Machapisho

MAMBO MHIMU KWA MWALIMU KWA MWAKA 2022

 Imeandikwa na MBEMBE J. S. EWE MWALIMU TUNAENDA MWAKA WA MASOMO 2022 TUJIEPUSHE NA MAMBO  HAYA ILITUEPUKE MIGOGORO BAINA YETU NA WATAALUMA, WAKUU NA HATA WAMILIKI KUPELEKEA KUTUFUKUZA KAZI kuacha kazi rahisi ila kazi kupata kazi TUSIWALAUMU VIONGOZI  TU HATA SIE WALIMU TUNAMAKOSA  baadhi Mambo ni*  1:Epuka Kufanya kazi kwa mazoea (jitahidi kuwa mbunifu mshawishi boss wako kwanini alikuajiri wewe na aliachakuajiri wengine  2: Epuka Makundi kazini kuwa mtu flexible unapenda story ila out of work hour na sio muendelezo  3:Epuka Kuingilia madaraka Ambayo wewe haya kuhusu ya kiuongozi  4: Wahi kazini na kuwa mnyumbufu pindi ufikapo kazini na siku moja moja shiriki majukumu ya usimamizi ya Mambo ya Mwl wa zamu hata kama sio mwl wa zamu  5: Tanguliza kujitolea kwanza hata pasipo kutamani malipo na jitoe kwa ajiri ya shule kwanza  6: kuzingatia na kutii maagizo ya mtaaluma na kuwasilisha kwa wakati Mfn lesson plan , scheme, lesson notes , teac...

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA DINI OSCAR KIHOMBO

 https://youtu.be/nu7OZZqL7Wo

MAMBO MATANO AMBAYO NIMECHELEWA KUYAJUA KUHUSU FEDHA*

 Na Isaack   Nsumba 1. Nimechelewa kujua kuwa fedha inaongea na mwenye nayo Fedha ina sauti, fedha inasema, fedha inaongea na mwenye nayo...kuna mambo huwezi isikia nafsi yako ikikutaka uyafanye kama huna fedha, ukiwa na fedha utaisikia nafsi yako ikikulazimu uyafanye, watu waliofanikiwa kifedha ni wale ambao walizishinda zile sauti mbaya zinazosema ndani yao mara baada ya kupata fedha, watu waliofeli ni wale ambao waliisikiliza sauti ya fedha na kuifuata kisha kufanya fedha ilivyowataka wafanye. 2. Nimechelewa kujua kuwa fedha haina uhusiano na kisomo. Ndio, fedha haina uhusisno hata kidogo na kisomo, ili mtu aweze kuipata fedha anahitaji elimu (ufahamu na maarifa) ili mtu aweze kuitunza na kuizalisha fedha anahitaji elimu pia (namna ya kuizalisha, kuitunza na kuisimamia "Financial Management Techiniques" ila haitaji kisomo, ndio maana tuna watu wengi wamesoma na hawana fedha walizoamini watapata mara baada ya kusoma, nimechelewa kujua kuwa wenye visomo wengi wanaongoza ...

BLACK IN AMERICA USIPITWE SOMA UELEWE

 Blessings in disguise Mungu anayefanya kazi zake in mysterious ways, anazo njia za kuwabariki watu wake kwa njia ambazo kwa macho yetu tunaona mateso na fedheha.  Chukua hii: Huyo jamaa anayesomeka kwenye cover ya kitabu kwenye picha ya kwanza anajulikana kwa jina la MALCOLM X. kwa walisoma historia ya watu weusi nchini marekani lazima amefahamu wanaharakati wawili wa haki za watu weusi waliokuwa maarufu miaka ya 1950s na 1960s. Wa kwanza alijulikana kama Martin Luther king Jr (siyo yule wa Walutheri) wa pili aliitwa Malcolm X.  Malcom aliwahi kufungwa jela kwa sababu ya harakati zake za kupigania haki za watu weusi. Wakati mwenzake Martin Luther king Jr aliamini kwamba haki itapatikana bila umwagaji damu yaani kwa njia ya amani (ikumbukwe King alikuwa Reverend pastor) Malcolm yeye aliamini dawa ya moto ni moto, akupigaye ngumi inabidi umrudishie ngumi. Kati ya nukuu zake maarufu "sometimes you have to pick the gun up to put the gun down" (wakati mwingine inabidi uchukue...

