USITESEKE NA MWEZI JANUARY NA ADA
SIKIA;
Kama hauna hela ya kumpeleka mtoto wako shule za gharama (ada kubwa) ambazo inasemekana zinatoa elimu bora kuliko hizi zetu za Serikali, Basi mlete tu shule za serikali kisha fanya yafuatayo.
1- hakikisha umemnunulia uniform kuanzia 3 Ili awe msafi kila siku shuleni, usafi huleta kujiamini kwa mwanafunzi (maana hata hao wa kimataifa ukiwatazama physically usafi kwao namba 1). Mnunulie sox pea 5, mashati 3 sketi/bukta 2 Ili Kati Kati ya wiki ziwe zinafuliwa , hakikisha zinapigwa pasi na kama unaweza tupiamo hata dodorant ya Buku 5, unajua hizi shule za serikali unakuta watoto wachafu, kola nyeusi, uniform imechanika n.k Sasa ile inaua confidence ya mtoto ,kumbuka hata walimu wanapenda wanafunzi wasafi.
2- kiherehere smart hakikisha unakua karibu na walimu wake,haswa ikiwezekana uhakikishe anakaa dawati la mbele darasani, au ambapo mwl atamfikia au kumuona kirahisi, kuna faida ya kukaa dawati la mbele achana na back benchers tabia zao tunazikumbuka na tunasikia.
3- hakikisha unafuatilia maendeleo yake darasani, hakikisha kila siku unakagua daftari zake, akusimulie amefundishwa nini na akufafanulie.
4- hakikisha unafahamu udhaifu wake, kama ni kwenye somo la hesabu au kiingereza tumia nguvu ya ziada (Tuition), fanya juu chini apate ufahamu zaidi.
5- Hakikisha anakula chakula chenye virutubisho, Mfano asubuhi ale walau viazi vya kuchemsha kabla hajaenda shule, mayai , mchicha na maji mengi (unashangaa nini ? Si ilikua ulipe ada ya sh. Milioni 2 kwa mwaka? Sasa hiyo ada wekeza kwenye misosi, uniform Safi na tuition)
6-Hakikisha unampa mtoto muda wa kucheza , usimbane, hakikisha anacheza, anaenda maeneo ya kutoa mawazo kama kuchota maji,kubembea pia hakikisha unamnunulia japo kampira ka sh 25,00/=nyumban,akiwa nyumban kuweka Chanel za katuni n.k
7.Shirikiana na kamati ya shule na wananchi na wazazi ktk kuhakikisha shule anayosoma mwanao inakuwa ktk mazingira sahihi ya kujifunzia na kufundishia, shirikini ktk ujenzi wa madarasa ya kutosha, Ofisi za Walimu, Viwanja vya michezo, nk. Shule ikiwa nzuri italeta mvuto kuhakikisha mwanao anasoma vyema zaidi. Hakikisheni hakuna mrundikano wa wanafunzi ktk madarasa.
Hali hii ukienda nayo kuanzia shule ya msingi mpaka shule ya sekondari, Basi mwanao atakuja kukutana UDSM au UDOM au SAUT na mtoto mwingine aliyesoma shule zenye gharama au zenye school bus na hapo hakutakua na wa kumcheka mwenzake, kizuri zaidi wakihitimu, Ili kupata ajira , waajiri hawaangalii huyu kasoma wapi, wanaangalia Brain, pia kukiwa na Tangazo la ajira wanatakiwa watu 20, kati ya watu elfu kumi mtakao-apply, wamo wa shule za kimataifa na mwanao aliyesoma shule setu za Serikali
Najua utakuja kunishukuru baadae π
NB:Shule nzuri zinaleta morali kwa mtoto lakin Kama uwezo unabana jaribu kufuata kanuni hizo hapo juu mwanao atakua mwenye furaha na atafaulu vizur darasan kila akifanya mtihan
Nakutakia maandaliz mema ya ulipaji Ada katika week hii ya mwisho ya likizo ya mwanaoπ π€π........
KAZI NJEMA
Comments
Post a Comment
Tafadhari usicomment matusi