HAYA NDIYO MABADILIKO UNAYOTAKIWA KUJUA
Usipobadilika, Dunia Itakubadilisha
1. Dunia ya Leo sio Dunia ya Kesho
Tunaishi katika dunia mbayo huwezi kujua nini kitatokea kesho. Miaka michache iliyopita, hakuna aliyejua kwamba biashara ya Taxi itachukuliwa na UBER, BOLT, OLA CABS, LIM nk. Hakuna aliyejua kwamba leo hii mtu mwenye nyumba yake ya vyumba 3 atakuwa akigombania wateja "customers" dhidi ya mahoteli makubwa ya nyota 5 kama Hilton na Wyndham Worldwide kupitia Air BnB. Hakuna aliyejua kwamba NETLFIX itakuwa na nguvu kuliko vituo vya Tv na majumba ya sinema kama Century Cinemax. Na mbaya zaidi, hakuna aliyejua kwamba kazi nyingi zikiwemo za kitaalamu kama za wanasheria “lawyers”, madaktari “doctors”, marubani wa ndege “pilots” na waamuzi wa michezo mbalimbali ikiwemo soka “referees” zitachukuliwa na mashine au “robots”.
Haya mabadiliko yapo kila sehemu kuanzia kwenye uchumi mpaka kwenye familia. Nani leo hii alijua kwamba itafika siku mwanamume na mwanamume wataruhusiwa kuwa mume na mke? “same sex marriage”. Nani leo hii alijua kuwa mwanamke na mwanamke wataruhusiwa kuwa mume na mke? “same sex marriage”. Nani leo hii alijua kwamba ipo siku mwanamume atabadilisha mwili wake na viungo vyake na kuwa mwanamke? Na nani leo hii alijua kuwa itafika siku mwanamke atabadilisha mwili wake na viungo vyake kuwa mwanamume? Haya ni baadhi ya mabadiliko lakini bado mimi na wewe hatujui kesho dunia itaelekea wapi na nini kitatokea.
Wataalam wa sayansi wanasema inawezekana kabisa dunia itafika kipindi ambacho haitokuwa lazima mchele “rice” kulimwa shambani. Kwa sababu teknolojia itawezesha mchele kutengenezwa bila kupanda mbegu shambani. Kama hivi leo inawezekana kuotesha mazao kwenye maji pasipo kuwa na udongo “hydropronics, kwanini unafikiri hili la mchele haliwezekani? Kama inawezekana kupandikiza mbegu za kiume kwenye yai la mwanamke ili apate ujauzito na mtoto azaliwe “In vitro fertilisation” kwanini unafikiri hili haliwezekani? Ni dunia inayobadilika kwa kasi ya ajabu.
Wakati wa uhai wake, Henry Ford, Mwanzilishi wa Ford Motor Company ndiye aliyejulikana na kusifika kwa ugunduzi wake wa Model T na uzalishaji wa magari mengi “mass production” kwa kutumia mfumo wa “assembly line”. Lakini Henry Ford akifufuka leo hii atashangaa kwa sababu hakuna anayezungumzia tena magari. Watu wanazungumzia kwenda kuishi katika sayari ya mars na safari hizo kutumia “rockets” zinazotengenezwa na kijana mdogo Elon Musk na kampuni yake ya Space X. Na hata wakizungumzia magari, hawazungumzii magari ya kutumia mafuta ya asili yaani “petrol au diesel”. Wanazungumzia magari ya kutumia mfumo wa umeme “electric vehicles”. Ina maana hata wanaouza nishati ya mafuta asilia “fossil fuel” kichwa kinawauma kwa sababu dunia inahamia kwenye nishati mbadala au “renewable energy”.
