YANGA YAKAANGWA KILUMBA MBAO ZATUMIKA KUUNGUZA
Baada ya Jumamosi ya April 29 Simba kucheza mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Azam FC na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Mohamed Ibrahim dakika ya 48, Yanga leo walishuka dimba kucheza nusu fainali dhidi ya Mbao FC.
Yanga waliingia katika uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Mbao FC katika mchezo huo wa nusu fainali, kabla ya mchezo kumalizika Yanga ndio alikuwa Bingwa mtetezi wa michuano hiyo, kwa bahati mbaya Yanga amevuliwa Ubingwa kwa kufungwa goli 1-0 lililopatikana kwa beki wake Andrew Vincent kujifunga dakika ya 27.
Ushindi wa Mbao FC ambao wanaingia fainali hiyo kwa mara ya kwanza ikiwa ni msimu wao wa kwanza toka wapande kucheza Ligi Kuu, unaifanya sasa kukutana na Simba katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo ya Kombe la FA (ASFC) katika tarehe ambayo itatajwa na TFF.
Comments
Post a Comment
Tafadhari usicomment matusi