WASIKILIZE MASHABIKI WA DIAMOND WALICHOSEMA
Naomba nikiri kwamba me ni shabiki namba moja wa Diamond,Lakini dah! kiukweli kwa ule ukimya wa mda mref kutoka kwa diamond nilitegemea akirudi safari hii hatakua level zile tulizomzoea za kufanya kolabo na wasanii wa nigeria, Nilitegemea huu upepo walionao kina Davido ama Wizkid ungemuamsha na kwenda level za mbali zaidi lakini badala yake ameniangusha na amerudi kule kule nigeria, Dah! Yani ile juzi niliposkia Kua kesho yake diamond ataachia hit nikajua kama sio feature Alicia Keys basi itakua ni French Montana ili kuzima ule upepo wa wakina davido na wizkid maana kusema ukweli kwasasa wanigeria wanazidi kuongeza gape kati yao na sisi tofauti na kipindi cha nyuma kidogo. anyway,yote kwa yote nimpongeze kwa hit nzuri aliyoiachia japo haijakuna mtima wangu haswa lakini nashkuru kwa Kuliamsha Dude maana na najua wasanii wengine nao watafuata kuachia hit kwakua kaka mkuu kashaliamsha DUDE.