HIZI NI FAIDA ZA POMBE MWILINI
pombe ni nini? pombe ni neno ambalo linajumuisha aina zote za vilevi unazozifahamu, pombe za aina mbalimbali zinatengenezwa na kutumika na jamii zote duniani japokua kuna baadhi ya dini haziruhusu pombe. historia ya pombe inaonekana kwanzia zamani sana, kibiblia hata kabla ya kuzaliwa kwa yesu. sasa pombe ina hasara nyingi ambazo kila mtu anazifahamu ikinywea kwa kiasi kikubwa lakini kuna faida zake muhimu iwapo zikinywewa kwa kiasi kinachotakiwa. kiwango sahihi cha pombe ni kipi kiafya? kitaalamu mwanaume mmoja anatakiwa anywe vinywaji viwili vya pombe wakati mwanamke anatakiwa anywe kinywaji kimoja cha pombe. sasa tunaposema kinywaji hatumaanishi chupa pombe ila tunamaanisha kiasi cha pombe na asilimia zake ndani. kinywaji kimoja ni tunachozungumzia ni kama ifuatavyo... milimita 354 za bia ya kawaida yenye 5% ndio kinywaji kimoja. milimita 147 za wine au mvinyo yenye 12% ndio kinywaji kimoja. milimita 44 za pombe kali kama viroba zenye 40% ndio kinywaji kimoja. mfano hai tu...