VUMBI LA KONGO KUCHUNGUZWA NI AGIZO LA RAIS

k
atika hotuba yake rais amesema“Lishe bora ni muhimu kwa Jamii, Wajawazito tunawapa lishe bora ili watoe Watoto wenye afya lakini Watoto wakizaliwa wanatakiwa pia kutunzwa na hata wakifika umri wa balehe wanapaswa kutunzwa ili wazae Watoto wenye afya ila Watoto balehe tufanye tafiti tunakosea wapi? kwanini wanakuwa na lishe mbovu? je ni masuala yaliyoingia ya mitindo? nataka niwe sijui na six packs!? nataka sijui niwe slim nisizidi kilo ngapi? nataka sijui mbavu ikae hivi?. “Kwanini Watoto wetu wakifika wakati wa kuongeza Jamii wanahangaika, mara supu ya pweza…… tuna tatizo na mnalijua mnalificha, Watafiti fanyeni utafiti……. tatizo hili kwasababu halisemwi ni siri linaumiza zaidi Vijana wetu, mara sijui udongo wa Congo (vumbi la Mkongo), mara sijui kitu gani lakini tatizo kubwa lipo kwenye lishe, sasa Watafiti chunguzeni tunafanyaje Watoto wetu wawe Shababi” “Tukiacha hali iwe hivi tunakwenda kuwa na Taifa goigoi, lenye Watu lakini sio rasilimali Watu ni Watu ambao ni mzigo kwa Taifa, sio Watu ambao watazalisha kwa ajili ya Taifa, kuzalisha mali kusimamia uchumi lakini pia kuzalisha wenzao ili Taifa liendelee, tutafika pahali hapa hatumjui Mke nani na Mume nani?, twendeni tukasimamieni”

Comments

  1. Wazee was alikasusi VUMBI LA KONGO mpoooo

    ReplyDelete

Post a Comment

Tafadhari usicomment matusi

Popular posts from this blog

RIWAYA YA KISWAHILI NA SIFA ZAKE

KI 311 SEMANTIKI NA PRAGMATIKI YA KISWAHILI

SEMANTIKI NA PRAGMATIKI