Machapisho

WALIMU WA MPWAPWA WASHUKURU HALMASHAURI YA BAHI KWA MAWAZO YA KUINUA UFAURU

Picha
Katika kikao chao ambacho walimu wa mpwapwa waliomba kujifunza mbinu za kuinua taaluma ikiwa ni lengo la kuifanya dodoma mpya ya kielimu aidha katika hali isiyo ya kawaida walimu wameshangaa Bahi walivyoweza kushirikiana katika suala la kielimu kwa pamoja ikiwa kuanzia wazazi na viongozi wote katika idara mbalimbali. kwaherini bahi karibuni mpwapwa mwakani mtajifunza kwetu pia.

WALIMU WA MPWAPWA WAFANYA ZIARA YA KUJIFUNZA WILAYANI BAHI UNGANA NAMI KATIKA MATUKIO

Picha
matukio ya awali katika ukumbi. tumekaribiswa vzuri sana

YANGA WASHAONDOKA TAYARI

Club ya Yanga SC kwenda Tunisia leo Feb 7, 2023, Afisa habari afunguka haya “Tuna Wachezaji 25” February 7, 2023 Share 1 Min Read Club ya Yanga SC inaondoka leo kuelekea Tunisia kwa ajili ya kuanza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika US Monastir. Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe amesema Timu itaondoka na kikosi cha Wachezaji 25, Aboutwalib Mshery atasafiri na Timu kwa ajili ya kwenda Tunisia kupatiwa matibabu wakati Bernard Morrison atabaki Dar es Salaam akitibiwa nyonga. “Tuna Wachezaji 25 katika kikosi chetu lakini hawa 25 yupo pia Aboutwalib Mshery, Mshery anakwenda Tunisia kwa ajili ya matibabu”

MAANA YA SEMANTIKI, MAANA YA MAANA

Picha
15.1  Utangulizi Katika muhadhara huu, tunakusudia kuelezea semantiki. Awali neno semantiki lilitumika kumaanisha sayansi ya “maana” kwa ujumla, hivi kwamba ilishughulikiwa na wanafilosofia, wanasaikolojia, wanamantiki, wanaanthropolojia na wengineo. Baadaye stadi hii ilijishughulisha zaidi na maana katika muktadha wa mwanadamu. Katika muhadhara huu tutashughulikia semantiki katika muktadha huu yaani maana katika misingi ya kinadharia ya isimu. Madhumuni ya Muhadhara Baada ya kumaliza kusoma muhadhara huu, mwanafunzi ataweza: (i)     Kueleza maana ya maana (ii)   Kuainisha aina za maana (iii)  Kueleza na kutofautisha uhusiano wa maana (iv) Kueleza dhana ya maana kiutendaji  15.2 Maana  Neno maana linafahiwa nyingi. Watu wa kawaida wamelitumia kumaanisha vitu mbalimbali: Una maana gani kwa kufika umechelewa Yale mawingu meusi yana maana mvua itanyesha sasa hivi Hiyo nguo nyekundu inamaanisha hatari Mradi huu una maana kubwa “Baba” maana ...

FAIDA ZA KUNYWA MAJI ASUBUHI KABLA YA KUTUMIA CHOCHOTE

Picha
  Miili yetu inaundwa na asilimia 70 ya maji, hivyo ni muhimu kunywa maji ya kutosha ili kuufanya mwili kufanya kazi vyema. Kunywa takriban Mililita 160 za maji kabla ya kuswaki au kula chochote mara tu unapoamka. Kunywa maji angalau dakika 30 kabla ya kula, lakini si ndani ya dakika 45 baada ya kifungua kinywa, chakula cha mchana au chakula cha jioni. Faida 8 Muhimu 1. Huondoa sumu mwilini Unywaji wa maji mengi husaidia kuondoa sumu mwilini kwani huwezesha viungo kama vile figo kufanya kazi yake vyema. Unapokunywa maji kabla ya kula chochote asubuhi utauwezesha mwili wako pia kujenga misuli na kuzalisha seli mpya za damu.

FAHAMU JINSI PESA YA CWT INAVYOLIWA MWALIMU ANAUMIA

PESA YA MWALIMU INAVYOPIGWA NA VIONGOZI WA CWT  Na Thadei Ole Mushi.  Walimu wa nchi hii asilimia 90 uliwaambia kwa nn Viongozi wa CWT huwa wanapigana wenyewe kwa wenyewe hawawezi kukuambia na wala hawajui chochote.  Nataka leo usijiulize tena kwa nini wanapigana na kupelekana mahakamani kila siku…. Twende sawa na ripoti hii ifuatayo:-  1. RIPOTI YA CAG Tarehe 27/3/2017 Katibu mkuu kiongozi alimuomba CAG afanye ukaguzi kwenye chama cha Waalimu CWT. Ukaguzi ulijikita katika tuhuma dhidi ya Uongozi wa chama cha waalimu zinazohisu ubadhirifu wa fedha na mali za chama. Ukaguzi maalumu ulikagua taarifa za mapato na matumizi ya Chama, Uliangalia uhusiano uliopo kati ya Benki ya waalimu na waalimu wenyewe, uhusiano uliopo kati ya Mwalimu haouse na mwalimu mwenyewe. YALIYOBAINIKA. a) Hakuna mfumo mzuri wa wanachama unaoonyesha kumbukumbu za wanachama. Katiba ya CWT inaeleza kuwa kunatakiwa kuwe na aina nne za wanachama lakini CWT hawaonyeshi aina hizo za wanachama hivyo haij...

FANYA HIVI UKIIBIWA SIMU YAKO

Mambo matano unayotakiwa kufanya iwapo simu yako ya mkononi imeibiwa 20 Aprili 2022 simu CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Mtu yeyote yule anaweza kuibiwa simu Tunaburudika tukiwa mbali na nyumbani, tunapuuzilia mbali kutumia simu ya rununu kwa muda na tunapoangalia mfukoni, begi au mahali tulipoiweka, haipo tena. Wezi wanaweza kuwa na ujuzi mkubwa wa kuiba simu za mkononi kwa kipindi kifupi tu. Mbali na kutufanya tujisikie vibaya, wizi wa simu za mkononi unaweza kuathiri hati na data ya kibinafsi na kusababisha athari katika akiba zetu Zifuatazo ni hatua tano unazotakiwa kuchukua iwapo simu yako imeibwa. 1. Ifunge simu yako Iwapo simu yako ya mkononi itaibiwa, hatua ya kwanza ni kuzuia kifaa hicho mara baada ya kupotea, kwa mujibu wa Emilio Simoni, mtaalamu wa usalama wa kidijitali na mkurugenzi wa dfndr Lab, wa kikundi cha CyberLabs-PSafe. "Ni muhimu sana kuwasiliana na kampuni ya simu unayotumia na kuwaomba waifungie kwa muda na kuifanya simu isiweze kutumi...