KWA SHERIA MPYA YA TCRA KILIO CHETU

Kama ilivyoandikwa na maadimi wa blogs tanzania

Sheria mpya na gharama za usajili na tozo kwa shughuli za mitandaoni zinazohusiana na blogs, website, forums, YouTube, TV na radio imeleta majonzi kwa watanzania na wamiliki wa mitandao hiyo ambao kwa kiasi kikubwa ni vijana wa kipato cha chini waliojiajili kulingana na ugumu wa ajira nchini.
Kwaniaba ya watanzania na bloggers,
uongozi wa blog hii unaandika kwa kusema haya:-
Binafsi tupende kuchangia kidogo juu ya sheria mpya ya usajili na ulipiaji wa huduma ya online content kwa blogs, website, YouTube channels na huduma nyinginezo zihusuzo online content service.
Niwazi kuwa serikali yetu ya Tanzania kwa jicho la pekee imeona kuwepo kwa umuhimu wa kufanya jambo hili ikiwemo kudhibiti utoaji wa Taarifa za uongo, uchochezi na uvujishwaji Siri za serikali, uvunjifu wa amani ya nchi, utoaji wa maudhui machafu na yenye lengo la kuharibu utamaduni wa kitanzania n.k.
Nchini Tanzania mapinduzi ya kiteknolojia juu ya huduma ya utoaji wa habari mitandaoni umeanza miaka ya 2005-2007. Mapinduzi haya yaliwawezesha watanzania kupata habari kwa wakati, kupanua huduma za masoko ya biashara, huduma ya elimu bure kwa wanafunzi mitandaoni, huduma za kiroho kwa dini, huduma ya Taarifa za schoolarships kwa wanafunzi kusoma nje na ndani ya Tanzania, Taarifa juu ya fursa za utalii na serikali zilizopo nchini.
Licha ya kuwepo kwa Taarifa zisizokuwa na maudhui na ueredi mitandaoni, huduma hii husaidia mamilioni ya watanzania kupata habari kwa wakati na muda muafaka. *Mfano* : miaka ya nyuma serikali ilipo kua ikitoa matokea ya kidato cha nne necta ilikua ni tabu kupata matokeo hayo kwa wakati kwani ilikua inachukua mpaka siku zaidi ya saba mtu ajaona matokeo yake, hii ilitokana na
*1:Uwepo wa mitandao michache*(blogs,forums na websites):- hivyo ilipelekea kuwepo Taarifa chache mitandaoni, hivyo ilikua ni vigumu kupata Taarifa kwa wakati kipindi hivyo.
2:Traffic jam:- Kutokana na idadi kubwa ya watu online at once.Hivyo mapinduzi haya yalileta faraja kwa mamilioni ya watanzania walio wengi.
Ni jambo lisilofichika kuwa mamilion ya watanzania, serikali na makampuni Binafsi wamefaidi kwa kiasi kikubwa uwepo wa wingi wa mitandoo hii kwani umeifanya Tanzania kuwa kijiji na kuitangaza Tanzania nje ya nchi, hivyo imekua ni kituo cha taarifa za utarii na fursa zilizopo nchini.
*Kwa nini kufungiwa kwa mitandao na kuwepo kwa sheria hii!?*
Ikumbukwe Rais Xi Jinping wa China alipoulizwa kwanini kumekuwepo na wingu la kufungia mitandao alijibu "mitandao imeleta Shida kubwa katika utawala wa nchi, ulinzi pia na maswala yetu ya maendeleo" kwahiyo walifanya hivyo kwa sababu kuu 3:
1: Kutoa fursa kwa mitandao ya ndani
Hii ilikua moja ya sababu kuu nchini humo, licha ya kuwepo sheria kali, hakukuwepo tozo na ushuru kwa mitandao ya ndani ili kuruhusu ushindani wa bidhaa na technolojia ya ndani kwa ajili ya Kukuza kipato cha nchi. Ni kweli kwamba nchini China hakuna mitandao Kama YouTube, what's App, na facebook na badala yake wanatumia mitandao Kama Baidu kama google, wechat badala ya what's App Meipai badala ya instagram na youku Kama mbadala wa YouTube
2:Kulinda sera na maudhui ya nchi
Serikali ya China Iliona haina uwezo wa kuzuia uchangiaji juu ya masuala ya kisiasa na ukosoaji wa serikali na kuamua kufungia mitandao ya nje ya nchi ili kuweka self regulation kwa mitandao ya ndani.
