FAIDA ZA KUNYWA MAJI ASUBUHI KABLA YA KUTUMIA CHOCHOTE
Miili yetu inaundwa na asilimia 70 ya maji, hivyo ni muhimu kunywa maji ya kutosha ili kuufanya mwili kufanya kazi vyema. Kunywa takriban Mililita 160 za maji kabla ya kuswaki au kula chochote mara tu unapoamka. Kunywa maji angalau dakika 30 kabla ya kula, lakini si ndani ya dakika 45 baada ya kifungua kinywa, chakula cha mchana au chakula cha jioni. Faida 8 Muhimu 1. Huondoa sumu mwilini Unywaji wa maji mengi husaidia kuondoa sumu mwilini kwani huwezesha viungo kama vile figo kufanya kazi yake vyema. Unapokunywa maji kabla ya kula chochote asubuhi utauwezesha mwili wako pia kujenga misuli na kuzalisha seli mpya za damu.