Posts
Showing posts from May, 2017
RIWAYA YA KISWAHILI NA SIFA ZAKE
- Get link
- X
- Other Apps
RIWAYA YA KISWAHILI NUKUU ZA SOMO: MAANA YA RIWAYA NA AINA ZA RIWAYA: Riwaya imefasiliwa na wataalamu mbalimbali miongoni mwao nikama vile, Encyclopedia Americana (EA), Jz. 20 (1982:510f) wakinukuliwa naMulokozi (1996) wanasema, riwaya kuwa ni hadithi ya kubuni inayotosha kuwa kitabu. Udhaifu; Maelezo haya yanaibua utata kwani hayafafanui kitabu kinapaswa kuwa na urefu kiasi gani. Matharani kwa mujibu wa UNESCO katika Mulokozi (1996) kitabu ni chapisho lolote lenye kurasa 48 au zaidi. Ama urefu wa kitabu hautegemei idadi ya kurasa tu pia unategemea ukubwa wa kurasa (upana na kina) ukubwa wa maandishi na mpangilio wake. Encyclopedia Britanica EB, Jz.8, (1985:810) wakinukuliwa naMulokozi (1996) wanaeleza kuwa, riwaya ni masimulizi marefu yakinathari yaliyochangamana kiasi, yenye kuzungumzia tajriba ...