Posts

Showing posts from April, 2023

KAIKA KUELEKEA MEI MOSI 2023 KILIO CHA WALIMU KIPO HAPA

WARAKA KWA SERIKALI KUHUSU WAALIMU, SERIKALI IWAJALI WALIMU Ni muda sasa umepita kukiwa na manung'uniko kwa walimu katika nyanja nyingi zinazohusu maslahi yao ikiwemo mishahara yao, stahiki zao na kunyima haki na kuonewa na kuchukuliwa kama watu wa shida na kila kiongozi. Kuna haja serikali kumwangalia mwalimu kwa jicho la tatu, walimu wanapitia wakati mgumu sana katika utendaji kazi wao. Nimejaribu kuorodhesha changamoto hizi ambazo kama serikali ikizitatua hasa katika bajeti ijayo, ili mwalimu naye aone faraja ya maisha Baadhi ya changamoto hizo ni; MISHAHARA Serikali ipitie a iboreshe kwa mapana mishahara ya walimu, suala hili limekuwa tatizo kwa muda mrefu ikiwa kuna manung'uniko makubwa juu ya mishahara kiduchu wanayopewa waalimu Mara kwa mara tumekuwa tukisikia "mama anaupiga mwingu" kwenye Elimu, lakini ukichunguza kwa kina na kwa mapana na hata ukiwasikiliza wanaosema hivyo wanaishi kutaja vyumba vya madarasa na mabweni au katika miundombinu tu, huwezi ...