BABA MZAZI WA BEN SANANE AFUNGUKA HAYA SIKU chache baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, kuliambia Bunge kuwa Serikali haijui kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ben Saanane aliko na zaidi akipinga taarifa za kutekwa, familia ya kijana huyo imesema juhudi zao za kumtafuta zimegonga mwamba. Akizungumza Jumamosi, baba mzazi wa Ben Saanane, Focus Saanane, ameiomba Serikali pamoja na vyombo vya dola kusaidia juhudi za kumtafuta, kwani juhudi zao zimegonga mwamba na suala hilo lipo nje ya uwezo wao kwa sasa. "Toka mwanangu Ben apotee imepita miezi sita na hakuna jitihada zilizofanyika za kumtafuta, hata kama zimefanyika basi nguvu ni ndogo sana, hivyo basi, sisi kama familia tunaiomba Serikali pamoja na vyombo vya dola kusaidia juhudi za kumtafuta,” alisema. Suala la kutoweka kwa Ben Saanane liliibuka kwa mara nyingine wiki hii kiasi cha kutikisa mhimili wa Bunge, kabla ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, hajahitimisha kwa kusema kuwa Serika...