zimetungwa chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma, 2002. Kanuni zinaeleza masuala ya msingi yanayohusu ajira au uteuzi wa watumishi wa umma, kuthibitishwa kazini; tathmini ya utendaji kazi; kupandishwa cheo; kusitishwa kwa ajira; nidhamu; rufaa; kanuni za maadili za watumishi wa umma; na mafao ya kustaafu. Pia, kanuni zinaeleza majukumu ya Tume ya Utumishi wa Umma. Angalizo Licha ya uwepo wa sheria zilizotajwa hapo juu, unatakiwa kuzisoma na kuzifahamu sheria nyingine zinazohusu maeneo maalum kama kuumia kazini, hitimisho la kazi, Sheria ya Usalama wa Taifa, Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria ya Ulipwaji wa Hasara na Fidia alizozisababisha mtumishi kwa serikali. 2.3 Haki na Wajibu wa Mtumishi wa Umma Mtumishi wa Umma una wajibu wa kutumia elimu, ujuzi na bidii katika kutoa huduma bora kwa wananchi. Kadhalika una haki na stahiki mbalimbali unazopaswa kuzipata kutoka kwa mwajiri wako kama ifuatavyo:- 2.3.1 Kupewa Mkataba wa Kazi (Barua ya Ajira) Mtumishi wa Umma una haki ya kupewa barua ya ajira inayoonesha jina lako, anuani yako, tarehe ya ajira, aina ya ajira, cheo, ngazi ya mshahara, kiwango cha mshahara na masharti mengine ya ajira yako [Rejea Kanuni D.32 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009]. 2.3.2 Posho ya Kujikimu Unapoajiriwa kwa mara ya kwanza unastahili kulipwa posho ya kujikimu ya siku 7 kwa ajili yako,. (Rejea Kanuni ya L. 6. Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2011). Aidha, unastahili kupata posho ya njiani kwa safari inayozidi masaa sita (6). Posho hii hulipwa kwa kiwango cha nusu ya posho ya kujikimu ya siku moja [Rejea Kanuni L. 2(3) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009]. 2.3.3 Kuthibitishwa Kazini Una haki ya kuthibitishwa kazini baada ya kipindi cha majaribio kisichozidi miezi kumi na mbili (12) chenye lengo la kupima tabia na utendaji wako wa kazi. Miezi mitatu (3) kabla ya muda wa majaribio kuisha, msimamizi wako wa kazi anapaswa kuamua kama: Uthibitishwe kazini, au Uongezewe muda wa majaribio, au Ajira yako isitishwe. Rejea Kanuni ya 14 (1) na (2) (a), (b) na (c) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003 na Kanuni D.40 na D.43 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009. 2.3.4 Likizo Maalum (Ruhusa) Una haki ya kupewa ruhusa isiyozidi siku kumi na nne (14) kwa mwaka ili kushughulikia matatizo na masuala mbalimbali ambayo hayaepukiki kama vile msiba wa ndugu wa karibu ambao ni pamoja na baba, mama, mwenza na mtoto, kushiriki vikao vya vyama vya wafanyakazi, michezo, kuuguza, kufunga ndoa n.k. Iwapo utaomba ruhusa zaidi ya muda huo basi siku zitakazozidi siku kumi na nne (14) ni lazima zikatwe kutoka kwenye likizo yako ya mwaka. Ni kosa kuomba ruhusa kufanya shughuli binafsi kama kulima, biashara, kufuga, kueneza dini au kufanya siasa kwani ni wizi wa muda wa serikali (Rejea Kanuni H.14 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009). 2.3.5 Likizo ya Mwaka Baada ya kupita miezi nane (8) tangu ulipoajiriwa unastahili kwenda likizo ya mwaka ya siku ishirini na nane (28) ikijumuisha siku za Jumamosi na Jumapili na siku za sikukuu. Katika likizo hiyo, wewe, mwenza wako na watoto au wategemezi wasiozidi wanne mtakuwa na haki ya kulipwa nauli kwenda na kurudi kwenye makazi yako ya kudumu mara moja ndani ya kipindi cha miaka miwili cha mzunguko wako wa likizo [Rejea Kanuni H.1 (1), (2) na (3) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009 na Kanuni ya 97 (1) na (2) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003]. Iwapo mwajiri atazuia likizo yako ya mwaka utastahili kulipwa mshahara wa mwezi mmoja bila ya makato kama fidia [Rejea Kanuni ya 97(3) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003]. 