Na Isaack Nsumba 1. Nimechelewa kujua kuwa fedha inaongea na mwenye nayo Fedha ina sauti, fedha inasema, fedha inaongea na mwenye nayo...kuna mambo huwezi isikia nafsi yako ikikutaka uyafanye kama huna fedha, ukiwa na fedha utaisikia nafsi yako ikikulazimu uyafanye, watu waliofanikiwa kifedha ni wale ambao walizishinda zile sauti mbaya zinazosema ndani yao mara baada ya kupata fedha, watu waliofeli ni wale ambao waliisikiliza sauti ya fedha na kuifuata kisha kufanya fedha ilivyowataka wafanye. 2. Nimechelewa kujua kuwa fedha haina uhusiano na kisomo. Ndio, fedha haina uhusisno hata kidogo na kisomo, ili mtu aweze kuipata fedha anahitaji elimu (ufahamu na maarifa) ili mtu aweze kuitunza na kuizalisha fedha anahitaji elimu pia (namna ya kuizalisha, kuitunza na kuisimamia "Financial Management Techiniques" ila haitaji kisomo, ndio maana tuna watu wengi wamesoma na hawana fedha walizoamini watapata mara baada ya kusoma, nimechelewa kujua kuwa wenye visomo wengi wanaongoza ...