Mambo ya kuzingatia unapotaka kununua used car Tanzania
Baada ya kusikia watu wengi 'wakiumizwa' na 'kupigwa' wakiwa kwenye harakati za kutafuta usafiri uliotumika nchini, nimeona sio mbaya nikitoa ushauri ni jinsi gani unaweza kuepuka majanga kwenye zoezi hilo. Naandika kama m nunuzi au muuzaji wa aina hio ya magari, kwahio siegemei upande wowote na ninachokiandika hapa sio sheria naweza kuwa sahihi au nisiwe sahihi ila ni imani yangu lipo litakalosaidia baadhi ya watu. Njia muhimu za kufuata ili kupata gari unalotaka ni kama ifuatavyo: 1. Fanya utafiti mdogo juu ya gari unalolitaka : Uliza ujue gari unalolitaka linauzwa kiasi gani[makadirio]. Ukiweza kujua bei ya showroom au ukiagiza mwenyewe Japan halafu linganisha na bei utakayopewa hapa. Hili ni muhimu kwa sababu nimeshuhudia watu wanan unua magari yaliyotumika Tanzania kwa bei ambayo ukiagiza mwenyewe unalipata kutoka japan au ukiongeza kidogo tu unapata la showroom. 2 . Usiwe na haraka : Usiwe na haraka kabisa kwenye kutafuta gari. Utaletewa kila aina ...