Takwimu zinaonyesha kwamba mwaka 2016, nishati mbadala “renewable energy” ilikuwa ni 26.2% ya umeme uliozalishwa duniani. Na itategemewa kupanda mpaka 45% ifikapo mwaka 2040. Ukizungumza hii lugha mbele ya mtu anayefanya biashara ya mafuta anaweza akapata presha. Ukizungumza habari ya UBER kwa dereva Taxi anapata msongo wa mawazo “stress”. Na ukizungumza habari ya “robots” kufanya kazi ambazo mtu amesomea miaka 12 shuleni kama “neurologists” unaweza ukaonekana huna utu. Lakini ukweli ni kwamba huwezi kushindana na mabadiliko “change”. Makampuni kama KODAK na COMPAQ yalikufa kwa sababu ya kushindwa kukabiliana na mabadiliko. Ndio maana Stephen Hawking, mwanasayansi wa Uingereza anasema “Akili ni Uwezo wa Kukabiliana na Mabadiliko” [Intelligence is the Ability to Adapt to Change].
2. Kwanini maisha yanabadilika kwa kasi?
Dunia inabadilika kwa sababu maarifa yanaongezeka na taarifa zinakwenda kwa kasi zaidi. Hii ilitabiliwa toka mwaka 1975 na CEO wa Intel aitwaye Gordon Moore. Mwanasayansi huyu alisema uwezo wa teknolojia unakuwa marambili “double” kila baada ya miezi 18. Ndio sababu mambo ambayo wanayajua watoto wako leo hii, wewe uliyajua ukiwa chuo kikuu au ukiwa umekwishaanza kazi. Ina maana kizazi cha miaka ya 1944 mpaka 1964 “the baby boomers” si sawa na kizazi cha miaka ya 1965-1979 “generation x’ si sawa na kizazi cha miaka ya 1980-1994 “the millennials” na si sawa na kizazi cha miaka ya 1995-2015 “generation x”. Kwa sababu kila mtoto anayezaliwa baada ya mwaka mmoja na nusu anakuta teknolojia imekuwa mara mbili zaidi. Hii ni kulingana na “Moore’s Law”.
Ni rahisi kufikiria kuwa hii haikuhusu, inawahusu wanasayansi lakini kitu ambacho lazima ujue ni kwamba toka kuumbwa kwa ulimwengu maisha yote kuanzia chakula, ndoa mpaka kazi yamebadilishwa na teknolojia. Kihistoria, miji ilianza kukua baada ya kupanuka kwa kilimo kutokana na ugunduzi wa tairi au “wheel” katika maeneo ya MESAPOTAMIA “Iraq, Iran, Uturuki”. Hata biashara ya kuuza na kununua watu “utumwa” ilionekana haina maana baada ya Thomas Newcomen kugundua STEAM ENGINE mwaka 1712. Hii ndiyo iliyopelekea kutokea kwa mapinduzi ya viwanda Uingereza “Industrial Revolution”. Ugunduzi wa “electromagnetic force” wa akina Thomas Edison, Michael Faraday na James Clerk ndio uliopelekea kushamiri kwa vifaa vya umeme kama X-Ray na TV. Quantum theory ya Albert Einstein ndiyo iliyopelekea kugunduliwa kwa mtandao “worldwideweb” au internet, kazi iliyofanywa na Tim Berners-Lee mwaka 1989. Ina maana huo ni mfululizo wa mapinduzi ya viwanda ya kwanza, pili na tatu. Leo dunia inazungumzia mapinduzi ya 4 ya viwanda. Ambapo fedha ya kwenye mitandao “digital currency” au “cryptocurrency” inataka kuchukua nafasi ya mabenki kupitia teknolojia ya “blockchain”. Teknolojia ambayo itapelekea wewe na mimi kutohitaji “passport” kusafiri wala nchi za dunia kuhitaji Tume za uchaguzi wakati wa kupiga kura. Ina maana teknolojia inaondoa kazi za taasisi kama mabenki na nyinginezo.
