FANYA HIVI UKIIBIWA SIMU YAKO
Mambo matano unayotakiwa kufanya iwapo simu yako ya mkononi imeibiwa 20 Aprili 2022 simu CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Mtu yeyote yule anaweza kuibiwa simu Tunaburudika tukiwa mbali na nyumbani, tunapuuzilia mbali kutumia simu ya rununu kwa muda na tunapoangalia mfukoni, begi au mahali tulipoiweka, haipo tena. Wezi wanaweza kuwa na ujuzi mkubwa wa kuiba simu za mkononi kwa kipindi kifupi tu. Mbali na kutufanya tujisikie vibaya, wizi wa simu za mkononi unaweza kuathiri hati na data ya kibinafsi na kusababisha athari katika akiba zetu Zifuatazo ni hatua tano unazotakiwa kuchukua iwapo simu yako imeibwa. 1. Ifunge simu yako Iwapo simu yako ya mkononi itaibiwa, hatua ya kwanza ni kuzuia kifaa hicho mara baada ya kupotea, kwa mujibu wa Emilio Simoni, mtaalamu wa usalama wa kidijitali na mkurugenzi wa dfndr Lab, wa kikundi cha CyberLabs-PSafe. "Ni muhimu sana kuwasiliana na kampuni ya simu unayotumia na kuwaomba waifungie kwa muda na kuifanya simu isiweze kutumi...