BLACK IN AMERICA USIPITWE SOMA UELEWE

 Blessings in disguise


Mungu anayefanya kazi zake in mysterious ways, anazo njia za kuwabariki watu wake kwa njia ambazo kwa macho yetu tunaona mateso na fedheha. 


Chukua hii:


Huyo jamaa anayesomeka kwenye cover ya kitabu kwenye picha ya kwanza anajulikana kwa jina la MALCOLM X.


kwa walisoma historia ya watu weusi nchini marekani lazima amefahamu wanaharakati wawili wa haki za watu weusi waliokuwa maarufu miaka ya 1950s na 1960s. Wa kwanza alijulikana kama Martin Luther king Jr (siyo yule wa Walutheri) wa pili aliitwa Malcolm X. 


Malcom aliwahi kufungwa jela kwa sababu ya harakati zake za kupigania haki za watu weusi. Wakati mwenzake Martin Luther king Jr aliamini kwamba haki itapatikana bila umwagaji damu yaani kwa njia ya amani (ikumbukwe King alikuwa Reverend pastor) Malcolm yeye aliamini dawa ya moto ni moto, akupigaye ngumi inabidi umrudishie ngumi. Kati ya nukuu zake maarufu "sometimes you have to pick the gun up to put the gun down" (wakati mwingine inabidi uchukue bunduki Ili kushusha bunduki chini" 


Lesson: Huyu mwamba aliwahi kufungwa jela kwa takribani miaka sita na ushee. Akiwa jela alipata fursa ya kujisomea vitabu mbalimbali, alijielimisha akiwa jela kwa hakuwahi kusoma. Alisomea jela. By the time anatoka alikuwa mwelewa wa mambo mengi sana. 


Mh. Mbowe asingekuwa mahabusu kwa muda huo wote naamini asingepata muda wa kutosha wa kusoma vitabu kama anavyofanya hivi Sasa. Kila mara anatuonesha kitabu kipya anachokisoma. Kama alivyosema Malcolm kuwa kitabu kimoja kinatosha kumbadilisha mtu akawa mwingine kabisa. Kwahiyo mahabusu ya Mbowe inaweza kuwa imegeuka shule ya kunoa ubongo wake. 


Kwenye Biblia tunaona ndugu wenye chuki wakishauriana kumuua ndugu Yao lakini wakakubaliana kumuuza kwa Wamisri, Hatimaye Yusuph alikuwa Waziri Mkuu huko Misri na akawasaidia wale ndugu waliomchukia wakati wa njaa. 


Aliwahi kusema Rugemalira Mutahaba (Ruge Mutahaba): Katika maisha ya sasa ogopa mambo mawili. 1. Mungu 2. Teknolojia


Mimi nasema: Mungu anaweza kukuletea changamoto itakayokuumiza nafsi na akili Ili kukutoa kwenye confort zone yako ILI aku-Rechannel kwenye destiny iliyo Bora zaidi. Katika hili ninao marafiki wawili.wa kwanza, ilibidi kufukuzwa kazi kwenye taasisi aliyofanyia kazi kwa muda nrefu, akawa jobless lakini Hatimaye alipata kazi kwenye taasisi iliyothamini uwezo wake na akapata maisha Bora zaidi.  Wa pili ilibidi afukuzwe ghafla kwenye kampuni aliyofanyia kazi kwa takribani miaka 8 Ndipo alipopata akili ya kujiajiri. Leo hii anamshukuru aliyemfukuza kazi kwani bila hivyo angebaki masikini. 


Katika maisha yawezekana ukakutana na push factor ikakuumiza sana lakini amini utaimarika na kuwa Bora kuliko mwanzo. Don't let challenges/problems break you. Stand tall. Walk tall. Never quit. Keep pushing. Fight meaningful fight for your dignity and well-being. 


Amini Mungu wako hatakuacha.

Comments

Popular posts from this blog

RIWAYA YA KISWAHILI NA SIFA ZAKE

KI 311 SEMANTIKI NA PRAGMATIKI YA KISWAHILI

SEMANTIKI NA PRAGMATIKI