HACKER APEWA ZAWADI YA JEZI BAADA YA KUHACK WEBSITE YA BAYERN MUNIC
Bayern Munich wampa zawadi ya jezi shabiki aliye-hack website yao
Club ya Bayern Munich ya Ujerumani imetangaza kumpa zawadi ya jezi ya Bayern Munich iliyosainiwa na Thomas Muller shabiki aliyekuwa ame-hack website yao.
Shabiki huyo aliyejulikana kwa jina la Daniel Martin amepewa zawadi hiyo baada ya ku-hack website ya club na kukuta taarifa za siri zilitaka kuvuja kisha kutatua tatizo hilo na kuzuiwa taarifa muhimu za club kutovuja kisha kutoa taarifa kwa club.
Daniel ni mtaalam wa masuala ya usalama wa taarifa za mtandaoni na alikuwa na dhamira ya kutembelea website ya club yake pendwa ila akuta kuna tatizo la configurations ambalo lingepelekea kuvuja kwa taarifa za siri za club ikiwemo taarifa za fedha.
Thomas Muller
Shabiki huyo amepewa jezi ya Muller kwakuwa Muller ndio icon ya club kwa sasa akiwa amefunga magoli 228 katika michuano yote ambaye amechezea club hiyo
Comments
Post a Comment
Tafadhari usicomment matusi