JEBII AMETUTOAKA SWAHIBA WETU WA DAMU
Msanii wa bongo fleva anayefahamika kwa jina la Jebby ambaye amewahi kufanya vyema na wimbo kama Swahiba amefariki dunia leo April 22, 2018 mjini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.
Watu wa karibu na msanii Jebby wamesema kuwa msanii huyo alikuwa anaumwa na mpaka umauti umemkuta Dodoma alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya bandama na ndiyo yaliyosababisha kifo chake.
Msanii Afande Sele pia amethibitisha hilo na kusema kuwa Jebby alikuwa anasumbuliwa na matatizo hayo ya bandama na kuwa leo ndiyo amefariki dunia.
"Hayupo tena duniani swahiba...pumzika kwa amani mdogo wangu wa haki Jebby.Tukimaliza kazi tutavalishwa taji"
Comments
Post a Comment
Tafadhari usicomment matusi