TUNAKUTHAMINI TUNAKUPENDA NI FAHARI YETU KUKULETEA TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA SEHEMU TOFAUTITOFAUTI ZA DUNIA KUWA MJANJA KUPATA TAARIFA MAPEMA
**IJUE DUNIA YAKO MAPEMAAAAAA**
RIWAYA YA KISWAHILI NUKUU ZA SOMO: MAANA YA RIWAYA NA AINA ZA RIWAYA: Riwaya imefasiliwa na wataalamu mbalimbali miongoni mwao nikama vile, Encyclopedia Americana (EA), Jz. 20 (1982:510f) wakinukuliwa naMulokozi (1996) wanasema, riwaya kuwa ni hadithi ya kubuni inayotosha kuwa kitabu. Udhaifu; Maelezo haya yanaibua utata kwani hayafafanui kitabu kinapaswa kuwa na urefu kiasi gani. Matharani kwa mujibu wa UNESCO katika Mulokozi (1996) kitabu ni chapisho lolote lenye kurasa 48 au zaidi. Ama urefu wa kitabu hautegemei idadi ya kurasa tu pia unategemea ukubwa wa kurasa (upana na kina) ukubwa wa maandishi na mpangilio wake. Encyclopedia Britanica EB, Jz.8, (1985:810) wakinukuliwa naMulokozi (1996) wanaeleza kuwa, riwaya ni masimulizi marefu yakinathari yaliyochangamana kiasi, yenye kuzungumzia tajriba ...
Daniel Seni Academia.edu KI 311 SEMANTIKI NA PRAGMATIKI YA KISWAHILI DOWNLOAD 27 Seni, Daniel John/ An ordained pastor at Shekinah Presbyterian Church (T) Madale-/DSM. Contact him through +255769080629/+255786684062 or senishekinah@gmail.com 27 Mfano wa maswali; Familia yenu ina watu wangapi? Mbali na Wamasai ni watu gani wengine wanaojihusisha na ufugaji? 2. Matendo uneni yasiyo dhahiri Haya ni matendo ambayo aina ya sentensi haiwiani bali inakinzana. Kwa mfano:- Unaweza kumkopesha shilinga elfu kumi — sentensi hii kimuundo ni swali lakini dhima ni ombi. Kwa hiyo inafanya tendo uneni lisilo dhahiri. Mfano mwingine Njaa inaniuma sana — kimuundo sentensi hii inatoa inatoa taarifa lakini dhima ni kuomba chakula. Kwa hiyo katika muundo huu ni kuwepo kwa muundo tofauti na dhima. Aina za Matendo Uneni Austin (1962) ametaja aina tatu:- 1. Kile kisemwacho Aina hii inahusu usemi wa sentensi yoyote yenye maana inayoeleweka pia iwe na kitu kinachorejelewa. 2. Lengo...
HABARI NA HISTORIA YA KABILA LA WANGONI NA MGAWANYIKO WA MAJINA YAO. Kama ilivyokwisha kufafanua kwenye makala zilizopita juu ya kabila la Wangoni, kuwa ni moja ya kabila linalopaikana nchini Tanzania na sehemu zingine za kusini mwa bara la Afrika. Na kutokana na kabila hili kupita sehemu mbalimbali wakitokea kusini mwa Afrika mpaka Afrika ya kati na mashariki,kuna mengi ya kujua. Kimasingi kuna aina mbili za Wangoni, kuna Wangoni asilia na kuna Wangoni wa kujiita tu. Wangoni wa asili ni wale ambao chimbuko lako ni kusini mwa Afrika. Na Wangoni wa kujiita hawa ni wale wakazi waliokutwa kwenye maeneo yao na kuamua kujiita Wangoni kwa sababu mbalimbali ambazo wao walikuwa nazo(nitafafua hili kwa kina hapa chini). Kwa ujumla Yapo mengi sana ya kusimulia juu ya kabila hili la Wangoni. Ila kwa leo tutajadili mgawanyiko wa majina ya Wangoni. Ukweli ni kwamba, Wengi tumekuwa tukifahamu kuwa Wangoni wanapatikana mkoani Ruvuma hasa kwenye wilaya ya Songea. Na kutokana na kabila hili...
Maoni
Chapisha Maoni
Tafadhari usicomment matusi