2.3.6 Likizo ya Uzazi kwa Mwanamke Ikiwa wewe ni mwanamke unastahili likizo ya siku themanini na nne (84) au siku tisini na nane (98) (kama utajifungua watoto mapacha) ikiwa ni likizo ya uzazi mara moja ndani ya kipindi cha miaka mitatu. Likizo hii haitaingiliana na likizo yako ya kawaida ya mwaka na iwapo ujauzito utaharibika au mtoto kufariki ndani ya miezi kumi na mbili (12) baada ya kujifungua, utastahili haki ya likizo ya uzazi katika ujauzito utakaofuata bila kujali masharti ya miaka mitatu [Rejea Kanuni H.12 (1-7) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009]. Aidha, kama utajifungua kabla ya kutimiza miaka mitatu baada ya kujifungua utastahili wiki 6 ambazo ni sawa na siku (42) siku hizi zitakakatwa/hazitakatwa katika likizo yako ijayo kulingana na mzunguko wako wa likizo. 2.3.7 Likizo ya Uzazi kwa Mwanaume Ikiwa wewe ni mwanaume unastahili likizo ya uzazi ya anaglau siku tatu (3) mara moja ndani ya kipindi cha miaka mitatu (3) iwapo mke wako atakuwa amejifungua. Likizo hii inapaswa kuchukuliwa ndani ya siku 7 tangu mke wako alipojifungua na haitaingiliana na likizo ya mwaka [Rejea Kanuni ya H.13 (a) na (b) ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009]. 2.3.8 Likizo Bila Malipo Likizo hii hutolewa kwa muda usiozidi miaka mitatu (3) ili kukuwezesha kujiunga na mashirika ya umma, programu za kimataifa na mashirika ya kimataifa/ kitaifa yenye uhusiano na serikali. Ili kupata likizo hii ni sharti uwe umethibitishwa kazini na hauna mashauri ya kinidhamu. Maombi ya likizo hii hupelekwa kwa Katibu Mkuu Utumishi kupitia kwa mwajiri wako. Aidha, hupaswi kulipwa mshahara, kupandishwa daraja na stahiki zako zote zitasimamishwa katika kipindi chote cha likizo hii [Rejea Kanuni ya 99 (1) na (2), ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003, na Kanuni H.19 (1) na (2) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009]. 2.3.9 Likizo ya Ugonjwa Likizo hii hutolewa kwa mtumishi mgonjwa baada ya kupata mapendekezo ya daktari yakithibitisha kwamba unapaswa kupumzika. Hutolewa kwa muda wa mwaka mmoja kwa utaratibu wa miezi sita (6) ya mwanzo, ambapo utapokea mshahara kamili na miezi sita ya mwisho utapokea nusu mshahara. Endapo hutakuwa umepona katika kipindi cha mwaka mmoja utastaafishwa kazi kwa ugonjwa [Rejea Kanuni ya 100 (1-2) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003]. 2.3.10 Ruhusa ya Masomo Ruhusa hii hutolewa baada ya mwajiriwa mpya kufanya kazi zaidi ya miaka miwili. Unaweza kuruhusiwa kwenda masomoni baada ya kuomba kuwekwa kwenye mpango wa mafunzo wa Taasisi. Utaweza pia kuomba kugharamiwa na mwajiri au kujigharamia mwenyewe au kuomba ufadhili kupitia Bodi ya Mikopo n.k. Kwa kuwa nia ya masomo ni kukuendeleza kitaaluma, ni vema ukajiendeleza katika fani unayofanyia kazi (proffessional carrier development) [Rejea Kanuni ya G.7(1)(a-j) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009].kwa mujibu wa Mwongozo wa Uendeshaji wa Mafunzo kwa Watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa. Wa mwaka 2008 2.3.11 Ruhusa Kwenda Nje ya Kituo cha Kazi Huruhusiwi kutoka nje ya kituo chako cha kazi wakati wa saa za kazi bila ya ruhusa ya msimamizi wako. Pia, huruhusiwi kutoka nje ya kituo chako cha kazi kwenda nje ya mkoa wako bila ya ruhusa ya maandishi toka kwa mwajiri. Unapaswa kuomba ruhusa ya kwenda nje ya mkoa hata kama utasafiri siku za Jumamosi, Jumapili na siku za Sikukuu. Pia, huruhusiwi kusafiri nje ya nchi bila ya kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi [Rejea Kanuni ya F.17(1-2) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009]. 2.3.12 Likizo ya Kustaafu Utakapokaribia kustaafu utastahili kupewa likizo ya siku ishirini na nane (28) ili kukuwezesha kujiandaa kabla hujastaafu (Rejea Kanuni ya 102 ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003). 