MAMBO MATANO AMBAYO NIMECHELEWA KUYAJUA KUHUSU FEDHA*

 Na Isaack   Nsumba

1. Nimechelewa kujua kuwa fedha inaongea na mwenye nayo


Fedha ina sauti, fedha inasema, fedha inaongea na mwenye nayo...kuna mambo huwezi isikia nafsi yako ikikutaka uyafanye kama huna fedha, ukiwa na fedha utaisikia nafsi yako ikikulazimu uyafanye, watu waliofanikiwa kifedha ni wale ambao walizishinda zile sauti mbaya zinazosema ndani yao mara baada ya kupata fedha, watu waliofeli ni wale ambao waliisikiliza sauti ya fedha na kuifuata kisha kufanya fedha ilivyowataka wafanye.



2. Nimechelewa kujua kuwa fedha haina uhusiano na kisomo.


Ndio, fedha haina uhusisno hata kidogo na kisomo, ili mtu aweze kuipata fedha anahitaji elimu (ufahamu na maarifa) ili mtu aweze kuitunza na kuizalisha fedha anahitaji elimu pia (namna ya kuizalisha, kuitunza na kuisimamia "Financial Management Techiniques" ila haitaji kisomo, ndio maana tuna watu wengi wamesoma na hawana fedha walizoamini watapata mara baada ya kusoma, nimechelewa kujua kuwa wenye visomo wengi wanaongoza kwa madeni.



3. Nimechelewa kujua kuwa fedha imejificha katika matatizo ya watu


Ndio, nimegundua kuwa mtu anaejihusisha na matatizo ya watu (sio kufuatilia maisha ya watu) katika namna ambayo inalenga kutafuta majibu ya matatizo yao basi ni rahisi sana fedha kumfuata na itaendelea kumfuata endapo hataacha kujihusisha na matatizo ya watu, nimechelewa kujua kuwa mtu anaekwepa matatizo ya watu amejiweka mbali na mfereji ambao fedha inapitia, kama unatatua matatizo hata kama huna kisomo fedha itakufuata tu!



4. Nimechelewa kujua kuwa fedha inatafutwa kwa siri na inatunzwa kwa siri.


Ndio, matajiri wote vifuani mwao wamebeba siri nzito kuhusu fedha inayowafanya wao waendelee kuwa matajiri, siri ambayo maskini anaendelea kuwa maskini kwa kutokuijua, nimechelewa kujua kuwa kama mtu akipewa fedha na hana siri za namna ya kuitunza basi ni suala la muda fedha itatoka kwake na atabaki kama mtu ambae hajawahi kuishika fedha, kuwa tayari kutafuta kuijua siri iliyojificha nyuma ya fedha ili kuipata na kuitunza.


5. Nimecjelewa kujua kuwa fedha haina ubaguzi.


Nilipokuwa mdogo nilidhani fedha inabagua watu, nilidhani kuna watu special ambao wameumbwa kuwa na fedha, nilichelewa sana kujua kuwa fedha haijawahi mbagua mtu ikiwa mtafutaji atafuata kanuni zote zinazovuta fedha kutoka katika mifuko ya watu kuja mfukoni kwake, nimechelewa sana kujua kiwa fedha ipo na inapatikana ikiwa itatafutwa kwa kufuata kanuni zote, moja ya kanuni inasema "Dont chase money, but Attract" fedha haikimbizwi, fedha inavutwa, Kama utakuwa unaikimbiza fedha basi itaendelea kukukimbia milele, kanuni ya kupata fedha haisemi tuikimbize fedha bali inatutaka tuivute fedha.


Hayo ni mambo matano niliyochelewa kuyajua kuhusu fedha, pamoja na kwamba nimechelewa kuyajua, najua bado sijachelewa kuanza kuyatendea kazi ili yanipe matokeo.


Comments

Popular posts from this blog

RIWAYA YA KISWAHILI NA SIFA ZAKE

KI 311 SEMANTIKI NA PRAGMATIKI YA KISWAHILI

SEMANTIKI NA PRAGMATIKI