Machapisho

Mambo ya kuzingatia unapotaka kununua used car Tanzania

Baada   ya kusikia watu wengi 'wakiumizwa' na 'kupigwa' wakiwa kwenye harakati za kutafuta usafiri uliotumika nchini, nimeona sio mbaya nikitoa ushauri ni jinsi gani unaweza kuepuka majanga kwenye zoezi hilo. Naandika kama m nunuzi au muuzaji wa aina hio ya magari, kwahio siegemei upande wowote na ninachokiandika hapa sio sheria naweza kuwa sahihi au nisiwe sahihi ila ni imani yangu lipo litakalosaidia baadhi ya watu. Njia muhimu za kufuata ili kupata gari unalotaka ni kama ifuatavyo: 1.  Fanya utafiti mdogo juu ya gari unalolitaka : Uliza ujue gari unalolitaka linauzwa kiasi  gani[makadirio]. Ukiweza kujua bei ya showroom au ukiagiza mwenyewe Japan halafu linganisha na bei utakayopewa hapa. Hili ni muhimu kwa sababu nimeshuhudia watu wanan unua magari yaliyotumika Tanzania kwa bei ambayo ukiagiza mwenyewe unalipata kutoka japan au ukiongeza kidogo tu unapata la showroom. 2 . Usiwe na haraka : Usiwe  na haraka kabisa kwenye kutafuta gari. Utaletewa kila aina ...

JANGUAR HUYOOO AULA UBUNGE KENYA

Picha
Msanii Charles Njagua maarufu kama Jaguar ambaye ameshinda kiti cha ubunge katika jimbo la Starehe nchini Kenya kufuatia uchaguzi mkuu ambao bado unaendelea, amewarudia wananchi na kuwashukuru. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jaguar ameandika maneno akisema kuwa bila wao asingefanikisha hilo, huku akiwashukuru wapinzani wake kwa kukubali ushindi wake huo. "Hakuna linalowezekana bila Mungu, Nawashukuru watu wa Starehe kwa ujasiiri na kuniamini kuwawakilisha bungeni, nawashukuru wote walioniunga mkono , marafiki, familia ambao walikuwa nami wakati wa kampeni. Na Pia nampongeza mpinzani wangu Steve Mbogo, Boniface Mwangi na Mh. Kwenya ambao waliweka kampeni safi. Huu sio ushindi wa Starehe tu bali ni ushindi wa vijana wote nchini Kenya ambao wameona mbele, sasa tuijenge Starehe ile tunayoitaka, Mungu awabariki", aliandika Jaguar. Jaguar ameibuka mshindi wa Jimbo hilo kwa asilimia 53% ya kura zote, huku akifuatiwa na Steve Ndwiga  aliyepata asilimia 31% na Boniface Mwan...

NIMEKUSOGEZEA MAGAZETI YA LEO TAREHE 10.08 YASIKUPITE

Picha

KAMA UPO KWENYE MAHUSIANO NA MWANAMKE MIAKA MIWILI NA HUJAWAHI KUONA CHOZI LAKE HUYO HANA MAPENZI YA KWELI

Picha
Leo nimeona nilete hili jambo, katika ujana wangu nimebahatika na kuwa na mahusiano ya kimapenzi na zaidi ya msichana mmoja ila kitu nilicho gundua hata wewe jalibu kufanya utafiti kama upo kwenye mapenzi na mwanamke zaidi ya miaka miwili na hujabahatika walau siku moja kuona machozi yake basi tambua huyo mwanamke hana mapenzi ya dhati kwako chamsingi nikuchukua tahadhari mapema OVA.

MOTO WAANZA KULINDIMA UCHAGUZI TFF

*Kampeni TFF zaanza kwa kishindo* Kampeni  za  uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) zimefunguliwa rasmi leo Jumatatu kwa wagombea wa nafasi mbalimbali  kunadi sera zao kwa wajumbe wa mkutano mkuu  wa TFF. Wagombea waliofunga kampeni leo ni Wallace Karia na Emmanuel Kimbe wanaonia urais,  huku wagombea nafasi ya Makamu wa Rais, Mulamu Ngh'ambi na Robert Selasela pia walikata utepe. Karia amezindua kampeni zao jijini Dar es Salaam na kueleza vipaumbele vyake 11 endapo ataingia madarakani wakati Kimbe aliyezindua kampeni mjini Mbeya sera zake ni tatu pekee. Mulamu naye amezindua kampeni Dar es Salaam na kuweka mipango yake mitatu ya kufanyia kazi endapo wapiga kura watampa ridhaa ya kuongoza TFF, huku Selasela naye akinadi sera ambazo ataombea kura kwa wanachama wenye mamlaka ya kuwaweka  madarakani. Katika uzinduzi wake Mulamu alisema kuwa, "Nitasimamia udhibiti wa fedha kuziba mianya yote ya upotevu au matumizi ambayo hayana ulazima nd...

MAMA KUWA MAKINI HOUSEGIRL ANAWEZA KUWA MKE MWENZIO

Picha
Ivi ni vibaya House girl kuolewa na baba mwenye nyumba? Ndugu msomaji wa Muungwana Blog, karibu kwenye makala hii maalumu, nimeamua kuandika habari hii ili kujaribu kupunguza mifarakano kwenye familia zetu especially familia zenye wafanyakazi wa ndani wanaojulikana kama house girl. Katika mada hii nimekuwa nikikutana na maswali mengi sana ambayo mda mwingine yalikuwa yakituchanganya hata sisi wenyewe katika kuwajibu wahusika, maswali haya malanyingi yalikuwa yakiulizwa na akina mama. Na kwa upande wa akina baba maswali yao sio mengi ukilinganisha na akina mama, sasa napenda nianze kwa kusema mambo yafuatayo ili wote twende sawa. WAJIBU WA MWANAUME KATIKA FAMILIA:  Mwanaume anawajibu wa kutimiza mahitaji yote ya msingi katika familia yake, moja ya majukumu hayo ni pamoja na kutoa pesa za matunzo ya familia yake kadri ipasavyo, kuonyesha upendo wa dhati kwa mama pamoja na watoto wake, na mambo mengineyo nk. WAJIBU WA MWANAMKE KATIKA FAMILIA:  Mwanamke ndiye mtendaji mkuu wa fa...

Mwalimu Atiwa Mbaroni kwa Kufanya Mapenzi na Mwanafunzi

Picha
Mwalimu Atiwa Mbaroni kwa Kufanya Mapenzi na Mwanafunzi wake wa Kidato cha Nne Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Igurubi, Maganga Ngassa (35) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga kwa tuhuma ya kufanya mapenzi na mwanafunzi wa miaka 17 anayesoma shule ya sekondari kidato cha nne, Kata ya Mwisi wilayani hapa. Mwendesha Mashitaka wa Polisi Igunga, Elimajid Kweyamba alidai mbele ya Hakimu Juhudi Mdonya, kwamba Julai 25, mwaka huu saa 9 alasiri katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Forest au Chacha iliyoko Mtaa wa Mwayunge mjini Igunga, kinyume na sheria za nchi, Ngassa alifanya mapenzi na mwanafunzi  mwenye umri wa miaka 17 anayesoma shule ya sekondari iliyoko Kata ya Mwisi kidato cha nne (jina linahifadhiwa).  Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 18, mwaka huu itakapotajwa tena.