TWENDE NA TIMU KWENYE UCHAGUZI WA CWT 2025

*Na mwandishi wetu* *Sir PANCRAS MAHELA* *From SONGEA MC* *0767549833/0786549833* *VIONGOZI NA TIMU ZAO ZA KAMPEINI* Ngoja tuongelee kidogo hizi timu za kampeni mwaka huu nimezipenda sana hasa hapa *KAHAMA MJINI* Zamani ilizoeleka kamati yote ya uendeshaji inasafiri pamoja hawataki mtu mwingine aivuruge kiukweli hapa ilikuwa ngumu sana kuimega ila miaka ya hivi karibu hapa kahama mwenyekiti ana msafara wake *Ke* anakundi lake *Vu* anakundi lake na *Ki* anakundi lake hapa zinapigwa siasa safi tulipokuwa kata ya mwendakulima Jana pale mgodini kabla ya kuingia kahama MJINI walimu walikuwa na shauku kubwa kumsikiliza mgombea alifika ila sasa tulicholalamika wengi mgombea Ali *select* mwakilishi tu kuzungumza naye kana kwamba huyu mwakilishi amebeba Mawazo ya walimu wote poa najua kupunguza maswali na muda ila mkishinda mje kama mnavyopita sasa hivi kutusikiliza matatizo yetu halafu myafikishe kwa mwajiri wetu. *Wawakilishi nawaomba msiwaombe* *chochote hawa wagombea* Uongozi ni dhamana ya kubeba matatizo ya watu wengine nakuyapeleka mbele kidogo unapo muomba kumtoa upepo mtu unayetaka kumtuma majukumu yako kesho unafikiri atatumika kweli waacheni wajinadi kisha kama una buku muongezee hela ya mafuta fikiria mbeba matatizo yako anatembea kata zote kwa usafiri anatumia mafuta kiasi gani kwanza niwakuwapongeza kwa ujasiri nyie wawakilishi mtapata posho ya kikao siku ya mkutano Mkuu kadri ya wilaya yako. *DHANA YA KUBADILISHANA MADARAKA* katiba ipo wazi miaka mitano watu wagombee akishindaa tena kwa haki kwa figisu ndo siasa hizo nenda kasome maana ya Propaganda utaelewa kule *kwimba* mkoani mwanza mwenyekiti wetu amedumu miaka 20 akishinda tena ataenda 25 huyu atastafia hapa ila miaka yote wajumbe wake wanabadilika wana kwimba tunajivunia huyu mwenyekiti na tunaamini baada ya utumishi wake serikalini huyu atachukua ubunge live bila chenga. Lakini siyo miaka yote hiyo anagombea pekeyake hapana kunamwaka walipishana kura moja na mwenzake sijui mwaka huu itakuwaje ila ni mtu kweli kweli tuache huyu amekaa madarakani muda mrefu huyu hajakaa kagombee tu ndugu. *SIASA ZA CWT* Hapo zamani hapakuwa na chama chochote nchi hii kilikuwa na siasa safi na zinazofuatiliwa zaidi kama chaguzi za CWT sasa hivi tumeahuka kidogo tumezidiwa na watu wa TLS KWA AKINA MWAMBUKUSI HUKO. CWT ilikuwa kitovu cha viongozi wa serikali niwakumbushe kidogo mh PM WA NCHI Alipita Cwt , mama SITTA alipita Cwt Mohammed utali alikuwa DC mvomero alipita Cwt Mzee mkoba mwaka huu atakuwa mbunge naamini naye kapita CWT hadi sasa teuzi nyingi viongozi wa CWT wanajitokeza mnajua kwanini basi nikunuze chama hiki kilipika watu wa uhakika hata sasa bado wapo tukiamini tu maana ndo chama cha kada yetu. *KWANINI WATU WANAJITOA CWT* shida siyo makato hapa kuna shida nyingi ngoja nitaje chache:- 1. Kutafuta moja ya tatu ili aweze kujiongezea kidogo kwenye mkwanja wake ili akopesheke mfano mtu akiondolewa makato ya elfu 25 kwa mwezi anakitu anakipata anaweza kukopesheka akijumlisha na nyongeza Yake ya mwaka wengi walihama Cwt kwa ajili ya hili afisa mmoja GEITA HUKO ALINUKULIWA AKISEMA HILI MKIJA WENYEWE povu litakuwa kubwa 2. Kukosa nafasi za uongozi kwenye chama Cwt hapa napo pamefagia wengi kila akijaribu hawezi kumtoa aliyepo madarakani kafanya jitihada kashindwa kagombea wilayani, mkoani hadi taifa kashindwa anaamua kujitoa Cwt .kwaleo hizi zinatosha zingine zipo tunazijua *MAONI YA MWANDISHI KUHUSU CHAGUZI* Ni maoni yangu kwa wapiga kura msije mkawaondoa kamati ya uendeshaji wote punguzeni wawili watatu wengine wabaki ili pasiwe na wageni wote hii ni kwa nchi nzima akibaki mwenyekiti mhazini labda na vu au yoyote lakini ingizeni sura mpya ili tujue kweli umefanyika uchaguzi au fyekeni kiti, mhazini bakisheni wengine hapo kadri mlivyowapima wagombea wenu na mkoani iwe hivyo hivyo kuna kaujinga Fulani kanafanyika watu wa Mkoa wote sasa hivi wanakimbia wilayani kuomba kura kwa walimu watakaoshinda kwenye CHAGUZI watu wa Mkoa muda wenu bado waacheni kwanza hawa wa wilaya wanyukane wenyewe baadaye waje kwenu. Chapisho linalofuata litakuwa kesho la matumizi ya fedha za chama na kwanini watu wa nataka kuuana ili wapate nafasi Hapa *Simanjiro* mkoani Tanga mwenyekiti wa kitengo Ke kagombea ukatibu wa kitengo , katibu naye kagombea hapohapo na mweka hazina wa kitengo ke kagombea ukatibu kitengo Ke niliwahi kuwaambia Ke ndipo penyepesa rahisi tukutane kesho haina shida MNAOFANYA UCHAGUZI KESHO HONGERENI

Maoni

Chapisha Maoni

Tafadhari usicomment matusi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

RIWAYA YA KISWAHILI NA SIFA ZAKE

KI 311 SEMANTIKI NA PRAGMATIKI YA KISWAHILI

TANZU ZA USHAIRI WA KISWAHILI