Nilipokuwa nikitafakari mabadiliko haya, nikagundua kuwa hakuna namna ya kuyazuia zaidi ya kujipanga kukabiliana nayo. Kwa sababu mabadiliko haya yameingia mpaka kwenye ndoa, kwenye malezi na maisha mengine ya sisi binadamu. Mfano ukiangalia ndoa za wazazi wetu, kizazi cha miaka ya 1944 mpaka 1964 “the baby boomers” ni tofauti sana na ndoa za kizazi cha miaka ya 1980-1994 “the millennials”. Siku hizi ni kawaida kwenda kwenye harusi leo kusherehekea halafu kesho kusikia wanandoa wameachana wakiwa “honey moon” baada ya meseji “mbaya” kuingia usiku wa manane. Nini kimepelekea? Taarifa kusambaa kwa kasi kupitia teknolojia hasa simu za mkononi. Leo hii ni rahisi ndoa kuvunjika kwa sababu hauhitaji kutumia mwaka mmoja au miaka 3 kumchumbia mtu. Mnakubaliana “Facebook” au “Instagram” halafu mnatumia M-PESA na TIGO-PESA kuchangisha fedha za send-off na harusi halafu mnakutana ana kwa ana siku ya harusi. Ndiyo sababu takwimu za dunia zinaonyesha kwamba zaidi ya 60% ya ndoa zinaishia kuvunjika “divorce”
Hoja yangu si kueleza ubaya wa mabadiliko ya teknolojia lakini kuweka mkazo katika namna ya kukabiliana na mabadiliko ambayo mengi yanaletwa na teknolojia. Kwa sababu kuwa na simu au teknolojia fulani ni jambo zuri. Leo hii hauhitaji kwenda ofisini ukiwa na simu. Simu ndiyo ofisi yako. Unaweza ukaamshwa asubuhi na simu “alam”, ukasoma magazeti kwenye simu “M-Paper”, ukafanya mazoezi kupitia simu, ukaandika na kutuma email kupitia simu, ukafanya kikao Uingereza kupitia simu, ukatoa hela benki kupitia simu, ukalipa mishahara kupitia simu nk. Na hata ikifika jioni unaweza ukaangalia soka kupitia simu, ukaangalia taarifa ya habari kupitia simu, ukaangalia sinema kupitia simu, ukaagiza chakula kupitia simu, ukajua hali ya hewa ya kesho kupitia simu nk. Siku yako inaweza ikaanza na kuisha katika simu. Kwa mantiki hiyo, swali la msingi ambalo mimi na wewe lazima tujiulize ni hili? Kwa sababu hatuwezi kukabiliana na haya mabadiliko, tunawezaje kubadilika ili tuende sambamba na haya mabadiliko? Ili tusipoteze kazi zetu, ili tusiue ndoa zetu, ili tusiue biashara zetu, ili tusipitwe na kasi ya dunia?
3. Usipobadilika, mabadiliko yatakubadilisha
Mwanadamu ameumbwa kukabiliana na mabadiliko kwa yeye mwenyewe kubadilika. Toka ulipokuwa tumboni mwa mama yako ulikuwa unakabiliana na mabadiliko. Uwezo huo ni sehemu ya DNA yako. Hebu fikiria namna mama yako alivyobadilika ukiwa tumboni. Ulipotungwa mimba tu, nayeye akapata ujauzito, ghafla akaanza kutapika, akaanza kutokwa na chunusi, akaanza kupata kichefuchefu, akaanza kupata hasira, akaanza kuchagua vyakula nk. Hayo ni mabadiliko ambayo ulikabiliana nayo ukiwa tumboni. Lakini haikuishia hapo, ulipozaliwa ukaendelea kukabiliana na mabadiliko tena kwa taabu. Kwa kujaribu na kushindwa mpaka ukaweza. Pengine hukumbuki lakini hebu fikiria mtoto anapotaka kuanza kutembea. Kwanza anatambaa kisha anajaribu kusimama na kuanguka. Anafanya hivyo mpaka anaweza. Ulipofikisha umri wa kupevuka kama wewe ni binti ghafla unaanza kubadilika umbo na mzunguko wa hedhi unaanza “menstruation circle”. Kama ni kijana wa kiume sauti inabadilika na misuli inaanza kutokea. Yote hayo ni mabadiliko. Ina maana uwezo wa kubadilika kulingana na mabadiliko ya maisha upo ndani yako.
