*Je, Tsh. 5000/- inatosha kuendesha Chama Cha Wafanyakazi?* *Utangulizi* Makala haya yanalenga kujibu swali Hilo, ikiwa ada ya 5000 inatosha kuendesha Chama Huru Cha Wafanyakazi, kwa misingi ya kazi adhimu za Vyama husika. *Dhana ya Vyama Huru vya Wafanyakazi* Chama Cha Wafanyakazi Ni umoja wa wanachama, wanaoamua kuja pamoja kwa ajili ya kulinda na kutetea haki na maslahi. Hata Hivyo, nchi nyingi katikati ya majangwa ya Murzuq na Red, kulinda haki na maslahi si kazi ndogo, kwa kuwa, kazi ya Kwanza Ni _kulinda ajira zenyewe na hadhi yake_. *Kazi za Vyama Vya Wafanyakazi Ni Zipi?* Kwa muktadha wa Tanzania, na Afrika kwa ujumla, Chama Cha Wafanyakazi kinatarajiwa kufanya yafuatayo na ziada;- i) Kuwaunganisha Wafanyakazi wa kada husika wawe kitu kimoja. ii) Kuwawakilisha wanachama wake kwenye majadiliano Kati yao na mwajiri, eneo walipo, wilayani, mkoani na Taifa. Lakini inakwenda mbali zaidi, kwa kuwa dunia Haina visiwa kwa mantiki ya ajira, Wafanyakazi wa Tanzania wanapaswa ku...