MAMBO MHIMU KWA MWALIMU KWA MWAKA 2022
Imeandikwa na MBEMBE J. S. EWE MWALIMU TUNAENDA MWAKA WA MASOMO 2022 TUJIEPUSHE NA MAMBO HAYA ILITUEPUKE MIGOGORO BAINA YETU NA WATAALUMA, WAKUU NA HATA WAMILIKI KUPELEKEA KUTUFUKUZA KAZI kuacha kazi rahisi ila kazi kupata kazi TUSIWALAUMU VIONGOZI TU HATA SIE WALIMU TUNAMAKOSA baadhi Mambo ni*
1:Epuka Kufanya kazi kwa mazoea (jitahidi kuwa mbunifu mshawishi boss wako kwanini alikuajiri wewe na aliachakuajiri wengine
2: Epuka Makundi kazini kuwa mtu flexible unapenda story ila out of work hour na sio muendelezo
3:Epuka Kuingilia madaraka Ambayo wewe haya kuhusu ya kiuongozi
4: Wahi kazini na kuwa mnyumbufu pindi ufikapo kazini na siku moja moja shiriki majukumu ya usimamizi ya Mambo ya Mwl wa zamu hata kama sio mwl wa zamu
5: Tanguliza kujitolea kwanza hata pasipo kutamani malipo na jitoe kwa ajiri ya shule kwanza
6: kuzingatia na kutii maagizo ya mtaaluma na kuwasilisha kwa wakati Mfn lesson plan , scheme, lesson notes , teaching aid
7: Jishushe hata kama unaamini wewe unauwezo mkubwa wa jambo kuliko anaekuamlisha jambo .Hiki kipengere walimu wengi wanashindwa kukimudu hii huwachanzo kikubwa Cha migogoro kazini
8: Epuka mahusiano na wanafunzi walimu Bora hata uwe muhuni kila mtaa wanakujua lakini epuka kutembea na wanafunzi
9:Epuka kujibu jambo ikiwa umeulizwa kwa kughasiwa jaribu kufikiria kabla ya kujibu
10: Ongeza ushirikiano baina ya Walimu na wanafunzi na hata kwa Uongozi katika ushiriki wa Mambo mbalimbali juu ya shule yenu
11: Epuka migomo isiyofuata utaratibu katika shule kuwa flexible fanya kazi kama kunatatizo mfuate utaratibu wa kuwasilisha jambo lenu naamini hakuna taasisi isiyokuwa na utaratibu wa kupokea maoni au mawazo mapya kutoka kwa watumishi wao
12: jitoe katika kufundisha na amini matokeo ya shule ni matokeo yenu wote na kufanya vizuri kwa wanafunzi ni furaha ya Mwalimu na wazazi na ndio jukumu lako kuu mwl anaeamini hivi hata shule isilipe mishahara hata miezi 4 yeye anafundisha na anajitoa huyu ndo mwalimu mwenye wito wa UALIMU
13: Epuka mabifu kazini piga kazi kazi ya mabifu waachie wao we piga kazi mkutane kwenye matokeo ya watoto wetu
14 : Epuka majungu piga kazi Wacha waongee we piga kazi kuwa mwl mpya mwalimu ambae yupo busy na kazi huwa Hana muda wa kudiskas majungu
**USHAURI TU WALIMU WENZANGU TWENDENI 2022 TUKAPIGE KAZI*
Maoni
Chapisha Maoni
Tafadhari usicomment matusi