HAYA NDIYO MABADILIKO UNAYOTAKIWA KUJUA
Usipobadilika, Dunia Itakubadilisha 1. Dunia ya Leo sio Dunia ya Kesho Tunaishi katika dunia mbayo huwezi kujua nini kitatokea kesho. Miaka michache iliyopita, hakuna aliyejua kwamba biashara ya Taxi itachukuliwa na UBER, BOLT, OLA CABS, LIM nk. Hakuna aliyejua kwamba leo hii mtu mwenye nyumba yake ya vyumba 3 atakuwa akigombania wateja "customers" dhidi ya mahoteli makubwa ya nyota 5 kama Hilton na Wyndham Worldwide kupitia Air BnB. Hakuna aliyejua kwamba NETLFIX itakuwa na nguvu kuliko vituo vya Tv na majumba ya sinema kama Century Cinemax. Na mbaya zaidi, hakuna aliyejua kwamba kazi nyingi zikiwemo za kitaalamu kama za wanasheria “lawyers”, madaktari “doctors”, marubani wa ndege “pilots” na waamuzi wa michezo mbalimbali ikiwemo soka “referees” zitachukuliwa na mashine au “robots”. Haya mabadiliko yapo kila sehemu kuanzia kwenye uchumi mpaka kwenye familia. Nani leo hii alijua kwamba itafika siku mwanamume na mwanamume wataruhusiwa kuwa mume na mke? “same sex marriage...