TUSIMLAUMU MAGUFULI TUJILAUMU WENYEWE

 Watanzania wa kipindi cha kwanza cha mkapa watakubaliana nami kuwa mazoea yanaharibu sana fikla za jamii, kipindi cha kwanza cha mkapa nchi ilikuwa imetoka katika uongozi wa ruksa maana yake nchi ilikuwa haina mifumo imara hivyo alipoingia mkapa alisababisha watu wengi kuanza kuona kwamba mkapa amewaharibia biashara na ndipo kodi nyingi zilianzishwa za sehemu mbalimbali watu walikimbia kwa sababu watu waliokuwa hawana shughuli zaidi ya uzurulaji na ujanja ujanja walimchukia sana jamaa lakini matokea yake yalionekana baadaye nchi ilianza kujiendesha. Sasa vijana wa leo nao wanarudi kulekule ambako tulitoka na ndio maana naanza kukubaliana na msemo samaki mkunje angali mbichi na tatizo hili linaanzia kwenye mifumo ya sheria kuoneka nzuri anapopatikana rais mpole na kuonekana mbaya na kandamizi akipatikana anayezisimamia sawia.


Wote mashahidi kwamba sheria za kodi hazijabadika hata kidogo bali kuna udhibiti na ukomeshwaji wa rushwa kwenye biashara, kwa sasa maghendo,rushwa,kukwepa kodi ni mwiba mchungu kwa wafanyabiashara kwa sababu ndiyo ilikuwa nyenzo kuu za biashara,
sheria ya manunuzi ya umma ilikuwa ni kichaka cha upigaji kwa wahasibu wakandarasi na mainjinia haya yote yalifanya maisha yawe rahisi kwa walio wachache na kutokuwa na mwanga kwa walio wengi na nchi ilikuwa kama mshumaa unaomulika huku ukiteketea na kuisha. Kama kweli Watanzania tunataka mabadiliko tuachane na tabia ya kuchagua kwa kutaka urahisi wa mambo tusijizoweshe kulishwa tujaribu kujitafutia rais Magufuli hajabadili chochote kuhusu sheria za kodi yeye alichofanya ni kuwaonyesha namna sheria zinapaswa kusimamiwa kama ambavyo ulaya wanazisimamia , isipokuwa kwamba watanzania wameshakuwa samaki mkavu ,walishazoeshwa kupata mali kwa njia zisizo halali na hwazitolei jasho hivyo anapopatikana mtu anayetaka
utaratibu ufuatwe anaonekana ni kikwazo jamani tujifunze kutafuta kwa kufuata sheria

Comments

Popular posts from this blog

RIWAYA YA KISWAHILI NA SIFA ZAKE

KI 311 SEMANTIKI NA PRAGMATIKI YA KISWAHILI

SEMANTIKI NA PRAGMATIKI