2.3.13 Kupanda Madaraja ya Utumishi wa Umma Kwa kuzingatia sifa za kimuundo, utendaji wa kazi, nidhamu kazini na uwepo wa bajeti ya mishahara mipya iliyotengwa na mwajiri, unastahili kupandishwa cheo (daraja) baada ya miaka mitatu tangu kuthibitishwa kazini au kila baada ya miaka mitatu (3) unapopanda kwa mara ya pili na kuendelea (Rejea Kanuni ya D.51 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009 na Waraka wa Katibu Mkuu Kumbukumbu CAC.45/257/01/E/83 wa tarehe 09 Septemba, 2013). Aidha, muda wa miaka mitatu (3) katika kupanda utategemea pia maagizo na maelekezo mbalimbali kutoka Ofisi ya Rais UTUMISHI katika kipindi cha utekelezaji wa IKAMA. 2.3.14 Matibabu Unastahili kugharamiwa na mwajiri wako matibabu ambayo hayagharamiwi na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Unastahili kulipwa posho ya kujikimu na nauli kwenda kutibiwa nje ya kituo chako cha kazi, endapo utapewa rufaa na daktari [Rejea Kanuni 1 (1-2) ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009]. Aidha, ukilazwa hustashili kulipwa posho ya kujikimu,. 2.3.15 Uhamisho Unaweza kuhamishwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine na kustahili kulipwa malipo yafuatayo: Posho ya kijikimu kwa siku 14 kwako, mwenza wako na nusu ya kiwango kwa watoto/wategemezi wako wasiozidi wanne. Posho ya usumbufu kwa kiwango cha asilimia kumi (10%) ya mshahara wako wa mwaka mzima Gharama ya kusafirisha mizigo kati ya tani 1.5 hadi tani 3 (kutegemea kiwango cha ngazi ya mshahara wa mtumishi) Posho ya kujikimu ukilala njiani Nauli Endapo utaomba kuhama kwa sababu zako mwenyewe na umeishi zaidi ya miaka mtano (5) katika kituo chako cha kazi, au katika mazingira maalum mtumishi anapokaribia kustaafu na amefanya kazi nje ya Mkoa wake kwa muda wa miaka 10 mfululizo au zaidi, basi utastahili malipo husika kama mwajiri anao uwezo [Rejea Kanuni ya 107(1-5) ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003 Kanuni J.4 na L.8 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009]. 2.3.16 Fidia ya Kuumia au Kufa Ukiwa Kazini Endapo utaumia au kufariki ukiwa kazini, utastahili kulipwa fidia kupitia Mfuko wa Fidia wa Watumishi (Rejea Kanuni ya 110 ya Kanuni za Utumishi wa Umma, 2003). 2.3.17 Mikopo Mbalimbali Una haki ya kukopa kwenye taasisi za kifedha/mikopo kwa makato ambayo kwa mwezi hayatazidi 2/3 ya mshahara wako. Hivyo basi, 1/3 ya mshahara wako ni lazima ibaki ili kukuwezesha kumudu maisha na kuondokana na mzigo wa madeni ili utekeleze majukumu yako ya kazi kwa ufanisi (Rejea Kanuni F.12 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009).ikisomwa pamoja na Ufafanuzi Kuhusu Utaratibu wa Kusiamamia Mikopo inayotolewa kwa Watumishi wa Umma na Serikali au Taasisi za Fedha,uliotolewa na Ofisi ya Rais Utumishi wa mwaka 2013. 2.3.18 Kushiriki Katika Shughuli za Vyama vya Wafanyakazi Una haki ya kujiunga na kuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi kama vile CHAKUHAWATA TALGWU, TUGHE, CWT na n.k Ni muhimu katika ushiriki huo, ukazingatia sheria na kujiepusha na migogoro na migomo isiyo ya kisheria (Rejea F.22 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009). 2.3.19 Posho ya Masaa ya Ziada Iwapo utapata kibali cha kufanya kazi zaidi ya muda wa kawaida wa masaa ya kazi na umeajiriwa ukiwa mtumishi asiye wa zamu kama vile watumishi wa kada za afya, walinzi n.k., utastahili kulipwa posho ya masaa ya ziada kwa kiwango kilichowekwa na serikali (Rejea Kanuni ya L.21-22 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009). 2.3.20 Posho ya Kukaimu Madaraka Iwapo utateuliwa kukaimu cheo cha madaraka kama vile Ukuu wa Idara au Ukurugenzi kwa zaidi mwezi mmoja (1) utastahili kulipwa posho ya kukaimu madaraka. Kiwango hicho ni tofauti ya mshahara wa cheo unachokaimu na mshahara wako wa cheo cha sasa (Rejea Kanuni ya L.15-18 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009) ikisomwa kwa pamoja na waraka wa Utumishi wa Umma Na.3,2018 Kuhusu Utaratibu wa Kukaimu Nafasi ya Uongozi. Pia, endapo mtumishi hajafika ngazi ya Afisa Mwandamizi atakaimishwa lakini hatastahili kulipwa posho ya madaraka na badala yake atakuwa katika kipindi cha kujifunza ‘Career Develeopment’ 2.3.21 Posho ya Nyumba Iwapo una haki ya kupewa nyumba kama vile mkurugenzi au mkuu wa idara na hujapewa nyumba wala kununua nyumba ya serikali, una haki ya kupewa posho ya nyumba kwa kiwango kilichowekwa na serikali kwa mwezi (Rejea Kanuni ya L.34 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009). 