Ukijaribu kukumbuka mabadiliko uliyokwisha kupambana nayo mpaka sasa huwezi kushindwa kukabiliana na mabadiliko yanayotokea kazini kama ambavyo kazi nyingi hata za kitaalamu kama wanasheria, madaktari, marubani wa ndege, waamuzi wa michezo mbalimbali ikiwemo soka zinavyochukuliwa na mashine au “robots”. Huwezi kushindwa kukabiliana na mabadiliko yaliyofanya kampuni kama KODAK na COMPAQ ziondoke sokoni. Na huwezi kuruhusu WhatsApp, facebook na Instagram ivunje ndoa yako. Lakini hii siyo rahisi kama unavyofikiria. Inahitaji kuwa na mfumo utakaokuwezesha kukabiliana na mabadiliko. Ndio maana hata mwili wa binadamu una mfumo unaokabiliana na mabadiliko ya mwili. Mfumo huu unaitwa “immune system”. Lakini hili si jina la mfumo naotaka kuueleza hapa, huu ni mfumo wa mwili, mfumo naotaka kuueleza hapa unaitwa Agile unaofanya kazi za mfumo wa mwili au “immune system”.
4. Mfumo wa Agile
Kama umeoa au umeolewa utakuwa ulipitia kipindi kinaitwa Uchumba. Kama umeajiriwa utakuwa ulipitia kipindi kinaitwa “Probation”. Na kama umewahi kufanya utafiti, utakuwa ulianza na kipindi kinaitwa “Pilot”. Uchumba ni wakati wa kufahamiana. Ni wakati wa kumjua huyo anayeenda kuwa mume au mke wako. “Probabtion” ni wakati wa kuangalia uwezo wako wa kutimiza majukumu kazini. Mara nyingi ni miezi 3 au 6. Baada ya hapo unapata au unakosa kazi. “Pilot” ni wakati wa kutekeleza mradi au kufanya utafiti wako kwa wigo mdogo au watu wachache ili kuona kama matokeo yanaridhisha kupanua wigo wa mradi. Kipindi cha yote haya (uchumba, probabtion na pilot) ndio kipindi cha kujenga matarajio “expectations”. Ni kipindi muhimu ambacho ukikosea kinakutesa ukiwa kwenye ndoa au kazini au kwenye utekelezaji wa mradi au utafiti wako “research”.
Wataalam wa masuala ya ndoa kwa mfano wanasema ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu ya mabadiliko ndani ya ndoa. Nakumbuka binti mmoja alimkimbia mume wake kwa sababu wakati wakiwa katika uchumba alikuwa akifuatwa kwa gari, akipelekwa katika nyumba ya ghorofa 3, akipelekwa hotelini nk. Lakini baada ya kuingia kwenye ndoa akagundua kuna mabadiliko. Yule bwana hakuwa na gari alikuwa akiazima kwa rafiki yake, hakuwa na nyumba, ilikuwa ya bosi wake na hakuwa na hela ya kumpeleka tena hoteli alikuwa amekusanya pesa za kumburudisha mchumba wake wakati wa uchumba na ilimchukua miaka 3 kufanya hivyo. Lakini mabadiliko yakavunja ndoa yake. Huo ni mfano mmoja wa ndoa lakini iko mingi. Sasa suala sio kuwa na mifano, jambo la msingi mabadiliko haya yakiwemo ya ndoa, kazi na teknolojia tunayakabili vipi?
Hapo ndipo mfumo wa Agile unapokuja. Katika dunia ya leo, makampuni mengi ikiwa ni pamoja na makampuni ya teknolojia kama Google, Netflix, Apple na mengineyo yameamua kutumia mfumo ambao utawafanya wakabiliane na dunia ambayo hujui kesho litatokea lipi. Zamani, makampuni mengi yalikuwa yanaweka mipango ya miaka 5, 10 au 100 mbele kwa kutumia mfumo ulioitwa “waterfall”. Kupitia mfumo huu, makampuni mengi yalikuwa yana muundo wa “pyramid” au pembe tatu katika uongozi. Makampuni mengi yalikuwa yanatengeneza huduma au bidhaa na kuipeleka sokoni kwa mteja pasipo kumshirikisha katika mchakato wa kutengeneza hiyo huduma au bidhaa.
