Posts

Showing posts from 2021

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA DINI OSCAR KIHOMBO

 https://youtu.be/nu7OZZqL7Wo

MAMBO MATANO AMBAYO NIMECHELEWA KUYAJUA KUHUSU FEDHA*

 Na Isaack   Nsumba 1. Nimechelewa kujua kuwa fedha inaongea na mwenye nayo Fedha ina sauti, fedha inasema, fedha inaongea na mwenye nayo...kuna mambo huwezi isikia nafsi yako ikikutaka uyafanye kama huna fedha, ukiwa na fedha utaisikia nafsi yako ikikulazimu uyafanye, watu waliofanikiwa kifedha ni wale ambao walizishinda zile sauti mbaya zinazosema ndani yao mara baada ya kupata fedha, watu waliofeli ni wale ambao waliisikiliza sauti ya fedha na kuifuata kisha kufanya fedha ilivyowataka wafanye. 2. Nimechelewa kujua kuwa fedha haina uhusiano na kisomo. Ndio, fedha haina uhusisno hata kidogo na kisomo, ili mtu aweze kuipata fedha anahitaji elimu (ufahamu na maarifa) ili mtu aweze kuitunza na kuizalisha fedha anahitaji elimu pia (namna ya kuizalisha, kuitunza na kuisimamia "Financial Management Techiniques" ila haitaji kisomo, ndio maana tuna watu wengi wamesoma na hawana fedha walizoamini watapata mara baada ya kusoma, nimechelewa kujua kuwa wenye visomo wengi wanaongoza ...

BLACK IN AMERICA USIPITWE SOMA UELEWE

 Blessings in disguise Mungu anayefanya kazi zake in mysterious ways, anazo njia za kuwabariki watu wake kwa njia ambazo kwa macho yetu tunaona mateso na fedheha.  Chukua hii: Huyo jamaa anayesomeka kwenye cover ya kitabu kwenye picha ya kwanza anajulikana kwa jina la MALCOLM X. kwa walisoma historia ya watu weusi nchini marekani lazima amefahamu wanaharakati wawili wa haki za watu weusi waliokuwa maarufu miaka ya 1950s na 1960s. Wa kwanza alijulikana kama Martin Luther king Jr (siyo yule wa Walutheri) wa pili aliitwa Malcolm X.  Malcom aliwahi kufungwa jela kwa sababu ya harakati zake za kupigania haki za watu weusi. Wakati mwenzake Martin Luther king Jr aliamini kwamba haki itapatikana bila umwagaji damu yaani kwa njia ya amani (ikumbukwe King alikuwa Reverend pastor) Malcolm yeye aliamini dawa ya moto ni moto, akupigaye ngumi inabidi umrudishie ngumi. Kati ya nukuu zake maarufu "sometimes you have to pick the gun up to put the gun down" (wakati mwingine inabidi uchukue...

USITESEKE NA MWEZI JANUARY NA ADA

 SIKIA;  Kama hauna hela ya kumpeleka mtoto wako shule za gharama (ada kubwa) ambazo inasemekana zinatoa elimu bora kuliko hizi zetu za Serikali, Basi mlete tu shule za serikali kisha fanya yafuatayo.    1- hakikisha umemnunulia uniform kuanzia 3 Ili awe msafi kila siku shuleni, usafi huleta kujiamini kwa mwanafunzi (maana hata hao wa kimataifa ukiwatazama physically usafi kwao namba 1). Mnunulie sox pea 5, mashati 3 sketi/bukta 2 Ili Kati Kati ya wiki ziwe zinafuliwa , hakikisha zinapigwa pasi na kama unaweza tupiamo hata dodorant ya Buku 5, unajua hizi shule za serikali unakuta watoto wachafu, kola nyeusi, uniform imechanika n.k Sasa ile inaua confidence ya mtoto ,kumbuka hata walimu wanapenda wanafunzi wasafi.   2- kiherehere smart hakikisha unakua karibu na walimu wake,haswa ikiwezekana uhakikishe anakaa dawati la mbele darasani, au ambapo mwl atamfikia au kumuona kirahisi, kuna faida ya kukaa dawati la mbele achana na back benchers tabia zao tunazikumbuka n...