2.3.22 Posho ya Sare Iwapo wewe ni mtumishi wa kada zinazostahili kulipwa posho ya sare kama vile madaktari, wauguzi, wanasheria, makatibu mahsusi, walinzi n.k, utastahili posho hiyo kila mwaka kwa kiwango kilichowekwa na serikali.(Rejea Kanuni ya L.37 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009). 2.3.23 Posho ya Mavazi Iwapo utapata nafasi ya kwenda nje ya nchi kikazi au kimasomo unastahili kulipwa posho ya mavazi kwa kiwango kilichowekwa na serikali. Posho hiyo italipwa mara moja ndani ya miaka miwili ili kukuwezesha kununua mavazi maalumu yanayohitajika kwenye nchi unayokwenda (Rejea Kanuni ya L.20 ya Kanuni za Kudumu Katika Utumishi wa Umma, 2009). 2.3.24 Posho za Viongozi kiIwa utateuliwa kushika nafasi ya uongozi katika taasisi kama vile ukuu wa idara, kitengo au ukurugenzi utastahili posho ya simu, umeme na samani kwa kuzingatia viwango vinavyotolewa na serikali kwa mwezi. 2.3.25 Kuacha Kazi Una haki ya kuacha kazi kwa kutoa taarifa ya maandishi ya miezi 3 ya kusudio hilo au kutoa taarifa ya saa 24 ya kuacha kazi na kulipa mshahara wa mwezi husika (Rejea Kanuni ya F.49 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009). Angalizo Kwa kuzingatia Waraka wa Katibu Mkuu UTUMISHI Kumbukumbu Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010 iwapo utaacha kazi utapaswa kupata kibali cha kuajiriwa upya serikalini kama utaamua kuomba tena ajira serikalini. 2.3.26 Gharama za Mazishi Ikitokea mtumishi amefariki au kufiwa na mwenza au mtoto wako, mwajiri atagharamia jeneza, uchimbaji wa kaburi, sanda, manukato na mapambo na usafiri kwenda kuzikwa eneo la makazi yako ya kudumu au eneo lingine lolote atakalochagua mtumishi mwenyewe (Rejea Kanuni ya Q.7(1-3) ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009). 2.3.27 Mtumishi wa Umma Kugombea Nyadhifa za Kisiasa Unaruhusiwa kugombea nyadhifa za kisiasa kama udiwani, ubunge na urais. Hata hivyo utaratibu ni kama ifuatavyo:- Ukigombea nafasi ya ubunge katika jimbo la uchaguzi, ubunge wa viti maalumu, ubunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, mara baada ya Tume ya Uchaguzi kukutangaza kuwa mgombea wa ubunge, utalazimika kuacha kazi na utalipwa mafao yako. Ukigombea nafasi ya udiwani katika kata mara baada ya Tume ya uchaguzi kukutangaza kuwa mgombea wa udiwani, utalazimika kuacha kazi na utalipwa mafao yako. Ukiteuliwa na waziri mwenye dhamana na TAMISEMI kuwa diwani, utakuwa na hiari ya kuchukua likizo bila malipo kwa kipindi chote utakachokuwa diwani, au kuacha kazi na utalipwa mafao yako kuanzia siku utakayoteuliwa kuwa diwani. Ukigombea nafasi yoyote ya uongozi katika chama cha siasa utalazimika kuacha kazi na utalipwa mafao yako. Ukiteuliwa na Rais kuwa mbunge, utakuwa na hiari ya kuchukua likizo bila malipo kwa kipindi chote utakachokuwa mbunge au kuacha kazi na utalipwa mafao yako kuanzia siku utakayoteuliwa kuwa mbunge. Rejea Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na. 01, 2015 kuhusu utaratibu wa watumishi wa umma wanaogombea nyadhifa za kisiasa. 2.4 Makosa na Adhabu Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, zimeainisha mamlaka za nidhamu kwa makundi mbalimbali ya watumishi wa umma, aina ya makossa na adhabu zake. Mamlaka za nidhamu katika utumishi wa umma ni kama ifuatavyo: Rais ambaye ni mamlaka ya nidha

Comments

Popular posts from this blog

RIWAYA YA KISWAHILI NA SIFA ZAKE

KI 311 SEMANTIKI NA PRAGMATIKI YA KISWAHILI

SEMANTIKI NA PRAGMATIKI