MITAZAMO YA MWALIMU WA PHILOSOPHY KWA KIZAZI CHA LEO
inaandikwa na james chotamasege anana kwa kusema Ujumbe huu ni maalumu kwa waliobeba NA wanaokuza vinasaba vyangu.... Hali zinapozalishwa kuisha huwa ni kazi kubwa kuliko zikijiunda. Jitihada zozote huwa zinafanywa kuzisawazisha hali hizo zilizozalishwa, lakini baada ya kipindi Fulani, wafanya jitihada husika, ama hugundua kwa asili au kwa ushawishi wa matukio kuwa walio zitengeneza hali wapo kazini pia ,lakini katika maumbile tofauti na ni vigumu kuyagusa katika hali ya matamanio. Ikifika hapo ,ama wahusika hujidanganya wao peke yao ,au na wenye matamanio pamoja nao. Ni vigumu sana kwa watu kukubali hali zilivyo, na kukubali zaidi wenye matamanio ya pamoja nao wakaelewa hali zote hazikuwepo au zilieleweka tofauti. Uelewa na nafsi ni kazi kuvihuisianisha. Ni rahisi sana kujiapiza kwa majina ya kuogofya, makubwa na yenye picha yoyote kubwa, lakini ni vigumu kukubali kukutana na vitu vyenye majina hayo. Kuchangia tabia au mifumo inayorandana, au hulka fulani na matamanio ndio misin...