MITAZAMO YA MWALIMU WA PHILOSOPHY KWA KIZAZI CHA LEO
inaandikwa na james chotamasege anana kwa kusema Ujumbe huu ni maalumu kwa waliobeba NA wanaokuza vinasaba vyangu....
Hali zinapozalishwa kuisha huwa ni kazi kubwa kuliko zikijiunda. Jitihada zozote huwa zinafanywa kuzisawazisha hali hizo zilizozalishwa, lakini baada ya kipindi Fulani, wafanya jitihada husika, ama hugundua kwa asili au kwa ushawishi wa matukio kuwa walio zitengeneza hali wapo kazini pia ,lakini katika maumbile tofauti na ni vigumu kuyagusa katika hali ya matamanio.
Ikifika hapo ,ama wahusika hujidanganya wao peke yao ,au na wenye matamanio pamoja nao. Ni vigumu sana kwa watu kukubali hali zilivyo, na kukubali zaidi wenye matamanio ya pamoja nao wakaelewa hali zote hazikuwepo au zilieleweka tofauti.
Uelewa na nafsi ni kazi kuvihuisianisha. Ni rahisi sana kujiapiza kwa majina ya kuogofya, makubwa na yenye picha yoyote kubwa, lakini ni vigumu kukubali kukutana na vitu vyenye majina hayo.
Kuchangia tabia au mifumo inayorandana, au hulka fulani na matamanio ndio misingi wa maisha ya jamii zenye miafaka.
Na ili kuiishi misingi hiyo ni muhimu sana kuzielewa tabia(kiwango cha uelewa, uimara wa imani, hali za kimaisha, vyanzo vya maisha na mifumo yao ya kujifunza na kujifunzia) za jamii hizo.
Miiko yao hasa inayohusu masuala ya uhuru na uhai hayahitaji kuwekewa mipaka kwani ni masuala ya asili. Kuyagusa lazima yatazalisha muelekeo mmoja. Vinginevyo lazima kuwe na utashi mbadala. Kwamba mwelekeo mmoja usidhuru mwelekeo mwingine.
Mikinzano mingi katika maisha ya jamii ni maslahi na sio hali halisi. Ukizingatia tabia au sifa za watu wanaounda jamii,mathalani yangu... Ni vigumu kusema muda wote unachokichakata(sio unachokifikiri), Kufikia hapo, mzunguko mzima wa maisha inakua utengenaji wa hali.
Tuzing'amue, tuzijadili na tuziseme hali halisi....'hata wanaopiga sana kampeni za kwenda mbinguni, wao wamejidhatiti sana... Zaidi kuishi duniani' Q.
Chapegasaipelele Chotamasege#@Igulubaisimaini$$$Lilinga
Baba usije ukatuulia watoto wetu bhana mi naupenda ugali wangu
ReplyDelete