Leo si hivyo tena, kwa sababu yamegundua unaweza ukaweka mpango wa muda mrefu wa kutengeneza simu ya laini 10 na wakati unafanyia kazi mpango huo, baada ya wiki moja mshindani wako anakuja na teknolojia ambayo haitumii line. Au unatumia pesa na nguvu nyingi kutengeneza software lakini unapokamilisha na kupeleka kwa mteja, anakuambia hapana umekosea, mimi situkata iwe hivyo. Kutokana na hayo, wataalam wa sayansi walikaa na kuzindua mfumo mpya unaoitwa Agile. Mfumo ambao hautumiki tu katika biashara lakini hata katika maisha ya kawaida kama vile malezi, ndoa nk. Mfumo ambao msingi wake mkubwa ni kuwa tayari kubadilika “adaptive” kushirikiana “collaborative” kumsikiliza mteja “customer centric” na kukubali kujifunza kutokana na makosa “learning from failure”.
Ndio maana leo hii ukitaka kutengenezewa “software” mfano Mobile App au Payment System utatengenezewa kwa hatua au “phases”. Na katika kila hatua utaulizwa kama kila kitu kinaenda sawa. Hakuna kampuni ya software itakutengenezea kitu mpaka mwisho halafu useme sio hivyo. Ndio maana leo hii makampuni mengi hayakulazimishi ufanye kazi ofisini. Unaweza ukawa nyumbani, au umesafiri “remote location” na bado ukawa ofisini kwa sababu ya mifumo shirikishi ya kufanya kazi. Ndio maana leo hii unaweza ukashangaa kampuni kama SONY inatengeneza Tv, majiko, vifaa vya umeme na wakati huohuo inatengeneza sinema na muziki. Au unaweza ukashangaa Bill Gates ambaye anajulikana katika eneo la “software” ndani ya Microsoft, amewekeza kwenye nishati mbadala “renewable energy”. Ndio maana ya utamaduni wa Agile. Kubadilikia kulingana na mazingira. Ni kama mdudu aitwaye mende “cockroach”. Mende wana uwezo wa kuishi mahali popote. Wanaweza kuishi jikoni, bafuni, chumbani hata chooni. Wako tayari kukabiliana na mabadiliko. Hivyo ukisema mende wako “Agile”, hujakosea, uko sahihi kabisa.
Mwanzoni niliandika juu ya binti mmoja mbaye alimuacha mume wake baada ya kugundua kuwa kila kitu alichomuona nacho wakati wa uchumba kuanzia nyumba mpaka gari havikuwa vyake. Huyu dada hakuweza kukabiliana na mabadiliko. Hakuwa “adaptive” na mazingira mapya. Ina maana hakuwa Agile. Ukweli utabaki palepale kwamba si jambo zuri kuishi maisha mbayo si yako kama alivyofanya yule kijana. Lakini katika maisha vitu vingi viko nje ya uwezo wetu. Je vinapotokea tunafanyeje? Tukimbie? Unapofukuzwa kazi ni jambo ambalo lipo nje ya uwezo wako, ufanyaje? Ujiue? Hapana! Kuwa Agile. Kumbuka nilisema hapo awali kwamba uliumbwa kukabiliana na mabadiliko toka ukiwa mtoto mdogo. Na kwa kutambua hilo, wanasayansi nao wakaja na mfumo wa kukabilaina na mabadiliko. Mfumo wa Agile ambao unaweza ukatumika katika maeneo yote ya maisha. Ni vitu gani vinavyoainishwa katika utamaduni wa Agile?
a) Pata muda wa kupata mrejesho “feedback”
Wale wanaotengeneza “software” wanamfanya mteja kuwa ni “product owner”. Wanaotengeneza “software” wana msimamizi wao anayeitwa “scrum master”. Mume wako au mke wako ni “mteja wako”. Kama “scrum master” anavyomuuliza “product owner” au mteja kama anatakiwa kufanya mabadiliko katika bidhaa “product” au huduma “service” anayotoa kwa hatua walizokubaliana au “phases”, na wewe pia unatoa huduma kwa mkeo au mumeo. Umeshawahi kumuuliza “mke wangu au mume wangu umeonaje huduma yangu wiki hii”? Usicheke, dunia imebadilika sana na wewe lazima ubadilike.