3:Udhibiti wa maudhui yasiyo na maadili .
Hii ilikua ni kwa ajili ya kuisaidia serikali kuweka pin kwa site za nje ya nchi zenye maudhui yasiyoendana na utamaduni wao.
OMBI KWA TCRA NA SERIKALI
Ndugu waheshimiwa viongozi wetu wa TCRA na Serikali, nikiwa miongoni mwa watanzania na bloggers wenye mapenzi mema na Tanzania naomba mtusaidie mambo haya yafuatayo kwa faida ya maendeleo ya taifa Letu.
1: Kuondolewa kwa tozo juu ya usajili wa blogs, you tube channel, website n.k
Hii itasaidia ukuaji wa technolojia ya mawasiliano nchini na kuruhusu uwepo wa stock ya Taarifa, documents na files kwa ajili ya kizazi kijacho. Pia itasaidia maelfu ya watanzania kujiajiri kwani huduma hii Mara nyingi hutolewa na vijana ambao ni tegemezi kwa taifa na familia.
2:Kuwepo kwa system yenye uwezo wa kuchuja nakuondoa maudhui yasiyofaa
Hii Itakua mbadala wa kublock na kufilt contests zenye lengo la kuharibu amani ya nchi pamoja na utamaduni wa nchi.
3:Kutoa ruzuku kwa blogs, you tube channels, forums, (online content platforms )zisizo za kibiashara
Niwazi kuwa zipo online content zilizoanzishwa kwa malengo ya kutoa elimu na huduma Katika jamii na nyinginezo zikiwa ni za mashule, afya, pamoja na mashirika mbali mbali ya maendeleo Katika jamii hivyo wengi wao hawatakua na uwezo wa kumudu gharama hizo kwani huduma zao ni bure.
4:Kuanzishwa kwa ushindani wa technologia za mawasiliano za Tanzania
Hii itasaidia kupromote technolojia ya ndani na kukuza kipato cha nchi. Nyongeza ya hapa nikwamba database yake itakua rafiki na sera ya nchi pamoja na tamaduni zetu.
5:Kutoa leseni za utambuzi kwa blogger Kutoka TRA
Niombe serikali iwape kibali TRA kutoa vibali kwa waendeshaji wa mitandao yote nchini ili kuendesha shughuli nzima chini ya sheria husika za mamlaka hii. Katika kipengele cha makadirio ya malipo ya ushuru niwazi kuwa kuna site maalumu
Mtandaoni zenye uwezo wa kukadiria kipato na thamani ya online content platform yeyote, hivyo itawarahisishia TRA Katika utoaji wa leseni za uendeshaji wa huduma hiyo pamoja na utozaji wa kodi kwa maendeleo ya taifa Letu.
Mwisho: tumalizie kwa kusema msemo huu wa kiswahili "vita ya panzi ni furaha ya kunguru" nikiwa na maana kwamba serikali na taasisi husika inabidi viwe makini na wamiliki wa mitandao hii wenye kipato kikubwa kwani watataka kupewa kipaumbele ili kudhibiti ukuaji wa ushindani Katika technolojia mawasiliano na kuwaacha maelfu ya watanzania bila ajira pamoja na kuminya upatikanaji wa Taarifa kwa wakati. Vivyo hivyo inaweza kupelekea upenyaji wa makampuni makubwa kutoka nje ya nchi kuendesha hudumu hizi kwa gharama za juu kuliko ilivyokua awali kwa lengo la kurejesha fidia ya undeshaji mzima wa mitandao hiyo.
Nimatumaini yangu serikali yetu tukufu chini ya Rais John Pombe Magufuli itafanyia mabadiliko sheria hii mpya kwa kuondoa tozo hii na kuweka njia mbadala kunusuru na kudhibiti ukuaji wa tasnia ya technolojia mawasiliano na uhuru wa kupata habari kwa urahisi.

Nakupenda Tanzania
MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Comments

Post a Comment

Tafadhari usicomment matusi

Popular posts from this blog

RIWAYA YA KISWAHILI NA SIFA ZAKE

KI 311 SEMANTIKI NA PRAGMATIKI YA KISWAHILI

SEMANTIKI NA PRAGMATIKI