Posts

Showing posts from October, 2018

TANZU ZA USHAIRI WA KISWAHILI

Ushairi wa Kiswahili waweza kuainishwa katika tanzu au kumbo mbalimbali. Mulokozi (1996), ameuainisha ushairi wa kimapokeao katika kumbo kuu tatu za kimtindo. Kumbo hizo ni: ushairi wa kijadi au kimapokeo; ushairi wa mlegezo; na ushairi wa maigizo. 1. Ushairi wa Kimapokeo Haya ni mashairi ya kijadi yenye kufuata kanuni za urari wa mizani na mpangilio wa vina vya mwisho na/au vya kati. Mfano wa shairi la kimapokeo ni huu hapa: Namshukuru Namshukuru Illahi, Mwenyezi mkamilifu, Kwa kuishi nikawahi, kazini kustaafu, Bado ningali sahihi, imara na mkunjufu, Alihamdulilahi, namshukuru Latifu. Ulimwengu wa rakadha, umejaa hitilafu, Sikuweza mambo kadha: karibu mambo elfu; Kanipa hii karadha, Bwana Mungu namsifu, Alihamdulilahi, namshukuru Latifu. Hii sikutazamia, kwamba litanisadifu, Bahati imenijia, kwa kupenda Mtukufu, Mfano kama ruia, Mungu hana upungufu, Alihamdulilahi, namshukuru Latifu. (Shaaban Robert, 2003: 102 – 104) 2. Ushairi wa Mlegezo Haya ni mashairi...
*πŸ’₯πŸ’₯HESLB: MAJINA YA WANAFUNZI AMBAO WALIKOSEA KUJAZA FOMU ZA MIKOPO/ FOMU ZAO ZINA MAPUNGUFU* πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½ πŸ—£ *BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU IMETANGAZA MAJINA 25000 YA WANAFUNZI WALIOKOSEA KUAJAZA FOMU ZA MIKOPO YA ELIMU YA JUU 2018/19* *πŸ—£WANAFUNZI WOTE WANATAKIWA KUFANYA MAREKEBISHO KUANZIA J3 MPAKA JUMAPILI IJAYO 30 SEPTEMBER* *MAJINA YOTE YANAPATIKANA HAPA ...PAKUA PDF* πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½ https://udahiliportal.com/2018/09/heslb-public-notice-to-all-loan-applicants-2018-19-academic-year/ *TAFADHALI SAIDIA KUSHEA TAARIFA HII MUHIMU KWA WANAFUNZI WOTE WALIAPPLY MIKOPO YA ELIMU YA JUU MWAKA HUU*