Posts

Showing posts from January, 2021

USITESEKE NA MWEZI JANUARY NA ADA

 SIKIA;  Kama hauna hela ya kumpeleka mtoto wako shule za gharama (ada kubwa) ambazo inasemekana zinatoa elimu bora kuliko hizi zetu za Serikali, Basi mlete tu shule za serikali kisha fanya yafuatayo.    1- hakikisha umemnunulia uniform kuanzia 3 Ili awe msafi kila siku shuleni, usafi huleta kujiamini kwa mwanafunzi (maana hata hao wa kimataifa ukiwatazama physically usafi kwao namba 1). Mnunulie sox pea 5, mashati 3 sketi/bukta 2 Ili Kati Kati ya wiki ziwe zinafuliwa , hakikisha zinapigwa pasi na kama unaweza tupiamo hata dodorant ya Buku 5, unajua hizi shule za serikali unakuta watoto wachafu, kola nyeusi, uniform imechanika n.k Sasa ile inaua confidence ya mtoto ,kumbuka hata walimu wanapenda wanafunzi wasafi.   2- kiherehere smart hakikisha unakua karibu na walimu wake,haswa ikiwezekana uhakikishe anakaa dawati la mbele darasani, au ambapo mwl atamfikia au kumuona kirahisi, kuna faida ya kukaa dawati la mbele achana na back benchers tabia zao tunazikumbuka n...