Machapisho

KAIKA KUELEKEA MEI MOSI 2023 KILIO CHA WALIMU KIPO HAPA

WARAKA KWA SERIKALI KUHUSU WAALIMU, SERIKALI IWAJALI WALIMU Ni muda sasa umepita kukiwa na manung'uniko kwa walimu katika nyanja nyingi zinazohusu maslahi yao ikiwemo mishahara yao, stahiki zao na kunyima haki na kuonewa na kuchukuliwa kama watu wa shida na kila kiongozi. Kuna haja serikali kumwangalia mwalimu kwa jicho la tatu, walimu wanapitia wakati mgumu sana katika utendaji kazi wao. Nimejaribu kuorodhesha changamoto hizi ambazo kama serikali ikizitatua hasa katika bajeti ijayo, ili mwalimu naye aone faraja ya maisha Baadhi ya changamoto hizo ni; MISHAHARA Serikali ipitie a iboreshe kwa mapana mishahara ya walimu, suala hili limekuwa tatizo kwa muda mrefu ikiwa kuna manung'uniko makubwa juu ya mishahara kiduchu wanayopewa waalimu Mara kwa mara tumekuwa tukisikia "mama anaupiga mwingu" kwenye Elimu, lakini ukichunguza kwa kina na kwa mapana na hata ukiwasikiliza wanaosema hivyo wanaishi kutaja vyumba vya madarasa na mabweni au katika miundombinu tu, huwezi ...

WALIMU WA MPWAPWA WASHUKURU HALMASHAURI YA BAHI KWA MAWAZO YA KUINUA UFAURU

Picha
Katika kikao chao ambacho walimu wa mpwapwa waliomba kujifunza mbinu za kuinua taaluma ikiwa ni lengo la kuifanya dodoma mpya ya kielimu aidha katika hali isiyo ya kawaida walimu wameshangaa Bahi walivyoweza kushirikiana katika suala la kielimu kwa pamoja ikiwa kuanzia wazazi na viongozi wote katika idara mbalimbali. kwaherini bahi karibuni mpwapwa mwakani mtajifunza kwetu pia.

WALIMU WA MPWAPWA WAFANYA ZIARA YA KUJIFUNZA WILAYANI BAHI UNGANA NAMI KATIKA MATUKIO

Picha
matukio ya awali katika ukumbi. tumekaribiswa vzuri sana

YANGA WASHAONDOKA TAYARI

Club ya Yanga SC kwenda Tunisia leo Feb 7, 2023, Afisa habari afunguka haya “Tuna Wachezaji 25” February 7, 2023 Share 1 Min Read Club ya Yanga SC inaondoka leo kuelekea Tunisia kwa ajili ya kuanza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika US Monastir. Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe amesema Timu itaondoka na kikosi cha Wachezaji 25, Aboutwalib Mshery atasafiri na Timu kwa ajili ya kwenda Tunisia kupatiwa matibabu wakati Bernard Morrison atabaki Dar es Salaam akitibiwa nyonga. “Tuna Wachezaji 25 katika kikosi chetu lakini hawa 25 yupo pia Aboutwalib Mshery, Mshery anakwenda Tunisia kwa ajili ya matibabu”

MAANA YA SEMANTIKI, MAANA YA MAANA

Picha
15.1  Utangulizi Katika muhadhara huu, tunakusudia kuelezea semantiki. Awali neno semantiki lilitumika kumaanisha sayansi ya “maana” kwa ujumla, hivi kwamba ilishughulikiwa na wanafilosofia, wanasaikolojia, wanamantiki, wanaanthropolojia na wengineo. Baadaye stadi hii ilijishughulisha zaidi na maana katika muktadha wa mwanadamu. Katika muhadhara huu tutashughulikia semantiki katika muktadha huu yaani maana katika misingi ya kinadharia ya isimu. Madhumuni ya Muhadhara Baada ya kumaliza kusoma muhadhara huu, mwanafunzi ataweza: (i)     Kueleza maana ya maana (ii)   Kuainisha aina za maana (iii)  Kueleza na kutofautisha uhusiano wa maana (iv) Kueleza dhana ya maana kiutendaji  15.2 Maana  Neno maana linafahiwa nyingi. Watu wa kawaida wamelitumia kumaanisha vitu mbalimbali: Una maana gani kwa kufika umechelewa Yale mawingu meusi yana maana mvua itanyesha sasa hivi Hiyo nguo nyekundu inamaanisha hatari Mradi huu una maana kubwa “Baba” maana ...

FAIDA ZA KUNYWA MAJI ASUBUHI KABLA YA KUTUMIA CHOCHOTE

Picha
  Miili yetu inaundwa na asilimia 70 ya maji, hivyo ni muhimu kunywa maji ya kutosha ili kuufanya mwili kufanya kazi vyema. Kunywa takriban Mililita 160 za maji kabla ya kuswaki au kula chochote mara tu unapoamka. Kunywa maji angalau dakika 30 kabla ya kula, lakini si ndani ya dakika 45 baada ya kifungua kinywa, chakula cha mchana au chakula cha jioni. Faida 8 Muhimu 1. Huondoa sumu mwilini Unywaji wa maji mengi husaidia kuondoa sumu mwilini kwani huwezesha viungo kama vile figo kufanya kazi yake vyema. Unapokunywa maji kabla ya kula chochote asubuhi utauwezesha mwili wako pia kujenga misuli na kuzalisha seli mpya za damu.