CHAKUHAWATA NI QNET ILIYOCHANGAMKA
CHAKUHAWATA NI QNET ILIYOCHANGAMKA. Na Thadei Ole Mushi. Juzi niliandika kuwa Chakuhawata ni mchongo wa wahuni wengine waliopo mjini, wakanipigia simu wakaniambia Koma kama kocha wa Simba Robentihno alivyokoma kumtoa Chama. Ninachojua mimi kumkata mwalimu maokoto ya 5,000 kila mwezi ni kumlagai Mwalimu tu ili aingie kwenye 18 na watu waanze kuokota maokoto na kutokomea kusikojulikana. Kwa vyovyote vile kama wanataka kuja kuwa chama cha kweli cha kutetea maslahi na haki za waalimu hawataweza kukiendesha chama hicho kwa shilingi 5,000 kwa kila mwalimu kukakatwa kila mwezi. Hesabu hazidanganyi. Kwa mujibu wa Takwimu zilizopo jumla ya walimu wote nchini Msingi na Sekondari wapo 258,291. Fuata link kupata taarifa za takwimu za walimu:- http://demo8.eganet.go.tz/tsc/statistics MAPATO YA CHAKUHAWATA. Chakuhawata wanakata 5,000 kwa kila mwalimu, tuseme sasa walimu wote wamejitoa wamejiunga nao hivyo ni 5,000 X 258,291 X 12 (Miezi) unapata jumla ya 15,497,460,000 (Bilioni 15.4) hapa...