Hata ukiwa mjasiriamali au mfanyabiashara au kiongozi wa kampuni ni lazima upate mrejesho au “feedback” kutoka sokoni. Hujajiuliza kwanini Cocacola walianza kuuza maji ya kunywa na kutengeneza soda zisizo na sukari? Ulishawahi kujiuliza kwanini Pepsi walianza kutengeneza soda zisizo na sukari? Ulishawahi kujiuliza kwanini Colgate ilianza kutengeneza dawa ya meno wakati biashara yake ya kwanza ilikuwa ni kutengeneza sabuni? Kwa sababu mpango wao wa awali ulikuwa ni huo lakini walipoingia sokoni wakakuta uhitaji wa “sabuni” hauwatoshi wao kuendelea kuwepo sokoni wakabadilika na kuanza kutengeneza dawa ya meno. Ndivyo ilivyokuwa kwa Cocacola na Pepsi. Dunia imebadilika na watu wanajali afya zao. Watu wako makini na vinywaji vya sukari. Kampuni hizi za vinywaji zisingebadilika inawezekana biashara zao zingebadilika. Wangefunga makampuni. Lakini wakaamua kubadiilika. Wamekuwa “Agile”.
b) Shirikiana na wenzako
Wenzako ni neno pana lakini linaingia hata katika ngazi ya familia au kazini. Familia ambazo ni “Agile” mke na mume wanashirikiana. Familia ambazo zinashirikiana zinafanikiwa sana. Jamii ambazo zina utamaduni wa kushirikiana zinafanikiwa sana. Mfano jamii nyingi sana za kitanzania zinashirikiana sana katika ndoa na misiba. Ni ngumu sana kushindwa kuoa au kuolewa na ni ngumu sana kushindwa kufanikisha msiba ukiwa Tanzania. Katika hilo tumefanikiwa. Ni tofauti na jamii za kimagharibi. Ukiwa Ulaya au Marekani ni ngumu sana kutegemea michango kufanya harusi au msiba. Lakini ni rahisi sana kutegemea wenzako katika kupata mtaji “capital” na kufanya biashara “partnerships”. Hii inakupa picha kuwa iwe ni harusi au biashara ushirikiano unafanya mambo yatokee. Ndio maana waanzilishi wa Agile waliweka hili katika ilani au “Agile Manifesto”. Hivyo unapotumia “software” fulani katika simu yako jua kwamba haijatengenezwa na mtu mmoja. Ni watu wengi waliogawanya kazi na kila mmoja kupewa jukumu la kutekeleza kwa muda fulani kwa lugha ya kitaalam wanaita “sprint” Ndio maana “Artificial Intelligence” imewezekana. Kwa sababu sio akili ya mtu mmoja, ni akili ya mtu zaidi ya mmoja.
Ukiweka akili yako na ya mke wako au mume wako hamuwezi kushindwa jambo, ukichanganya akili ya meneja masoko na meneja utawala na meneja wa fedha hapo ofisini hamuwezi kushindwa kitu. Ukichanganya akili yako na ya rafiki zako hapo chuoni hamuwezi kushindwa kitu. Kitu kinachofanywa na watu wengi hakiwezi kulingana na kitu cha mtu mmoja. Ndio maana biashara kubwa duniani ni za kifamilia. Ukiongelea watu wenye biashara kubwa kuliko zote duniani, unaongelea familia ya Rothschild. Lengo sio kushindana nani ana uwezo kuliko wote katika familia, lengo ni kutumia kila kipaji na uwezo wa wanafamilia kufanya mambo makubwa. Hiyo ni katika ngazi ya familia, lakini hata ukiwa kazini, ukitaka wewe ndiye upate sifa “credits” wakati wote, hauwezi kufanikiwa kwa sababu kuna kitu ambacho wewe huna ambacho mwenzako anacho. Huo ni utamaduni wa Agile.
c) Uwe na hamu ya mafanikio
Ungeniuliza niseme kwa kiingereza namaanisha nini kusema hamu ya mafanikio ningesema “ambition”. Ingawa “mafanikio” usiyafunge kwenye fedha na vyeo, ni zaidi ya hapo. Unaweza usiwe na hela nyingi au cheo kikubwa na bado ukawa umefanikiwa. Ukiangalia historia ya ubunifu “creativity and Innovation”, utagundua kuwa watu wengi waliogundua vitu vikubwa katika dunia walikuwa na hamu ya mafanikio “strong desire to succeed”. Mafanikio madogo au makubwa yanataka “hamu ya mafanikio”. Sikuwa na mpango wa kuandika hii makala leo. Lakini nimepata nguvu ya kuandika ndani ya saa moja kwa sababu ya kuwa na “hamu ya kubadilisha mtazamo wa wengi juu ya mabadiliko”. Nina hamu ya kufanikisha hili lengo. Mfumo wa Agile unahitaji watu wenye hamu ya mafanikio.