USITESEKE NA MWEZI JANUARY NA ADA

 SIKIA;  Kama hauna hela ya kumpeleka mtoto wako shule za gharama (ada kubwa) ambazo inasemekana zinatoa elimu bora kuliko hizi zetu za Serikali, Basi mlete tu shule za serikali kisha fanya yafuatayo.    1- hakikisha umemnunulia uniform kuanzia 3 Ili awe msafi kila siku shuleni, usafi huleta kujiamini kwa mwanafunzi (maana hata hao wa kimataifa ukiwatazama physically usafi kwao namba 1). Mnunulie sox pea 5, mashati 3 sketi/bukta 2 Ili Kati Kati ya wiki ziwe zinafuliwa , hakikisha zinapigwa pasi na kama unaweza tupiamo hata dodorant ya Buku 5, unajua hizi shule za serikali unakuta watoto wachafu, kola nyeusi, uniform imechanika n.k Sasa ile inaua confidence ya mtoto ,kumbuka hata walimu wanapenda wanafunzi wasafi.   2- kiherehere smart hakikisha unakua karibu na walimu wake,haswa ikiwezekana uhakikishe anakaa dawati la mbele darasani, au ambapo mwl atamfikia au kumuona kirahisi, kuna faida ya kukaa dawati la mbele achana na back benchers tabia zao tunazikumbuka n...

TUSIMLAUMU MAGUFULI TUJILAUMU WENYEWE

  Watanzania wa kipindi cha kwanza cha mkapa watakubaliana nami kuwa mazoea yanaharibu sana fikla za jamii, kipindi cha kwanza cha mkapa nchi ilikuwa imetoka katika uongozi wa ruksa maana yake nchi ilikuwa haina mifumo imara hivyo alipoingia mkapa alisababisha watu wengi kuanza kuona kwamba mkapa amewaharibia biashara na ndipo kodi nyingi zilianzishwa za sehemu mbalimbali watu walikimbia kwa sababu watu waliokuwa hawana shughuli zaidi ya uzurulaji na ujanja ujanja walimchukia sana jamaa lakini matokea yake yalionekana baadaye nchi ilianza kujiendesha. Sasa vijana wa leo nao wanarudi kulekule ambako tulitoka na ndio maana naanza kukubaliana na msemo samaki mkunje angali mbichi na tatizo hili linaanzia kwenye mifumo ya sheria kuoneka nzuri anapopatikana rais mpole na kuonekana mbaya na kandamizi akipatikana anayezisimamia sawia. Wote mashahidi kwamba sheria za kodi hazijabadika hata kidogo bali kuna udhibiti na ukomeshwaji wa rushwa kwenye biashara, kwa sasa maghendo,rushwa,kukwepa k...

UCHAGUZI TANZANIA 2020

Picha
  KWA MOJA YA TV MEDIA CENTER Uchaguzi Mkuu Tanzania 2020 Joto la uchaguzi nchini Tanzania linazidi kupanda ambapo taifa hilo la Afrika Mashariki linafanya uchaguzi wake wa tano tangu kuasisiwa kwa demokrasia ya vyama vingi zaidi ya miongo miwili iliyopita. Nchini Tanzania vyama vya siasa vimekamilisha michakato ya ndani ya kuwatafuta makada watakaoviwakilisha vyama vyao katika uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2020. Uchaguzi huo ni wa tano kufanyika tangu kuasisiwa kwa demokrasia ya vyama vingi 1995, zaidi ya miongo miwili iliyopita.