Zamani ilikuwa ngumu kwa mtu kufanya biashara na kampuni. Ilikuwa ni rahisi kwa mtu kuajiriwa na kampuni. Na ilikuwa rahisi kwa kampuni kwa kampuni kufanya biashara. Siku hizi mambo yamebadilika, mtu anaweza akawa taasisi pasipo hata ya kuwa na kampuni na akafanya bishara na kampuni. Kwa kiingereza “A person can be an institiution”. Hebu fikiria mtu kama Larry King aliyekuwa akiendesha kipindi cha Larry King Live cha CNN. Unawezaje kumuajiri Larry King? Watu kama Larry King walikuwa ni taasisi na walifanya biashara na taasisi. Lakini Larry King hakuwa taasisi kibahati. Alifanya kazi nzito kwa weredi na umakini kufika alipofika. Alikuwa mweredi na alielewa fani yake “mastery” kiasi kwamba watu walimfuata, walimtaja au walimnukuu yalipokuja masuala yanayohusu tasnia ya habari. Hicho ndicho kilichomfanya Larry King akawa taasisi.
Pamoja na kwamba Agile inahamasisha ushirikiano lakini ili wenzako wakubali kushirikiana na wewe lazima uwe unajua na uko vizuri katika eneo lako “mastery”. Lazima uwe na mamlaka katika taaluma au kazi yako “authority”. Lazima uwe “Scrum Master”. Hata makampuni makubwa kama Google na Facebook wanapokuwa wanataka kutengeneza “software” ya mabilioni ya fedha, wanatengeneza “scrum teams” za watu ambao wana weredi “mastery” katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na “developers”, “testers” nk. Hata kocha wa timu anapofanya usajiri wa kikosi kipya anaangalia wachezaji wenye weredi “mastery” katika maeneo mbalimbali kama ulinzi, viungo, wachezaji wa pembeni na wafungaji.
Ina maana ushirikiano unaoongelewa katika Agile sio wa watu ambao hawajitambui. Ni ushirikiano wa watu waliosheheni ujuzi na weredi katika maeneo yao ya kujidai. Ni kwa sababu tunaishi kwenye dunia ambayo huwezi kushirikishwa kama huna cha kuchangia. Kama ni rafiki utapata wa kufanana naye. Kama ni mshirika utapata mwenye maono kama yako. Ndio maana Bill Gates na Aliko Dangote ni marafiki. Jiulize, wametoka bara moja? Hapana! Wako katika fani moja? Hapana! Huyu anatengeneza “software’ huyu anatengeneza “cement”. Sasa urafiki wao unatoka wapi? Ni kwa sababu wana mtazamo mmoja! Ina maana mnaweza mkawa kampuni moja lakini mkashindwa kushirikiana kwa sababu mnatofautiana mtazamo. Wakati wewe una mtazamo wa kupata weredi na kufanya mambo yatokee, mwenzako ana mtazamo wa kukupiga majungu na fitina ili wewe ushuke yeye apande “office politics”.
Dunia imebadilika na itaendelea kubadilika lakini binadamu tumepewa akili ya kukabiliana na mabadiliko hayo. Ukweli wa mabadiliko ni kwamba uyapende au usiyapende yapo. Unachoweza kufanya ni kukabiliana nayo. Makala hii imeandikwa na Paul R.K Mashauri. Hairuhusiwi kuchapisha au kutumia sehemu ya makala hii pasipo ruhusa ya mwandishi. Haki zote zimehifadhiwa@ 2019. Kwa maelezo zaidi andika barua pepe kwenda kwa ceo@masterclassworldwide.co.tz.

Comments
Post a Comment
Tafadhari usicomment matusi